Tukio gani ukilikumbuka unacheka tu mwenyewe?

Tukio gani ukilikumbuka unacheka tu mwenyewe?

ANKO JEI

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Posts
1,302
Reaction score
2,462
Maisha yana matukio mengi ambayo yana muunganiko wa moja kwa moja kwenye hisia zetu, hivyo unapoyakumbuka unaweza patwa na hisia ya huzuni au furaha.

Hivyo leo tukumbuke matukio ambayo tuliwahi yashuhudia yakatuchekesha,lakini hata baada ya siku, wiki, miezi au miaka kupita bado matukio hayo hutuchekesha tunapoyakumbuka hata tunapokuwa peke yetu chumbani, njiani au chooni.

Binafsi kuna matukio mawili huwa yananichekesha sana kila ninapoyakumbuka.

TUKIO LA KWANZA
Mwaka 2018 nilikua katika harakati zangu za kununua matisheti ya buku jero, pale karume, nilipomaliza nikavuka upande wa pili, pale wanapouza mabegi begi nikawa nasubiri gari ya Mabibo niirukie nirudi home.

Sasa kuna shehe mmoja alikua amekula kanzu nyeupe safi inayong'ara kama umetoka dukani jana. Sasa kuna ile mitaro mikubwa sana ya kupitisha maji taka, na shehe akawa anataka avuke bara bara kwa haraka, bahati mbaya akasahau kuwa mavaa kanzu na inabidi aikunjie kwa juu ili aweze kukimbia vema na kuruka ile mitaro. Hivyo shehe akajaribu kuruka ule mtaro, aisee ndugu msomaji kanzu ilimchota ngwara, shehe mzima mzima kaingia mtaroni mpaka akapotelea, nilishtuka sana lakini shehe alivyotoka ndani ya mtaro akiwa mzima wa afya aisee nilijikuta nacheka kila nikikumbuka hahahhah aisee shehe alikimbilia karume sokoni kutafuta hifadhi.

TUKIO LA PILI
kipindi nipo sekondari shule ya bweni, nilikua na tabia ya kudoji bwenini tukiwa na wana kibao wenye tabia kama zangu, kikubwa tulikua tukicheza karata na kupiga soga.

Sasa ilikua lazima awepo anaepiga chabo kuangalia kama kuna mwalimu anakuja,sasa siku hiyo kumbe walimu kama wanne hivi wamezunguka njia nyingine wakitaka kutuwinda.Tumekuja kushtuka wapo karibu sana na bweni, hivyo mpiga chabo alivyotushtua, ilikua pata shika.

Kila mmoja alikimbilia alikojua, sasa mimi nikakimbilia chooni nijifanye nilikuja kujisaidia haja kubwa,mwalimu akausoma mchezo akaja hadi vyooni akawa anafungua mlango mmoja baada ya mwingine, me nikawa nishavua suruali nimekaa mkao kabisa kama najisaidia, sasa mwamba choo cha pili alisahau kuvua suruali so akawa amechuchumaa huku amechomekea.

Me nasikia tu mwalimu anafungua milango ya karibu, mara akafungua mlango ambao niko mimi akanambia "dogo maliza fasta kimbia darasani"

Nikajua tu nimepona, sasa wakati namwaga nazuga kujisafisha ticha akaenda mlango alipo jamaa, akafungua akamkuta mwana kachuchumaa. Nikawa nasikia maongezi

Ticha akamuuliza jamaa, unafanya nini? Jamaa kwa woga akajibu "najisaidia" ticha akacheka sana akauliza "dogo unajinyea au? Unajisaidiaje umechomekea?" jamaa akakosa jibu akatolewa nje akila kichapo me nikapita kama siwajui huku kicheko kimenibana sana.

Tafadhali share nawe ni tukio gani lilikuchekesha na linakuchekesha mpaka leo.
 
Kuna siku moja nilikuwa natoka shule na wanangu kipindi hiko primary story za hapa na pale ulimladi tufawahi kufika nyumbani. Punde kidogo akatokea mzee mmoja ambaye alikuwa amekimbiza Sana baiskeli na ile sehemu ilikuwa Ina mteremko flani ivi so alikuwa stidi sanaaaa Mara ikatokea gari kwa kushtukiza mbeleee yule mzee akakosa balance akadondoka vibaya sana. Ikabidi tuende kumnyenyua juu tukamuweka sawa akasema hajaumia yupo ok.

Tukamuacha zetu tukaendelea na michezo yetu huko tunaelekea nyumbani Kama kawaida. Kuna uchochoro tukawa tunapita tukamkute yule yule mzee analiaaaa tulijikuta tunacheka badala ya kumuonea hurumaa
 
Yompa's last salute
FB_IMG_16136945709194630.jpg
 
Nilitekenywa hadi nikajikojolea.....!!!!!!

