Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Msela wangu alikuwa na manzi yake mmoja mkali sana. Yule manzi alikuwa kanizoea kinoma maana niliwahi soma nae shule moja. Sasa kuna siku akanialika kwenye graduation yake mkoa mwingine. Nikafurahi kinoma alafu ujinga ni kwamba nikamtumia message msela wetu mwingine ikisema kitu kama "Demu wa bro kanialika kwenye sherehe na ananilipia nauli kwenda". Kumbe message ikaenda kwa yule manzi aisee. Toka kipindi hicho akanionaga snitch, akanikaushia mpaka leo
 
Msela wangu alikuwa na manzi yake mmoja mkali sana. Yule manzi alikuwa kanizoea kinoma maana niliwahi soma nae shule moja. Sasa kuna siku akanialika kwenye graduation yake mkoa mwingine. Nikafurahi kinoma alafu ujinga ni kwamba nikamtumia message msela wetu mwingine ikisema kitu kama "Demu wa bro kanialika kwenye sherehe na ananilipia nauli kwenda". Kumbe message ikaenda kwa yule manzi aisee. Toka kipindi hicho akanionaga snitch, akanikaushia mpaka leo
huu ulikuwa ushamba mixer na usnitch usnitchimba pro max 😀
 
Nipo Kama darasa la Kwanza Kuna mafuta ya mgando nilikuwa napaka kila nikimaliza kuoga. Sasa Yale mafuta yalikuwa yananukia vizuri mno Hadi nilikuwa natamani kulamba.
Siku moja mama kaenda kwa jirani jioni home Niko peke yangu 😀 nikachukua kijiko nikayachanganya kwenye wali uliokuwa unapikwa yote eti ili wali unukie Kama Yale mafuta 😀😀. Mama akarudi Wala hajastukia Hadi wakati wa kuanza kula. Fikra zangu nikawa nikihisi kila atakaekula atasifia chakula kinanukia. Mmmmh! Wote tulilala njaa siku hiyo😄😄😄😄😄 alafu hawakujua Nani kaweka na Mimi nikajikausha.
 
Habari wakuu
Mara ya kwanza kujiunga na huduma za kibenki nilienda kwenye tawi la benki wakanisajili ikafika mda wa kufanya kadi iwe active.
Nimeenda kwenye ATM na yule mhudumu akaiweka kadi ndani ya ATM ananiambia chagua lugha, me hapo hata sijui wanabonyeza wapi, akanionesha zile button za pembeni nikachagua, akanambia bonyeza hapa nikabonyeza, akasema weka namba ya siri nikaanza kuijaza.

Sasa yeye akatoka nimemaliza akakawia kuja. Namsubiri mara nashangaa kadi inamezwa nikamuita nikamuuliza mbona kadi imedumbukia tena, akasema aisee ungeitoa dah, me nikamwambia sasa hukuniambia, nilikaa pale saa zima nasubiri wailete dah!

Mara ya pili, nimeenda ATM pekeangu kufika kumbe ile ATM ni ya touchscreen haina buttons za pembeni zipo za namba tu maandishi yale ya pembeni kumbe unatouch, duh nikadata nje kuna bonge la foleni wanasubiri nitoke, naweka kadi naweka PIN nasubiri hola! duh nikaona nitoke hapa nishatolewa ushamba, hata nikaona kuuliza watanicheka nikaenda kutoa kwa wakala, haha dah!
ushamba mzigo
Bora wewe ushamba wako upo kwenye michakato ya pesa tu..
 
Nikiandika hapa mtacheka sana hasa ukizingatia kwamba mimi ni ngosha 😂

Screenshot_20230602_173056_Chrome.jpg
 
Kutokana na kuwa mshabiki wa soka na mpondaji wa marefa wa ligi kuu Tanzania bara niliteuliwa kuwa refa katika mashindano ya Mpira wa miguu yaliyoandaliwa na mbunge wetu.
Siku ya Kwanza nikapangiwa kuwa referee wa pembeni yani linesman shida ilikuja pale nilipokuwa nakimbia kuanzia kona hadi kona yaani kutoka kwenye kibendera hadi kibendera na nilikuwa namshangaa mwenzangu wa upande wa pili anaishia katikati ya uwanja nakumwona mvivu wa kukimbia.
Nilipogundua kuwa nilikuwa nimefanya makosa nilijifanya mnyonge na nilihama mkoa.

Nilitamani ningejuana na realMamy na Nifah wangenipa ABC zihusuzo maswala uamuzi.
Narudia tena, hii siku sitaisahau kamwe, niliona soni!!
 
Kwa sababu mtaani Kila mtu aliyeniona alinicheka kwa sababu waliamink kuwa kwenye football Niko vema kumbe ni holla.
Hahahah! Mwenyewe niliwahi kimbia mkoa lkn sababu kubwa kadem ambako wote walijua wangu na walijua nitakatoa usichana lkn kakifika kananifanyia ubabe nashindwa Hadi pale rafiki yangu mmoja alipokakamata kwa nguvu akakachapa vibao kakaachia akakatatua, alafu nakuja pata stori sikuamini macho yangu. Ilibidi jioni Nimwite msichana kumuuliza akagoma lkn kumvua nguo kilaini naingia hivi duh! Tayari kweli, ndipo nilipohama mkoa kwa aibu hahahah!
 
Back
Top Bottom