Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Kila kunapokuwa na jambo ka moto mara zote CCM huja na vijambo Ili kuwatoa wananchi kwenye umakini. Wote tunajua kuwa moja, kuna mgao mkali sana wa umeme ambao hata haueleweki, kuna mgao wa maji huku bili za maji zikiwa ni zile zile na kuna ucheleweshaji wa mishahara pamoja na ugawaji wa kihuni wa mbolea.
Ili kupunguza na kuwasahaulisha watu mambo ya msingi kuna matukio yamepangwa ili tuhamishie akili zetu finyu huko. Mfano, jambo la Bashiru Ally, imekuzwa bila sababu za msingi! Pili, jambo la waziri kuitisha mkutano na waandishi wa habari nje ya muda wa kawaida kutoa repoti ya uchunguzi wa ajali ya ndege, ambayo kimsingi ilishasambaa kwenye mitandao, kesho usishangae kukaja tukio la kufumaniwa au la mtu kuhamia chama cha Majizi. Yote haya ni kufanya watu wahamishie akili zao huko huku tukiyaacha mambo ya msingi yanapita.
Wito: Ewe Mtanzania usikubali kupotezewa muda, dai haki yako, umeme, maji na mbolea siyo hisani ya chama wala ya mtu.