Tetesi: Tukio la kijiografia la mwezi mpevu sana (Supermoon) litatikea Nchini Tanzania siku ya Alhamisi tarehe 7/5/2020 saa 13:45

Kweny ungezeko la watot hapo nakuelewa maan tanzania tu watot wa shule wanapat mimba kwa kasi sas huko kweny lockdown ya coron itakuwaje
Hapana jaribu kupitia maandiko yanayoelezea mwezi, mzunguko wake na uzazi hasa hasa pitia astronomy utaelewa
 
Hizo athari ni kwa majibu wa Nolle mwaka 1979 na zinaonekana kutokana na mambo makubwa mawili
1.graviti ya mwezi.
2.Mvutano kati ya ganda la Dunia na mwezi.
Lakini athari hizo Nolle hakuzitolea majibu ya kisayansi.
Kama Magufuli 😀😀😀
 
Kweny ungezeko la watot hapo nakuelewa maan tanzania tu watot wa shule wanapat mimba kwa kasi sas huko kweny lockdown ya coron itakuwaje
Hadi shule zifunguliwe idadi ya wajawazito itaongezeka. Kuna kadenti yuko kidato cha 4 juzi kati kapimwa ana mimba ya wiki 4.
 
13:45 iko moja tu kwa siku yaani ndani ya saa 24.
Kachanganya kingereza na kiswahili.Saa zetu za kiswahili masaa yanaanza saa moja asubuhi kwa saa za Afrika mashariki ina maana akisema saa 13.45 kwa saa za Afrika mashariki kwa masaa 24 in maana saa 13.45 itakuwa saa 1:45 usiku lakini Kama Ni kwa saa 24 za masaa ya uingeteza Hilo tukio la saa 13:45 litakuwa saa 7:45 mchana ndio maana nikauliza hiyo daa 13:45 Ni saa ngapi anaongelea? Kwa saa za Afrika mashariki au kwa masaa ya uingereza.Tusaidie wewe Sasa Hilo tukio litakuwa saa ngapi kwa saa zetu za Afrika mashariki
 
Inatokea sasa hivi.
 
Mbona sioni hayo makitu hapa nje. Naona mawingu tu yametanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…