Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Ni mchezo wa Fainali ya kombe la dunia, takribani watu bilioni 1 duniani wanafatilia mtanange huo.

Dakika ya 3 ya nyongeza ndani ya dakika 120, ubao ukiwa unasomeka 3-3 kwa Ufaransa na Argentina.

Ndani ya dakika 3 za nyongeza, zikiwa zimebaki sekunde 16 mtanange uishe ili waende penati, huku Leo Messi akijaribu bahati yake ya mwisho ya kutwaa kombe la dunia, ghafla mpira mrefu wa kushtukiza unapigwa kuelekea lango la Argentina.

Kolo Muani, mshambuliaji wa Ufaransa anaupokea mpira ule huku akiwa amebaki yeye na kipa Emiliano Martinez na akijua kabisa akifanikiwa kuweka mpira ule nyavuni anaipa nchi yake goli la 4 na pengine la ushindi.

Kolo Muani anaucha ule mpira unadunda kisha akipiga shuti kati ambalo kipa Martinez anafanikiwa kuzuia na mguu wake na kuinyima Ufaransa nafasi ya ushindi.

Sekunde chache baadae refa anamaliza mpira. Wanaenda mikwaju ya penati na Argentina wanaenda kutwaa ndoo ya dunia mara baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho pale Mexico mwaka 1986.

Hili tukio siwezi kulisahau maana lilibadilisha muelekeo mzima wa mechi, na tukio hili linatajwa kama moja ya save bora kuwahi kufanywa na kipa katika historia ya mashindano ya kombe la dunia.

Wewe ni tukio lipi huwezi kulisahau?

E513AE4F-81ED-4F78-BDBF-94474E888682.jpeg
 
Hilo la Muani hata yeye mwenyewe kichwani mwake haliwezi kufutika.Pia matukio kama haya hayafutiki kichwani mwangu (1) Gatuso kumkaba Ronaldo, hiyo ilikuwa AC Milan Vs Man utd
(2) Suarez kudaka mpira uliokuwa unaelekea kuwa goli, Uruguay Vs Ghana (3) World cup 2010 German Vs England Lampard anasawazisha lakini refa anakataa goli.Nadhani hiyo ndio iliwafanya waingereza wagundue goal line technology maana mpira aliopiga Lampard ulivuka mstari WA goal na kurudi ndani.
 
Hii save ya Martinez ni funga kazi maana kama Muani angeweka mpira wavuni historia ingebadilika na Messi status yake ingekua tofauti. Angelia usiku na mchana akikumbuka finali zake mbili chungu. Ya 2014 na 2016 copa America

Mm nachokumbuka ni ile kichwa alichopogiwa Marco Materraz. Kingine ni ile last second/minute goal ya Ramos uefa 2016
 
Timu zote zina point 86, huku City akiwa na tofauti ya Mabao 63 Man United akiwa na GD ya 55.

City akikipiga na QPR, Man United akigongana na Sunderland.

United alimaliza kwa ushindi wa goli moja, bao la Waza hivyo kufanya kuwa na point 89. City kang'ang'aniwa na QPR, mpaka dakika ya 90, City 1-2 QPR.

Kumbuka hii mechi ni muhimu kwa timu zote mbili. City anapaswa kushinda ili achukue ubingwa na QPR ashinde ili asishuke Daraja.

Sisi Mashabiki wa Manchester United, tupo tunashangalia kombe letu. Mechi imeshaisha tayari.

Zikaongezwa dakika 5 kufidia dakika zilizopotea. Asalaleeeh, dakika ya 92, Dzeko anasawazisha ubao. Sasa ni 2-2.

Bado matumaini kwetu ni makubwa mno. Droo hiyo isingesaidia. Ubingwa ni wetu sisi.

Dakika ya 93, La haula!. Aguero anafunga goli na kufanya kuwa 3-2.

Nilihuzunika mno. Hakika nilipata huzuni iliyo kuu. Mpaka na leo sitosahau. City anatawazwa kuwa bingwa kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo QPR aliponea kushuka baada ya Bolton kutoka sare.

Mungu naomba hili jambo lifutike kwenye kumbukumbu zangu.
 
1. Sitasahau ubora wa Oliver Khan kwenye World Cup finals 2002.
Jamaa alikuwa kafungwa goli Moja tu mpaka wanacheza fainali na Brazil, anakuja mnyama Ronaldo anamtia mbili kwenye fainali. Hakuamini mpaka akagoma kutoka golini mwisho wa game.

2. Sitasahau zile nyuso za machozi za wabrazil ile siku wanabamizwa 7 na Germany pale pale kwao. Ile game Neymar hakucheza baada ya kutenguliwa pingili ya uti wa mgongo na yule dogo Mcolombia.

3. Sitasahau ile siku Barca amekandamizwa 4-0 pale Anfield kwenye usiku wa UEFA mwaka 2019. Ile ni come-back yangu bora ya muda wote ikifuatiwa na Ile fainali Uefa final match ya AC Milan vs Liverpool 2005.
 
1. Goli la Kibu D dhidi ya Yanga 2023
2. Simba 5 Yanga 0
3. Yanga 3 Simba 0 kipindi cha kwanza, FT Yanga 3 Simba 3

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mashabiki wengi wa Barça tunalikumbuka sana hili tukio, ilikuwa UEFA 2017

Sergi Roberto anaingia kambani dakika ya 95 anaipeleka Barça robo fainali ya UEFA

1st leg: Barça 0– 4 PSG (Parc de France)
2nd leg: Barça 6– 1 PSG (Camp Noú)


FT: Barça 6–5 PSG on aggregate

What a comeback!

images (3).jpeg
 
Back
Top Bottom