Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Mwenzenu nimewahi kukaa ukweni zaidi ya miezi nane, nikiwa na ujauzito wa miezi mitatu mpaka nikajifungua, nilikuja kuondoka mtoto anamiezi mitatu. Katika muda wote huo niliwahi kufanya tukio ambalo najutia sana ingawa lilitokea kwa bahati mbaya tu.
Mume wangu alinikataza kitu fulani nikakubali tena nikamuahidi hakitajirudia tena. Basi siku hazikupita nyingi likajitokeza wakati nazuia si akanipinga, tena mbele ya wazazi wake! Aisee, nilijisikia vibaya na mbaya zaidi akaniita mbele nieleze.
Sasa wakati namlalamikia akumbuke yeye ndiye kanikataza, na hii sauti yangu mbaya sikujua kumbe nilikuwa namfokea mume wangu mbele ya wazazi na ndugu zake. Baadae nilijisikia aibu sana, niliomba radhi na kusamehewa lakini lilikuwa jambo baya sana kutokea. Nilitamani niondoke bila kuaga!
Umewahi kukaa muda mrefu kiasi gani ukweni, na tukio gani siyo rahisi kulisahau?