Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Ni mchezo wa Fainali ya kombe la dunia, takribani watu bilioni 1 duniani wanafatilia mtanange huo.

Dakika ya 3 ya nyongeza ndani ya dakika 120, ubao ukiwa unasomeka 3-3 kwa Ufaransa na Argentina.

Ndani ya dakika 3 za nyongeza, zikiwa zimebaki sekunde 16 mtanange uishe ili waende penati, huku Leo Messi akijaribu bahati yake ya mwisho ya kutwaa kombe la dunia, ghafla mpira mrefu wa kushtukiza unapigwa kuelekea lango la Argentina.

Kolo Muani, mshambuliaji wa Ufaransa anaupokea mpira ule huku akiwa amebaki yeye na kipa Emiliano Martinez na akijua kabisa akifanikiwa kuweka mpira ule nyavuni anaipa nchi yake goli la 4 na pengine la ushindi.

Kolo Muani anaucha ule mpira unadunda kisha akipiga shuti kati ambalo kipa Martinez anafanikiwa kuzuia na mguu wake na kuinyima Ufaransa nafasi ya ushindi.

Sekunde chache baadae refa anamaliza mpira. Wanaenda mikwaju ya penati na Argentina wanaenda kutwaa ndoo ya dunia mara baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho pale Mexico mwaka 1986.

Hili tukio siwezi kulisahau maana lilibadilisha muelekeo mzima wa mechi, na tukio hili linatajwa kama moja ya save bora kuwahi kufanywa na kipa katika historia ya mashindano ya kombe la dunia.

Wewe ni tukio lipi huwezi kulisahau?

View attachment 2633541
Comeback ya Liverpool vs Barcelona 2019
 
Hilo la Muani hata yeye mwenyewe kichwani mwake haliwezi kufutika.Pia matukio kama haya hayafutiki kichwani mwangu (1) Gatuso kumkaba Ronaldo, hiyo ilikuwa AC Milan Vs Man utd
(2) Suarez kudaka mpira uliokuwa unaelekea kuwa goli, Uruguay Vs Ghana (3) World cup 2010 German Vs England Lampard anasawazisha lakini refa anakataa goli.Nadhani hiyo ndio iliwafanya waingereza wagundue goal line technology maana mpira aliopiga Lampard ulivuka mstari WA goal na kurudi ndani.
Euro ya 2012 England walikaa kimya kuhusu goal line technology baada ya wao kupigwa goli afu Johnny Terry kutoa nyavuni na referee hakuona goli mpira ukaendelea
 
Timu zote zina point 86, huku City akiwa na tofauti ya Mabao 63 Man United akiwa na GD ya 55.

City akikipiga na QPR, Man United akigongana na Sunderland.

United alimaliza kwa ushindi wa goli moja, bao la Waza hivyo kufanya kuwa na point 89. City kang'ang'aniwa na QPR, mpaka dakika ya 90, City 1-2 QPR.

Kumbuka hii mechi ni muhimu kwa timu zote mbili. City anapaswa kushinda ili achukue ubingwa na QPR ashinde ili asishuke Daraja.

Sisi Mashabiki wa Manchester United, tupo tunashangalia kombe letu. Mechi imeshaisha tayari.

Zikaongezwa dakika 5 kufidia dakika zilizopotea. Asalaleeeh, dakika ya 92, Albino KDB anasawazisha ubao. Sasa ni 2-2.

Bado matumaini kwetu ni makubwa mno. Droo hiyo isingesaidia. Ubingwa ni wetu sisi.

Dakika ya 93, La haula!. Aguero anafunga goli na kufanya kuwa 3-2.

Nilihuzunika mno. Hakika nilipata huzuni iliyo kuu. Mpaka na leo sitosahau. City anatawazwa kuwa bingwa kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo QPR aliponea kushuka baada ya Bolton kutoka sare.

Mungu naomba hili jambo lifutike kwenye kumbukumbu zangu.
Point of correction goli la kusawazisha alifunga Eden Dzeko kupitia mpira wa kona iliyopigwa na david silva. Game ikaenda 2-2. Then baada ya hapo Aguero ndio akafunga goli la tatu Assist kutoka kwa Baloteli. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa goli la kwanza la city pia lilifungwa na Zabaleta nafikiri ndio lilikua goli la kwanza ndani ya huu mchezo kabla ya Qpr kusawazisha na kuongeza.
 
Sitasahau jinsi manyumbu walivyokung'utwa goli 7-0 dhidi ya Liverpool, kama wamesimama.
 
Point of correction goli la kusawazisha alifunga Eden Dzeko kupitia mpira wa kona iliyopigwa na david silva. Game ikaenda 2-2. Then baada ya hapo Aguero ndio akafunga goli la tatu Assist kutoka kwa Baloteli. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa goli la kwanza la city pia lilifungwa na Zabaleta nafikiri ndio lilikua goli la kwanza ndani ya huu mchezo kabla ya Qpr kusawazisha na kuongeza.
Hakika Mkuu. Ni Dzeko.... Hivi si huwa wanafanana hao na KDB?
 
