Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

We braza ni mshamba sana
Ushamba ni pamoja na kutokua na akili ya kujiongeza na kutojua mambo kadhaa madogo lakini muhimu.

Mimi nikiwa kidato cha kwanza bibi yangu alinipa kadi nikatoe pesa ATM, akanipa na namba ya siri ilhali sijui wala sijawahi kuingia ATM. Kwa udogo wangu wa umri na umbo hata sikuhangaika kuwauliza walinzi nilijua tu wanganisumbua na maswali kibao.

Nikazama ndani, ile kufika nikaichomeka kadi (nikafanikiwa bila bugdha) nikafarijika baada ya kuona kumbe kuna instructions kabisa, nikazifata mpaka nikatoa hela.

Kikwazo kikawa bi mkubwa alikua anataka kutoa laki 3, na mimi nikawa nimetoa laki mbili then laki moja.

Nikiwa pale pale akapiga simu kua kwanini natoa hela mala nyinginyingi namna hiyo wakati huo sijui kua kuna option ya kutype na kutoa kiasi unachotaka, nikajitetea ni mtandao na akaelewa.

Ila thanks to her, nilimaster mambo ya kibenki nikiwa mdogo kabisa, nikiwashangaza wenzangu kina
Haha noma!
 
Siku moja nilienda baa fulani kubwa sana ,nikavuta kiti nikaa, ,baada ya muda kidogo,akaja mrembo akachagua meza ya peke yake ,akatoa laptop kwenye mkoba na kuanza kubofyabofya ,kipindi hicho mtu kutembea na PC anaonekana maisha fulani ya kishua.

Mimi nikajiongeza nikamuita muhudumu ,nikamwambia qkamwabie Yule dada akimaliza shughuli be zake Kwa PC naomba nimjoin. Dada wa watu hakuwa na shida akaenda Kwa Yule demu akamwambia kisha akarudisha jibu kuwa dada kasema hayupo bize ,ukitaka mjoin ti,ila wewe ndiyo ukakae pale.

Nilifurahi kinoma nikajikuta mwanaume ni Mimi tu mle ndani, nikamsalimia ,demu akajibu Kwa sauti ya chini huku macho yakiwa kwenye PC.

Wakati huo Yule demu kaagiza maji madogo,nikamwambia unakunywa kinywaji gani (pombe) akadai alcohol hatumii alishaachaga kitambo,na akasema hatumii chochote. Nikatoa burungutu la pesa tena za watu nilitumwa na mwarabu fulani nikamnunulie vifaa vya ujenzi nikiwa kama mtoto wake maana zamani nilikuwa dereva wake hivyo akaendelea kuniamini

Demu hanywi pombe,hatumii hata soda
Nikaona sasa demu si huyu kuliko Yale mapaka yanayotumalizia pesa,Bora huyu hataki chochote,nikamshawishi basi ale chakula akadai hajisikii njaa kwani ana Mawazo Sana hapo ndipo nilipojikanyaga.lakini Ile pesa ilimtamanisha akanifanyia mchezo.

Wakati natoka nje nikaangalie nilipopaki butterfly yangu,ili nijilidhishe na usalama kuna mshikaji alinifuata akionekana ni mtu wa jikoni ,mazungumzo yakawa hivi,

Vipi kiongozi" alisalimia Jamaa.

Kwema niambie Kaka" nilimjibu

Yule uliyekaa naye ,mnafahamiana naye?
aliuliza.

Hapana ,sifahamiani naye,nimemuona hapa hapa,si unajua tena mambo ya kampani (huku nikijichekesha)

Yule demu jau,ni tapeli ,ni mlevi halafu anawaibia sana wanaume.aliongeza

(Huku nikichukia)
Weee dili na jiko bro,habari zingine achana nazo.kama hunitaki nihame baa,nilitishia

Samahani bro ,nisamehe sitarudia tena .alijibu Yule jamaa huku akiondoka .

