Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
 
Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri .
Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.

Mungu yupo na anaishi. Leo Kesho na milele najuta Sana kuishi majira ya UPOFU ila now I'm healed .

God is real
Kupata zero
Kupata one
Kukosa Kazi
Kupata kazi
Kuajiriwa
Kujiajiri

From Gheto to My own empire
From Corolla to V8

👏👏God never get too big
 
Una experience nzuri ya haya maisha mkuu
 
Nimeponea kifo mara kadhaa kwenye ajali . Ya kwanza niligongwa na bike ya wajeda nadhani nikiwa mdogo sana mwanzoni mwa miaka ya 2000 thanks god niliponea. Nyingine nikiwa dom tuliigonga semi trailer kwa nyuma pale kwenye mataa ya jamhuri tukiwa kwenye harrier. Ashukuriwe mungu ile trailer pale nyuma ilikuwa na ngao hivi la sivyo tulikuwa tunakusanywa kule chini ya tairi za semi. Tulitoka safe. Lakini nasikitika kusema the same guy alekuwa anaendesha haikupita miezi mitatu mbele alisababisha ajali tena iliyogharimu maisha ya mama na watoto 2 . Mmoja amekuwa crippled. It was sad kwa kweli.
 
Mungu yupo na anaishi. Leo Kesho na milele najuta Sana kuishi majira ya UPOFU ila now I'm healed .

God is real
Kupata zero
Kupata one
Kukosa Kazi
Kupata kazi
Kuajiriwa
Kujiajiri

From Gheto to My own empire
From Corolla to V8

👏👏God never get too big
Mkuu tunafanaa kasoro kwenye baadhi ya mambo.Mungu anakusaidia pale ww uoni mbele wala nyuma na kila mtu kakutenga.
 
Nimeponea kifo mara kadhaa kwenye ajali . Ya kwanza niligongwa na bike ya wajeda nadhani nikiwa mdogo sana mwanzoni mwa miaka ya 2000 thanks god niliponea. Nyingine nikiwa dom tuliigonga semi trailer kwa nyuma pale kwenye mataa ya jamhuri tukiwa kwenye harrier. Ashukuriwe mungu ile trailer pale nyuma ilikuwa na ngao hivi la sivyo tulikuwa tunakusanywa kule chini ya tairi za semi. Tulitoka safe. Lakini nasikitika kusema the same guy alekuwa anaendesha haikupita miezi mitatu mbele alisababisha ajali tena iliyogharimu maisha ya mama na watoto 2 . Mmoja amekuwa crippled. It was sad kwa kweli.
Asee iyo Ajali ya kwanza ni kama Mungu alikuwa anampa tahadhari awe makini anapokuwa barabarani
 
Binafsi Mungu anajidhihirisha karibu kila siku.

Mara kadhaa nakaa naunganisha matukio moja baada ya lingine, na napata picha ya umuhimu wa kila jambo linalotokea katika maisha yangu ( la kufurahisha sana au kuacha alama ya maumivu) na mchango wa kila tukio katika kunifikasha hapa nilipo.

Hakika hesabu za Mungu ni kubwa sana sana. Kwa kulitambua hili sehemu kubwa ya maombi yangu huwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kuomba rehema.

God's arithmetics are of Higher and Peculiar Degree. Just trust the process and stay greatful before Him.
 
Nilikuta msg za mapenz anachat na rafiki yangu akaninyakua cm akafuta ushahidi akakataa hana mahusiano nae, Mungu alivyomkuu baada ya wiki 1, wakajirecord wanaongea mambo ya mapenz na jinsi mechi ilivyokua na hawakujua kama cm inarecord....nikaja sikiliza kilakitu
 
Enzi hizo nikiwa form three.
Usiku mmoja wa mwezi wa sita nikiwa najisomea ghetto baridi kali, humo ndani kulikuwa na jiko la mkaa mala kibatari kikazima. Nikaanza kutafuta karatasi Ili nikiwashe bahati nzuri nikapata kipande Cha karatasi. Sasa Kila nikiwasha lile karatasi kwenye jiko haliwaki wala kuonyesha dalili ya kuwaka. Nikatafuta karatasi lingine kuwasha likawaka huku lile karatasi la maajabu nimeshika mkono wa kushoto. Baada ya kuwasha kibatari mala Moja nikaangalia kile kipande Cha karatasi nikashangaa kumbe ulikuwa ukurasa wa BIBLE
 
Haukuchoma vizuri chief au ulikuwa huoni.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Darasani maisha yote nilikuwa natokea wa 25 na kuendelea huko, siku ya mtihani mzee namuona anaongea na teacher. Hafla naona mzee kampa teacher kitu nae teacher kaweka mfukoni alicho pewa.

Mwanangu matokeo yamekuja naambiwa eti nimetokea wa 3 🤣🤣.

Hapo nikasema Mungu anatuona kiazi mimi leo nime kuwa wa 3, halafu teacher alikuwa ananipa majibu muhuni yule😂😂
 
Back
Top Bottom