secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Katika maisha kuna muda akili zetu zinasahau vitu vidogo vidogo tunavyovijua ila baada ya dakika chache kumbukumbu hurudi.
Kuna stori moja nilishawahi kuisoma humu JF mtu mmoja alienda msituni kutafuta kuni na shoka lake begani lakini alipofika kule alilala kwa dakika 15, alipoamka alianza kutafuta shoka lake aina ya inkosekaz kuanzia saa 1 asubuhi hadi sa 11 jioni kumbe shoka alikuwa nalo begani, ndiyo maana kuna msemo mmoja unasema "utakiona cha mtema kuni".
Binafsi nikiwa mdogo nilitumwa dukani kununua kilo ya mchele, nilipofika nikasahau neno 'kilo' nilikaa takribani dakika 15 kulikumbuka hili neno lakini nikashindwa, nikamua kuingia dukani nikamwambia muuza duka anipe lita moja ya mchele jamaa alinielewa lakini alicheka mpaka akaanza kukohoa.
Ahlan wasahlan!