Tukio gani la football liliwahi kukutoa machozi

Me nililia sana nafikiri mwaka 1994 yanga alipigwa nne na simba.ile yanga ya constatine kimanda na lunyamila na huku simba kina duwa said ndio walikuwa wanatokezea.sisi ndio tulikuwa wakali nilikuwa bado mdogo nilia sana hadi mtaa mzima ukawa unanitania
 
Mpira wakati mwingine kama mapenzi.ukiyachukulia serious sana yatakachokufanya utakuja kujuta.
 
[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
Umenikumbusha machungu mkuu[emoji24]
 
Man U vs Chelsea, Ivanovic na Torres wanapewa red cad then Chicharito anafunga goli la offside...kwakweli niliumia sana tena niliapa kutokua mnazi wa mpira na ningekua karibu na refa ningemfanya kitu kibaya sana. Football is not a fear game always
 
Mwenzio ile siku nilikuwa na kibunda cha tiketi na niliwaliika jamaa kutoka Morogoro kuja kucheck ile game.

Usisahau pia nilikuwa na shemeji yako pembeni. Tulikula jezi ya TAIFA KIJIJI kizima.

Kama unakumbuka, kabla ya mechi ile, tulipiga friend match na UG, nadhani alikuwa KIGGY MAKASI aliwanyamazisha UG kimoja. Maximo ktk ubora wake.

Hiyo mechi na WAMAKONDE, kuna mtu wao anaitwa TICO TICO, alitufanya vibaya. Sina hamu.
 
Kuna pahala umesema PAN AFRICAN, na baadae ukasema AFRICAN SPORTS. Kwa kuwa unamzugumzia VICTOR NKANWA, bila shaka ni AFRICAN SPORTS ya Tanga
 
holland vs italy euro nusu finali 2000. holland imejaa vijana wangu wa barca na alsenal. mpira mwingi sana huku italy wamepaki basi. patrick cruvet anakosa penati. jap stam anapaisha kwa mashabiki. mpira sio kitu kidogo.siku hiyo kipa buffon hakudaka akacheza kipa anaitwa toldo kikwazo balaa.
ila furaha ni fainal uefa man U anapigwa vizuri na barca huku fegi anakufa kwa kideri benchini
 
Kuna pahala umesema PAN AFRICAN, na baadae ukasema AFRICAN SPORTS. Kwa kuwa unamzugumzia VICTOR NKANWA, bila shaka ni AFRICAN SPORTS ya Tanga

Asante mkuu ni African sport kwani victor mkanwa hajawahi kuchezea yanga B Pan Africa
 
Dah yani wote tungekua kama wewe hizi timu zetu za kina Majimaji zingekua mbali sana.
Mkuu hiyo timu nilikuwa naifeel sana... Primary ilikuwa ni issue kuchezea upande Wa Yanga au Simba so nilikuwa neutral leo nikichezea Simba kesho Yanga nilikuwa lazima nibadilishe upande... Japo wengine walikasilika na nikaona vipi sichezi maana kufunga kwangu ilikuwa ni lazima nilitamani siku moja niichezee Pamba tatizo mkoa tofauti... Niliishi ila Pamba kila walipokuwa wakija Dar mazoezi walikuwa wakichezea Mnazi mmoja Asubuhi lazima niwacheki and then niende shule kile kikosi cha kina Marshah timu nzima nilikuwa nawaona yaani ilikuwa raha burudani...
 

Mkuu ume nikumbusha mbali Sana miaka ya themanini watoto wa TMK walikuwa na uwezo wa kukutajia first eleven ya timu zote za ligi kuu kuanzia yanga,Simba,nyota nyekundu,cost union,African sport,reli,mecco,Tukuyu star,pamba nk
 
Niliumia sana siku wanangu wenyewe deportivo la coruna walipofungwa 1 -0 na fc porto kwenye nusu fainali ya uefa 2004 game ya marudiano,ikumbukwe walitoka kumpiga ac milan 4-0 baada ya kupoteza mechi ya kwanza 4-1,ac milan ya kina sheva,Nesta,Maldini,seedof,gattuso,etc
Nilihuzunika sana sana,jamaa hawajarudi tena,kikosi kilikuwa hivi:


Deportivo Coruna: 1-Jose Molina; 2-Manuel Pablo, 4-Noureddine Naybet, 5-Cesar, 3-Enrique Romero; 18-Victor, 23-Aldo Duscher, 8-Sergio, 19-Albert Luque; 21-Juan Carlos Valeron; 7-Walter Pandiani
Subs: Munua, Capdevila, Fran, Scaloni, Djalminha, Pablo Amo, Tristan.
 
Juventus kutoka draw na kusababisha nikapoteza hela ya matumizi chuoni 2013
[emoji1] [emoji1] [emoji1] mkuu uliona dunia imekua nyekundu[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Arsenal kutolewa robo final na Barcelona km scosei hiii iliniumaaaaaaaa sana walaaaaaa stasahau
 
World cup 2014 fainal, Argentina vs Germany. Niliumia sana king Messi aliposhindwa kuinua kwapa. Hii inapelekea kumwa under rate king wakati ukerli hamaa ni nourma.

Niliumia zaidi nilipowaona albiceleste wakitiririsha machozi. Nililia pamoja nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…