Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Nomadix

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
2,411
Reaction score
6,646
Habari wakuu
Mara ya kwanza kujiunga na huduma za kibenki nilienda kwenye tawi la benki wakanisajili ikafika mda wa kufanya kadi iwe active.
Nimeenda kwenye ATM na yule mhudumu akaiweka kadi ndani ya ATM ananiambia chagua lugha, me hapo hata sijui wanabonyeza wapi, akanionesha zile button za pembeni nikachagua, akanambia bonyeza hapa nikabonyeza, akasema weka namba ya siri nikaanza kuijaza.

Sasa yeye akatoka nimemaliza akakawia kuja. Namsubiri mara nashangaa kadi inamezwa nikamuita nikamuuliza mbona kadi imedumbukia tena, akasema aisee ungeitoa dah, me nikamwambia sasa hukuniambia, nilikaa pale saa zima nasubiri wailete dah!

Mara ya pili, nimeenda ATM pekeangu kufika kumbe ile ATM ni ya touchscreen haina buttons za pembeni zipo za namba tu maandishi yale ya pembeni kumbe unatouch, duh nikadata nje kuna bonge la foleni wanasubiri nitoke, naweka kadi naweka PIN nasubiri hola! duh nikaona nitoke hapa nishatolewa ushamba, hata nikaona kuuliza watanicheka nikaenda kutoa kwa wakala, haha dah!
ushamba mzigo
 
Mimi nilikuwa najiona mzungu kinoma yaani najua english siku nikaenda jukwaani kupiga inglish sasa ile kusema "several times(severo taims)" nikasema "severali taimes"
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]ung'eng'e huwa nikipengele skuli wengine walikuwa wanatamka:
muscle (msukule)
tongue (tongwu)
 
Sijaona ushamba hapa!,yaan kutokujua kitu ndio ushamba?! Hata hao wahudumu wenyewe walifundishwa jinsi ya kutumia hizo ATM hakuna aliyezaliwa anajua
 
Mimi nilikuwa najiona mzungu kinoma yaani najua english siku nikaenda jukwaani kupiga inglish sasa ile kusema "several times(severo taims)" nikasema "severali taimes"
Kuna sister wa kihindi pale skuli alikua na tabia ya kufinya sikio na funguo ukifanya kosa.

Siku hiyo ilikua mwanetu mmoja alizingua, sasa ile sister anataka kumfinya tukasikia mchizi anajitetea, "Sister my ear is sick.", akimaanisha sikio langy linauma.

Mwingine assemble alitajwa na prefect kwa kosa ambalo hajafanya yeye. Kwa ghadhabu akaropoka " Teacher Teacher he is mixing me."

Noma sana English.
 
kipindi flani mimi mshamba wa wanawake sekondari huko

natongoza binti flani whatsapp akanichomolea basi nikamwambia 'please let's be friends'

akascreenshot ile chat akaiweka status na emoji ya kicheko

aisee niliumia hakuna mfano aisee.
 
πŸ˜€ πŸ˜€ haha nakumbuka nilikua nikikuta teacher naomba kuingia class, nasema
Pitisha mageti (please teacher may I get in)
 
Me ilikuwa ni kitambo nilikuwa bado sijui nafasi za kwenye mpira najua tu kipa ni namba moja ila wengine najua ni mabeki, viungo na washambuliaji ila sijui namba zao
Hivyo nikaitwa kucheza nikauliza we unacheza namba ngapi nikasema winga namba nane, jamaa akauliza nini ! nikarudia tena bila wasi wasi basi hapo ilikuwa ni kicheko dakika kama tano nachekwa tu
 
Mimi mwenyewe nilienda Dom kwa mjomba wangu wakaniachia mkate na lile coca kubwa la familia .Nikawa na kikombe changu pembeni namimina nakunywa huku nabunya na mkate wangu laini.Nikamaliza vyote mkate na lile coca babalao.
Ya pili ni tea bag tulienda sehemu nikakafyeka kwa meno kale kakamba toboa vile vimajani mimina koroga kwenye maji.
Wenyeji wangu wakabaki wametumbua macho tu.
Oooi.
 
Umenikumbusha dogo mmoja alikuwa anamwambia mwalimu mwenzake anamng'ata

Alisema "teacher this boy is ng'at me"
 
kipindi flani mimi mshamba wa wanawake sekondari huko

natongoza binti flani whatsapp akanichomolea basi nikamwambia 'please let's be friends'

akascreenshot ile chat akaiweka status na emoji ya kicheko

aisee niliumia hakuna mfano aisee.
[emoji1787]out of mada umenikumbusha mambo ya screenshot
kuna manzi mmoja ni rafiki alikuwa ananiomba hela whatsapp
Yeye: Naomba 5k kama unayo
Me: aah we 5k yote io
Yeye: acha ubahili
Me: kama ni ubahili jamba ukalale
Yeye: puuh!
Nikascreenshot nikapost alicheka sana
 
[emoji1787] maskini katea bag
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…