Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Kutokana na kuwa mshabiki wa soka na mpondaji wa marefa wa ligi kuu Tanzania bara niliteuliwa kuwa refa katika mashindano ya Mpira wa miguu yaliyoandaliwa na mbunge wetu.
Siku ya Kwanza nikapangiwa kuwa referee wa pembeni yani linesman shida ilikuja pale nilipokuwa nakimbia kuanzia kona hadi kona yaani kutoka kwenye kibendera hadi kibendera na nilikuwa namshangaa mwenzangu wa upande wa pili anaishia katikati ya uwanja nakumwona mvivu wa kukimbia.
Nilipogundua kuwa nilikuwa nimefanya makosa nilijifanya mnyonge na nilihama mkoa.

Nilitamani ningejuana na realMamy na Nifah wangenipa ABC zihusuzo maswala uamuzi.
hahaha hii ndo fedheha sasa.
 
Hii yako inafanana na yangu, me hadi leo sina interested na mpira, sio kucheza wala kushabikia.

Nilikuwa shule ya msingi, mtaani kwetu panaanzishwa timu mpira wa gozi, sasa wanacheza kinamba, me nikaulizwa nacheza namba ngapi, wakati natafakari(maana nilikuwa sijui) kuna jamaa akaninong'oneza namba 13, halafu na mimi nikaropoka namba 13 .
Asee nilichekwa mpaka nikapewa jina namba 13
Hahaha wakunong'onezana jau sana.

Kuna mwanetu mmoja alisinzia class, Madam wa Kiswahili akampoint ghafla asimame ataje aina ya kitenzi kilichoandikwa pale ubaoni. Kuna jamaa bila huruma akamnong'oneza "Sema Kitenzi Kinomino.." jamaa akaitaja kama ilivyo ikawa vicheko tu...

Mwingine alikua madam mmoja wa Physics huwa mkifanya test siku inayofata anaingia na ile pepa anawasimamisha wote anauliza maswali anayejibu vizuri anakaa chini. Sasa wale wenzangu na mimi maswali ya True and False yalikua yanatubeba sana maana akikosa mwenzako kasema True we unasema False chapu kwa haraka unakaa chini.

Sasa bwana ndugu yetu mmoja asijue kwamba maswali ya True or False yameisha likaulizwa swali la kudefine asee. Kuna jamaa likamnong'onza "Semaa TRUE". Tukasikia TRUEEEEEE......Ikawa full vicheko na kipindi kikaishia hapo hapo..

Toka kipindi hicho niko makini sana na watu wanaonong'oneza.
 
Siku ya kwanza kwenda kijijini mkoa wa Kagera nilipanga nyumba nzima. Njee ya nyumba kulikuwa kumepandwa migomba na maharage sasa Mimi maharage nilikuwa sijui jinsi yanavyo kuwa shambani nilijua majani tu yamezunguka migomba. Nika mwita mwana kijiji nikampakazi yaku fyeka Yale maharage. Aisee nilionekana mshamba mpaka niliona Aibu
hahaha kwa hiyo alikustua huyo mwanakijiji kwamba unataka kuzingua?
 
Kuna siku nilienda ugenini na rafiki yangu kwa ndugu zake. Hapo tulipokwenda wenyeji wetu ni familia fulani hivi ya kishua. Sasa katika story tulizokuwa tunapiga tukawa tunaongelea ile skendo ya Mengi na Jackline Ntuyabaliwe.

Mzee nikaanza kutoa madesa yangu ya udaku nafunguka najikuta nina za ndani zenyewe konki.

Kuna sista pale alikuwa amekaa kimya alipoanza kuongea ndio nikaja kujua ni family friend wa akina Jackline Ntuyabaliwe kabisa na alisoma na dada yake so anajua story kwa uhakika yaani bila kusikia kwa watu ni kwamba anajua kash kash zote na alitunyooshea habari vizuri kabisa.

Aiseee nilijiona bonge la fala ikabidi kikae kimya na hakuna story nyingine nilichangia. Nikaja kujua kuwa yule dada ana ukaribu na watu mashuhuri wengi sana na anajua habari zao bila kuhadithiwa au kusikia mitandaoni yaani ni anapata zile fresh info.

Akikwambia waziri fulani kimada wake ni fulani basi sio nyepesi nyepesi ni ana ile pure information from primary source na sio cooked data.

Dah nikajifunza kukaa kimya ninapokuwa na company ya watu nisiowajua. Maana unaweza tukana kiongozi kumbe upo na mwanafamilia wake hapo kikaoni.
 
Huo ulikuwa udaku spesheli mkuu😂 afu mwenye udakuzi kumbe yupo
 
Back
Top Bottom