Halafu nikaanza kulia baada ya kujikojolea, waliokuja kunibembeleza wakaanza kunitekenya tena.......

Nikaanza kucheka tena huku machozi yanatoka....!!!
 
Shule yetu yenye boarding ilikuwa imezungukwa na miti,mara kwa mara mwalimu wa nidhamu alikuwa anakuja kuwakurupusha watu ahsubuhi watu waende madarasani.Yule mwalimu kila akija kuna wale watukutu wanaanza kumwita mwalimu jina lake kwa sauti mwafuuuu! Akiiitika wanasema k***m*e!,halafu wanapotelea kwenye msitu huko wanaendelea kumwita mwafuu!. yule mwalimu alikuwa haji Kule kwenye msitu.Tabia hii wakaanza kuiiga hadi wadogo zetu form 1.

Kuna siku ticha kama kawaida kaja kutimua watu ahsubuhi waende darasani watu kama kawaida yao wakaanza mwafuuu!,katika hawa waliokuwa wanamuita jina ticha kwa nguvu ni dogo mmoja wa form 1 siku hiyo dogo alijificha nyuma ya ukuta wa chooni kakazana kuitwa mwafuuu! Kumbe ticha kamzunguka yuko nyuma yake,dogo hana habari amekazana mwaafu! Ticha akanyata mpaka alipofika karibu yake kisha ticha akaitika naam! dogo kugeuka nyuma acheki nani kaitika anakutana na ticha mwafu,nahisi dogo alijikojolea siku ile kwa hofu.Dogo aliruka kichura mpaka staff kwenye kuchukua zawadi zake huko za utovu wa nidhamu.
 
nikifikiria kuwa tupige nyungu ili kutibu korona wakatihuohuo tunaambiwa korona iliondoka kwa nguvu ya sala za cku tatu hua nacheka sana
 
Hahahaha mzee aliamua kwenda kulilia uchochoroni.
Kuna siku moja nilikuwa natoka shule na wanangu kipindi hiko primary story za hapa na pale ulimladi tufawahi kufika nyumbani. Punde kidogo akatokea mzee mmoja ambaye alikuwa amekimbiza Sana baiskeli na ile sehemu ilikuwa Ina mteremko flani ivi so alikuwa stidi sanaaaa Mara ikatokea gari kwa kushtukiza mbeleee yule mzee akakosa balance akadondoka vibaya sana. Ikabidi tuende kumnyenyua juu tukamuweka sawa akasema hajaumia yupo ok.

Tukamuacha zetu tukaendelea na michezo yetu huko tunaelekea nyumbani Kama kawaida. Kuna uchochoro tukawa tunapita tukamkute yule yule mzee analiaaaa tulijikuta tunacheka badala ya kumuonea hurumaa
 
Nilitekenywa hadi nikajikojolea.....!!!!!!

Halafu nikaanza kulia baada ya kujikojolea, waliokuja kunibembeleza wakaanza kunitekenya tena.......

Nikaanza kucheka tena huku machozi yanatoka....!!!
Hahahah kasie matata
 
Shule yetu yenye boarding ilikuwa imezungukwa na miti,mara kwa mara mwalimu wa nidhamu alikuwa anakuja kuwakurupusha watu ahsubuhi watu waende madarasani.Yule mwalimu kila akija kuna wale watukutu wanaanza kumwita mwalimu jina lake kwa sauti mwafuuuu! Akiiitika wanasema k***m*e!,halafu wanapotelea kwenye msitu huko wanaendelea kumwita mwafuu!. yule mwalimu alikuwa haji Kule kwenye msitu.Tabia hii wakaanza kuiiga hadi wadogo zetu form 1.

Kuna siku ticha kama kawaida kaja kutimua watu ahsubuhi waende darasani watu kama kawaida yao wakaanza mwafuuu!,katika hawa waliokuwa wanamuita jina ticha kwa nguvu ni dogo mmoja wa form 1 siku hiyo dogo alijificha nyuma ya ukuta wa chooni kakazana kuitwa mwafuuu! Kumbe ticha kamzunguka yuko nyuma yake,dogo hana habari amekazana mwaafu! Ticha akanyata mpaka alipofika karibu yake kisha ticha akaitika naam! dogo kugeuka nyuma acheki nani kaitika anakutana na ticha mwafu,nahisi dogo alijikojolea siku ile kwa hofu.Dogo aliruka kichura mpaka staff kwenye kuchukua zawadi zake huko za utovu wa nidhamu.
Hahhahhaa mwafuu alimkuta dogo eneo la tukio kabisa akiita hahha
 
Back
Top Bottom