Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Haijakamilika bwashee ongeza hivi
IMG-20240724-WA0018.jpg
 
Me mara ya kwanza kupanda ndege kwenda nje ya nchi(nilikuwa ndo nimemaliza advance)
Jamaa mmoja kati ya waliokuwa wananisindikiza akanambia kama nina maker pen, basi niandike majina kwenye mizigo yangu ili isipotee.

😂Baade ndio nilikuja kugundua kuwa ule ulikuwa ushamba, lakini sikuelewa yule jamaa, alinifanya mimi mshamba au na yeye alikuwa mshamba pia😂, maana sina hakika kama aliwahi kupanda ndege
 
Me mara ya kwanza kupanda ndege kwenda nje ya nchi(nilikuwa ndo nimemaliza advance)
Jamaa mmoja kati ya waliokuwa wananisindikiza akanambia kama nina maker pen, basi niandike majina kwenye mizigo yangu ili isipotee.

Baade ndio nilikuja kugundua kuwa ule ulikuwa ushamba, lakini sikuelewa yule jamaa, alinifanya mimi mshamba au na yeye alikuwa mshamba pia, maana sina hakika kama aliwahi kupanda ndege
[emoji1787] 😀 😀 😀 ushamba ni noma!
 
ahahahaha me perfume nilikua hata sijui majina yake nilivoanza kupuliza napuliza mpaka kwenye viatu mpaka mdomoni alooh [emoji1787]
MIaka hiyo kulikuwa na sista mpangaji wetu alikuwa mfamasia akapata kazi JD Pharmacy.
Sasa kule JD pharmacy walikuwa wanauza na unyunyu wakishua. Ila hua wakileta mzigo mpya kuna perfume za sample kwa ajili ya kutest watu wamezipokeaje?
Nilivyomaliza chuo siku ya graduu, akamwomba dogo kuwa anitafutie nguo chakavu zangu kama mbili amabzo sizivai,
Akapewa akachukua box zuri sana.kafunga zile nguo pamoja na ile perfume za sample wanazopewaga JD PHARMACY.
Mwamba wakati wa kufungua zawadi nafungua nylons nakuta nguo zangu nkaona maajabu kwenda kucheki room hazipo kuangaliaa vizuri nkakuta unyunyu na msg yake ya pongezi,
sasa mtoto wa mbwa na unyunyu wapi na wapi?
Basi ule unyunyu nkawa napulizia hovyo hocyo, ila ukipuliza aisee ulikuwa ni balaa. Sasa demu wangu kaja geto kasema unyunyu wako mzuri nkampa.
Yeye akaanza kuutumia, kistarabu sasa siku moja kaenda kwenye sherehe, nduguze wacha wamsifie wacha wampe compliment unanukia balaa umenunua wapi? Jibu ni moja tu kanipa mpenzi wangu.. mwambie atuelekeze,
Sasa siku kaja kunipa zile habari na kuulizia nimenunua wapi, nkasema nilipewa zawadi na mpangaji wetu,. Akaomba nikaulizie bei maana mama yake mkubwa ameupenda,
Mimi nkanyoosha komwe kama nyundo inaenda kugonga msumari kwa mpangaji, kuwa ule unyunyu nimeupenda umenunua wapi? JIBU LAKE ALIKAA KIMYA AKASEMA MIMI NINAO KAMA WAKO SIJAFIKISHA HATA ROBO TATU, NI GHARAMA SANA ULE SIDHANI KAMA UTAWEZA BEI, UPO OFISINI PALE ZIPO PC 3 TU ZILKKUJA 5. Nkamjibu kesho naenda kuchukua niwahi kabla haujaisha. Akasema sawa..

