SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Ndugu zangu, matukio ya siku chache zilizopita mnaweza kuyachukulia kwa utani ila ni matukio serious sana ambayo yangeweza kuleta maafa makubwa.
Sitaongelea tukio la Simba kushindwa kufanya mazoezi wala Yanga kupeleka timu uwanjani maana kuna nyuzi nyingi zinazozungumzia hayo.
Mimi nitaongelea tukio ambalo najua nalo limejadiliwa ila nahisi halijapewa uzito unaostahili. Hili ni tukio la Klabu ya Yanga kupeleka basi lao Mo Simba Arena kule Bunju siku ya Jumapili 09/03/2025.
Ndugu zangu, baada ya matukio ya weekend, nchi ilikuwa kwenye tension kubwa sana. Ilihitaji katukio kamoja tu ka kuwasha moto, aisee ungeshangaa hali inalipuka ghafla na ingechukua muda mpaka kutulizwa.
Wahenga wa kizungu wana msemo "the straw that broke the camel's back". Maana ya msemo huu ni kwamba katukio kadogo kanaweza kusababisha athari isiyotegemewa kutokana na kwamba kulikuwa na mfululizo wa matukio mengine madogo madogo hapo kabla ambayo yalileta uzito ambao labda haukutiliwa maanani. Matokeo yake katukio kadogo sana kanakuja kuleta maafa makubwa.
Mimi nilifanya kautafiti kangu siku ya Jumamosi na Jumapili maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, nikagundua tension ilikuwa juu sana. Nina njia zangu za kusoma watu au hali inayozunguka maisha yanayonizunguka hasa kipindi ambacho joto linapanda kutokana na sababu fulani.
Katikati ya tension tuliyokuwa nayo, inakuwaje mtu anachochea zaidi uhasama kwa kufanya kitendo kama kile kwa kisingizio cha "utani wa jadi"? Kama sisi ni watani wa jadi, inakuwaje usiku wa jana yake tu ulinifanyia vitimbwi, fujo na kunidhalilisha huku ukinizuia kufanya mazoezi ambayo ni haki yangu? Huu ni utani au unafki tu?
Nashauri vyombo vya ulinzi na usalama wafanye uchunguzi wa tukio la basi la Yanga kupelekwa Bunju karibu na Mo Simba Arena na ikionekana lilifanyika maksudi, hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
Tukio la basi la Yanga kupelekwa Bunju halihusiani na mpira kwa hiyo vyombo hivyo visisite wala kujificha kwenye kisingizio cha kutoingilia mambo ya mpira.