Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenzenu nimewahi kukaa ukweni zaidi ya miezi nane, nikiwa na ujauzito wa miezi mitatu mpaka nikajifungua, nilikuja kuondoka mtoto anamiezi mitatu. Katika muda wote huo niliwahi kufanya tukio ambalo najutia sana ingawa lilitokea kwa bahati mbaya tu.
Mume wangu alinikataza kitu fulani nikakubali tena nikamuahidi hakitajirudia tena. Basi siku hazikupita nyingi likajitokeza wakati nazuia si akanipinga, tena mbele ya wazazi wake! Aisee, nilijisikia vibaya na mbaya zaidi akaniita mbele nieleze.
Sasa wakati namlalamikia akumbuke yeye ndiye kanikataza, na hii sauti yangu mbaya sikujua kumbe nilikuwa namfokea mume wangu mbele ya wazazi na ndugu zake. Baadae nilijisikia aibu sana, niliomba radhi na kusamehewa lakini lilikuwa jambo baya sana kutokea. Nilitamani niondoke bila kuaga!
Umewahi kukaa muda mrefu kiasi gani ukweni, na tukio gani siyo rahisi kulisahau? Itakuwa alikuonya usijambe, Sauti yako ya Zege akajua unamfokea akakupa Tena vitasa.
Apike na dadii .ile nyeupe.Weee [emoji1787][emoji1787]
Ili warombo tukusamehe unatakiwa upike pipa 36 za mbege
Ile Dadii aisee Kuna siku nilienda Olili huko kwenda tu kuona kaburi la Aqwilina aliyepigwa risasi. Nikiwa pale na mshikaji na baba mdogo nikawapiga biere sasa Kuna demu alikuwa anakunguta Dadii akidhania ni maji. Tulikaa mpaka jioni akawa anapiga kwikwi balaa😂 sie poa kabisa IleApike na dadii .ile nyeupe.