Mashabiki wengi wa Barça tunalikumbuka sana hili tukio, ilikuwa UEFA 2017

Sergi Roberto anaingia kambani dakika ya 95 anaipeleka Barça robo fainali ya UEFA

1st leg: Barça 0– 4 PSG (Parc de France)
2nd leg: Barça 6– 1 PSG (Camp Noú)

FT: Barça 6–5 PSG on aggregate

What a comeback!

View attachment 2633637
Hii mechi mlibebwa mkabebeka
 
Timu zote zina point 86, huku City akiwa na tofauti ya Mabao 63 Man United akiwa na GD ya 55.

City akikipiga na QPR, Man United akigongana na Sunderland.

United alimaliza kwa ushindi wa goli moja, bao la Waza hivyo kufanya kuwa na point 89. City kang'ang'aniwa na QPR, mpaka dakika ya 90, City 1-2 QPR.

Kumbuka hii mechi ni muhimu kwa timu zote mbili. City anapaswa kushinda ili achukue ubingwa na QPR ashinde ili asishuke Daraja.

Sisi Mashabiki wa Manchester United, tupo tunashangalia kombe letu. Mechi imeshaisha tayari.

Zikaongezwa dakika 5 kufidia dakika zilizopotea. Asalaleeeh, dakika ya 92, Albino KDB anasawazisha ubao. Sasa ni 2-2.

Bado matumaini kwetu ni makubwa mno. Droo hiyo isingesaidia. Ubingwa ni wetu sisi.

Dakika ya 93, La haula!. Aguero anafunga goli na kufanya kuwa 3-2.

Nilihuzunika mno. Hakika nilipata huzuni iliyo kuu. Mpaka na leo sitosahau. City anatawazwa kuwa bingwa kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo QPR aliponea kushuka baada ya Bolton kutoka sare.

Mungu naomba hili jambo lifutike kwenye kumbukumbu zangu.
Mkuu
Goal alisawazisha Eden Dzeko sio haji manara (kdb)
 
[emoji23][emoji23][emoji23] asenane ashawahi pigwa 8 na manyumbu haikutosha waka pigwa 10 na Bayern uefa
images (1).jpg
 
Ni mchezo wa Fainali ya kombe la dunia, takribani watu bilioni 1 duniani wanafatilia mtanange huo.

Dakika ya 3 ya nyongeza ndani ya dakika 120, ubao ukiwa unasomeka 3-3 kwa Ufaransa na Argentina.

Ndani ya dakika 3 za nyongeza, zikiwa zimebaki sekunde 16 mtanange uishe ili waende penati, huku Leo Messi akijaribu bahati yake ya mwisho ya kutwaa kombe la dunia, ghafla mpira mrefu wa kushtukiza unapigwa kuelekea lango la Argentina.

Kolo Muani, mshambuliaji wa Ufaransa anaupokea mpira ule huku akiwa amebaki yeye na kipa Emiliano Martinez na akijua kabisa akifanikiwa kuweka mpira ule nyavuni anaipa nchi yake goli la 4 na pengine la ushindi.

Kolo Muani anaucha ule mpira unadunda kisha akipiga shuti kati ambalo kipa Martinez anafanikiwa kuzuia na mguu wake na kuinyima Ufaransa nafasi ya ushindi.

Sekunde chache baadae refa anamaliza mpira. Wanaenda mikwaju ya penati na Argentina wanaenda kutwaa ndoo ya dunia mara baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho pale Mexico mwaka 1986.

Hili tukio siwezi kulisahau maana lilibadilisha muelekeo mzima wa mechi, na tukio hili linatajwa kama moja ya save bora kuwahi kufanywa na kipa katika historia ya mashindano ya kombe la dunia.

Wewe ni tukio lipi huwezi kulisahau?

View attachment 2633541
Kwa gharama yoyote ilibidi Argentina awe bingwa.

Hili wala halikuhitaji mjadala.

Ingawa niliona kabisa ufaransa alistahili. Sijui tu ni uzembe gani.....???
 
UEFA 2012
BAYERN MUNICH vs CHELSEA
penalty shout-out
Master wao Bastian Shwaztaiger anakosa tuta afu drogba akamaliza kazi,
What a moment!

WORLD CUP 2006
ITALY vs FRANCE
penalty shout-out
Mtaalamu wao france trezeguet anakosa tuta na Grosso anapiga penati kawe_mbagala, imoooo
What a coincidence!!

UEFA FINAL 2011
FC BARCA vs MANJESTA YUNAITED
ilipigwa mbungi mpaka babu fergie pete ilitetemeka ikataka kutoka, after match babu alisema "tokea nianze kufundisha mpira sijawahi kutana na timu ya hatari kama barca hii"
 
Back
Top Bottom