Huyoo kesho yake na komwe kama masai na fimbo yake, nkaenda JD YA MLIMANI PALE, NIMEBEBA SAMPLE YA KOPO,.
weka sample mezani, ni habari yako boss naomba hii pc 1,
Nakumbuka muhindi alinyanyuka akasema karibu ipo na zimekuja brand nzuri zaidi. Hii umeipata wapi? Nkakaa kimya, kwa lugha ya kuogofya nikikjmbuka maneno ya sijui kama utaiwsza bei..
Nkauuliza bei ngapi?
Akanijbu lak 6 ila naweza nkakupunguzia ukichukua mbili... moyo ukalia paaa! Ukamalizia ondoka hapa chap kabla cjaamua kusimama mazima,... jasho jembamba linatoka nkasema kwa sauti ya upole.
Naenda kwenye atm ya crdb nakuja,

Nilichukua sample yangu nkampigia demu wangu nkamwambia kila nilipokuwa najipulizia nilikuwa nachez3a hela bwana hii ngoma 600k...

UShamba huu. Sikujua nimepewa vitu hadimu
 
MIaka hiyo kulikuwa na sista mpangaji wetu alikuwa mfamasia akapata kazi JD Pharmacy.
Sasa kule JD pharmacy walikuwa wanauza na unyunyu wakishua. Ila hua wakileta mzigo mpya kuna perfume za sample kwa ajili ya kutest watu wamezipokeaje?
Nilivyomaliza chuo siku ya graduu, akamwomba dogo kuwa anitafutie nguo chakavu zangu kama mbili amabzo sizivai,
Akapewa akachukua box zuri sana.kafunga zile nguo pamoja na ile perfume za sample wanazopewaga
Kwenye historia niliskia kuna watu walikuwa wanatumia tanzanite kucheza bao, wasijue wanacheza na utajiri, haha dah hii yako kali hapo hio laki6 ni kwa thamani ya hela ya kitambo saivi si inafika hata 1M 😀 hatare
 
Daahhh me nakumbuka siku moja nilikuwaga darasa la saba tena mwalimu alikuwa darasani anafundisha sasa bwana pembeni yangu kukawa kuna wanafunzi wawili wanatukanana mwishowe wakagombana mimi huyu na kihelehele nikanyanyuka kuwashitaki nikasema mwalimu aroni na aziziz wanagombana akaniuliza Chanzo nini me nikasema walikuwa WANATUKAMANA BADALA ya wanatukanana daaahhh aki hiyo siku siwezi kuisahau nilichekwa kila siku na darasa Zima daahhh
 
daah 😀 😀 😀 mambo ya michapio
 
Mara ya kwanza kujifunza kupika ugari nilikua sijui ni muda gani Natakiwa kuweka unga na muda gani Natakiwa kusonga daaaa niliumia sana ilikuwa mwaka 1999nikiwa na miaka 8
 
Mara ya kwanza kujifunza kupika ugari nilikua sijui ni muda gani Natakiwa kuweka unga na muda gani Natakiwa kusonga daaaa niliumia sana ilikuwa mwaka 1999nikiwa na miaka 8
😀 😳 noma sana hata me nilikuwa nasweat sana namwaga maunga mara niungushe 😀
 
Boss wangu enzi za 2009 akaniambia kijana twenzetu waache hao wengine, nakumbuka siku nzima sikula sababu wateja wengi weekend.

Huku na huku gari prrrrr mpaka bar, imeletwa nyama choma plus njaa tena nikajifanya nna haraka, kumeza kipande cha nyama hakipandi wala hakishuki jicho limenitoka balaa na chozi limeanza ile mbaali, ilibidi niact kama natafakari kwa kuweka 'ngumi ya kutafakari' mdomoni kumbe nabembeleza finyango ishuke [emoji23][emoji23][emoji23].

Funny enough nilienda kwa Dr nikamweleza since ilinitokea twice, nikajua Dada Dr though tunajuana atanibembeleza kwa majibu soft, alinipa jibu moja tu nilijiona mbugila "R ukiwa unakula hizo nyama choma zako uwe unalainisha koo kwanza n nilipata aibu asee, utakuja pigwa ngumi za mgongo sasa hapo kuna dawa ya kukupa kweli" [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom