Katika mjadala huo sikuwepo ndio maana nabisha kutokana na presentation yako.
Ina bidi habari ijitosheleze maana hata baada ya miaka 100, yasiposemwa wazi wazi yale ambayo hayasemwi, watu wataendelea kubisha.
WeWe MSA upo kutetea kile ulichohadithiwa na wazee wako, siku haupo je nani atatetea.
Maana ukisoma presentation yako , maswali ya kujiuiza bado yapo.
Naje baada ya Abdul na Ally sykes kutunukiwa Medali ya mwenge wa Uhuru na Serikali, was it an admissiob of fault?
Na je hili limekuwa documented.
Na siamini kuwa Abdu na Aly Sykes ndio watu pekee waliostahili medali hiyo.
Jidu...
Hakika hukuwepo na wengi hawakuwapo na kila siku wanakuja na tunaanza mjadala upya nami huwa siwagutui kwa sababu napenda kusomesha.
Mimi sikuhadithiwa tu mimi nimeishi ndani ya historia hii na nimetafiti na kusoma nyaraka nyingi za wakati ule.
Maktaba yangu imesifiwa na waandishi wa kitabu cha Julius Nyerere.
Usiseme najipigia tarumbeta hawa waaandishi wa kitabu cha Mwalimu wakiongozwa na Prof. Shivji wametaja Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu bora walizopitia wakati wa utafiti wa kitabu cha Nyerere nazo ni za Dr. Salim Ahmed Salim Brig. Hashim Mbita ni hii yangu.
Zaidi wameaniambia kuwa katika watu wanaomjua Nyerere mimi nimetia fora.
Kwa nini nisitie fora ilhali wazee wangu ndiyo waliompokea na kuwa na yeye hadi uhuru umepatikana?
Mimi najua hadi ''brand,'' ya sigara aliyokuwa anavuta Nyerere.
Huyu ni Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya kiongozi katika TAA na mwanachama wa TANU kadi yake No. 6 huyo kushoto ni mimi hapo ni nyumbani kwake Ruiru, Nairobi mwaka wa 1972.
Huu ndiyo upeo wangu wa kuijua TANU na viongozi wake ndipo ninposema wazee wangu naomba unielewe.
Dome alikuwa mmoja katika watu ambao mimi walinijua katika utoto wangu.
Huyu ni Dennis Phmbeah Mnyasa kadi yake ya TANU No. 5.
Katika uchaguzi wa 1953 Dennis Phombeah alihangaika sana kumfanyia kampeni Nyerere ashinde kwa kuwa hakuwa katika Inner Circle hakuwa anajua kuwa mipango imeshakamilika na Nyerere atashinda uchaguzi ule.
Kaka usifanye maskhara mimi naijua historia ya TANU.
Kulia ni Ilyassar Abdulwahid Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes, Mohamed Said (nimeshika Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa Abdul Sykes), Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes 2017.
Hakika wako wengi walistahili kupewa medali kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Hamza Mwapachu, Bi. Tatu bint Mzee, Steven Mhando, Zuberi Mtemvu kwa kuwataja wachache.
Muthaiga Club, Nairobi na Ally Sykes 1989 hapa Nairobi kuna historia ya pekee katika harakati za kuunganisha TAA na KAU iliyopekea Abdul Sykes kukutana na Kenyatta Nairobi mwaka wa 1950 Kenyatta akiwa na Peter Mbiu Koinange, Kungu Karumba, Paul Ngei, Bildad Kaggia timu nzima ya Kapenguria Six.
Unataka nikuwekee hapa ripoti ya kikachero ya Special Branch kuhusu mkutano huu?
Kaka narudia tena mimi naijua historia ya wazee wangu kuna kitu wazee wangu walikiona kwangu.
Wazee wangu walikuwa watu hodari mashujaa na walipambana na ukoloni kwa dhati ya nafsi zao na wakatoa na mali zao ili Tanganyika iwe huru.
Hawakunificha jambo wamenieleza mengi mengine si ya kuandikwa sasa wakati wake bado.