Tukio gani la football liliwahi kukutoa machozi

steven gerrard anateleza na demba ba anafunga ,chels na liver
 
Mechi ya Tanzania 0 - 5 Brazil niliumia sana, Ila nikaumia zaidi anko ngassa alivokosa goli la wazi kabisa
Mkuu kumbukukumbu zako Bado matokeo ilyalikuwa ni 1-5 tulifungwa sio bila maana goli la Tanzania la kichwa lilishangiliwa kwa nguvu sana maana kikwete alinyenyuka kana kwamba tumeshinda game... Ile mechi hakuna aliyeumia maana wote tulijua tunakula kichapo tu
 
La Asamoah Gyan ile robo fainal siatasahau nililiia yaa kichwa kiliuma maana tulikua shule gals tupu tumeenda kutizama hukooo alaf vile, from there nikasema nitajifunza kuupotezea ikaja yanga kufungwa tano bila mara misukosuko ya arsenal akah nikasema isiwe tabu. Saivi moyo unatulia sana hata timu nizipendazo zikifungwa, labda iwe mech na mahasimu hasa
 
Pamba vs Malindi Abdu Malaika anafunga goli la penati golikipa marehemu Paul Rwechungura anaenda upande mwingine ma mpira unaenda upande mwingineo Malindi wanatawazwa ubingwa Wa muungano... Mji wa mwanza unakuwa kimya tupu.. Nilisikiliza on radio chozi lilinitoka.... Ndio my team sipendi Yanga Wala Simba... Ila Red star au nyota nyekundu niliipenda pia
 
Mzee alitununulia gozi jamaa wa darasa la 6 wakanishauri nliliete shuleni mi nikiwa darasa la nne kuna mechi mwaka 1991 nikaenda nalo kwa ahadi kuwa watanipanga hasa kipindi cha pili. Mpaka dk 90 zinaisha nipo nje tu jamaa wenyewe wanasata gozi langu. Baada ya kipyenga kupulizwa nlikamata mpira wangu nikaweka kwapan huku nikilia sana.
 
WC-1998:France vs Brazil-Final Results 3-0............Mwanzo wa kumchukia Zidane...akaja kutonesha kidonda 2006..hapa ilibidi nimpende tu(can't beat them,join them)
siku Ronaldo De Lima alipotangaza kwa masikitiko makubwa ana ugonjwa wa Hypothyroidism.
 
Ligi ya kuku mtaanini kwetu {2006 Tabora}, pale tumeshinda fainali tujinyakulie kuku, lakini wababe wa timu pinzani walimnyonga kuku pale pale uwanjani... [emoji27]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kombe la dunia 2010,Mechi ya Ghana vs Uruguay. Suarez anadaka mpira na Gyan anakosa penalti.
 
Barca anateseka sana akikutana na blues hata messi anajua hajawai kufunga hata penalty japokuwa alipata nafasi ya kupiga
NB:Siku Messi akiifunga Chelsea kwenye uefa ntauzunika sana
weka head to head tangu waanze na ikitokea yokobus kaiongoza BARCA iwe kimagol au kwa kuifunga MIMI NAHAMIA THE BLAUZ
 
Simba kung'oa viti taifa,wamenifanya hata mgeni shabiki wa simba akija home kwangu nimtandikie mkeka nje aketi. Sitting room never....
 
Siku Manchester City kaja Oldtrafford Aguero akatangulia kufunga nkajua tushapoteza,ila tukaja kuwanyuka 3-1 niliona machozi yanatoka huku nkieka wide smile
 
Dah yani wote tungekua kama wewe hizi timu zetu za kina Majimaji zingekua mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…