Mwanzo nilikua nachukulia masihara na mimi nikajiamini ni 'gangster' siwezi kuumizwa na vitu kidogo kama mapenzi labda msiba na hasara kubwa ya kibiashara hata mali
Hapo tayari nishadate karibia miaka 5+ zile kuacha na kuachwa so nikachukulia kawaida wanaoumia ni wajinga tu
Kumbe sikuwa nimependa bhana, nilikuwa najidanganya
Si huyo manzi akanipa nachostahili, maana bora hata angeniacha ningejua moja ila baada ya kuchoshwa na vituko vyangu pamoja na kumvimbia mixer kiburi, simjali mpaka niwe na shida tena ya yale masuala ya pale kati, sometimes nasarandia videmu vingine
Alichofanya akahamishia majeshi kwa mwamba mmoja hivi mtaa wa pili tu halafu akanizimia data[emoji23]
baada ya kunipotezea kwa muda nikawa namsaka sana lakini wapi, wana wakaniambia meza ishapinduliwa huna chako we si ulimvimbia? kampata wanaependana
Ndio nikajua kweli nilitoa boko, ngoja nimbembeleze arudishe majeshi nitajirekebisha, kumbe bhana tayari ana mambo matano kama Jide na harudishi mateka asilani
Kilichoniuma siku hiyo nakatisha mitaa nikakutana nao ana kwa ana wameongozana, manzi ananicheki na mchizi ananichora, dah roho iliniuma sana
Aisee mapenzi yasikie tu, sikulala ilikuwa ikifika night nakosa Usingizi kabisa yaani ile usiku silali niliyokuwa naisikia kwenye nyimbo nilikutana nayo kabisa. . .
Yale mateso yalizidi mwamba alipompa kibendi yule binti, nilitaka kupasuka maana ndio basi tena nikajiona kama sio kidume iweje nikae nae muda mrefu, kila siku ligi kuu napekua tukicheza boli ila no kibendi afu mwamba miezi kadhaa tu tayari kashamjaza bila pampu bali pipe
Dah yale maumivu naweza kuandika gazeti, nyie acheni mapenzi yasikie tu, ila nashukuru yale maumivu yalinipa roho ya chuma, japo ilinichukua miezi mingi kupona.
sasa hivi yakinitokea tayari yalishanikomaza, hivyo hata kama nitateseka ila sio kama kipindi kile.[emoji123]
NOTE: MAUMIVU YA MAPENZI YASIKIE TU, ILA USIOMBE YAKUKUTE