Nilirudi nikakuta dada yupo kashika Tama huku akionekana mwenye Mawazo.

Pisi Kali ,pua ya kisomali ,nywele zimchanwa saaaafi kabisa nikaona huyu mbona mzuri, halafu hanywi pombe halafu boya mmoja analeta wivu na kudai pisi hii ni tapeli.

Vipi mbona ni mwenye Mawazo shida ni mrembo,niliuliza Kwa sauti ya kiume yenye mahaba.

Weee Acha tu nawaza hivi ni lini nitapata mpenzi wa kweli ,na nipendwe kama wengine.alijibu.

Wee usinitanie binti mrembo hivi huna mpenzi,sema unachagua Sana Sisi masikini mnaona tutawapa nini ,.niliongeza

Weee Bora mwanaume masikini lakini mwenye mapenzi ya dhati. alijibu.

Naitwa Daniel ,nimependa kampani yako sana,naenjoy naomba tafadhali niagize chochote,ule walau nafsi yangu itatulia.
Niliongea Kwa hisia.

Sasa Daniiiiiii(akiongea Kwa kudeka kama vile ananijua siku nyingi )

Hapa kuna makelele sana kwanini tusitafute sehemu nzuri,tutakapokuwa comfortable na mazungumzo yetu.demu alishauri.

Sikupinga nilitafuta nilikabidhi pikipiki yangu Kwa mlinzi nikimwambia nitairudia.(unapakiaje mtoto mzuri kwenye pikipiki?)

Nikaita taxi hao tunaenda location nyingine demu akawa anaonekana mwenye Mawazo kiasi cha kudondosha machozi .nikawa na kazi ya kumbembeleza.

Hatimaye tukafika sehemu husika Ile nashuka na watu wengine wanashuka kwenye taxi nyingine huku jamaa mmoja akiwaambia wenzie aliokuwa nao kuwa Yule demu ni mke wake na sikuzote wanagombana kisa Mimi ,nikaanza shushiwa kichapo .huku wakidai nipelekwe polisi ,nikaona polisi itakuwa soo Bora tulimalize tu tunamalizaje nikatoa kiasi cha laki sita na thelathini,hii thelathini elfu nilimpa Mzee mmoja aliyenishauri ni Bora nikubali kumalizana nao kuliko mambo Yale kufika mbali. Nilijiona mshamba Sana yaani baada ya kujua Yule demu alinichoresha
 
Me ilikuwa ni kitambo nilikuwa bado sijui nafasi za kwenye mpira najua tu kipa ni namba moja ila wengine najua ni mabeki, viungo na washambuliaji ila sijui namba zao
Hivyo nikaitwa kucheza nikauliza we unacheza namba ngapi nikasema winga namba nane, jamaa akauliza nini ! nikarudia tena bila wasi wasi basi hapo ilikuwa ni kicheko dakika kama tano nachekwa tu
hahahaha umenikumbusha movie ya BANA CONGO, Mboto anajifanya Mkongoman kasajiliwa na timu gani sijui waandishi wanamuuliza unacheza namba ngapi? Anajibu nmba yoyote nacheza hata mkiniweka benchi mi nacheza.
 
Nilikuwa natoa presentation bana, hall imetulia ile nasikika mimi tu dadeki, sasa bwana ulimi ulinitenda badala ya kusema "to avoid poor performance" si nikasema "to avoid poor farfomance" kuna bidada mbele kabisa alikuwa natabasamu....jamaa yangu si fala kajifanya kakohoa bana, nje kamalizia kicheko chake 😅
 
Nilikuwa natoa presentation bana, hall imetulia ile nasikika mimi tu dadeki, sasa bwana ulimi ulinitenda badala ya kusema "to avoid poor performance" si nikasema "to avoid poor farfomance" kuna bidada mbele kabisa alikuwa natabasamu....jamaa yangu si fala kajifanya kakohoa bana, nje kamalizia kicheko chake
mfupa hauna ulimi [emoji1787]
 
Back
Top Bottom