Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Eti ni kweli hii kazi bila ushirikina hautoboi?
Naomba uwe mkweli...
 
Struggle za mwanaume ni hatari,,, machimbo, kufanya mapenzi mara kwa mara,,kazi za ufundi ambazo ni hatari'umeme'kujenga'kuchomelea'uzinzi,, bodaboda,, uvuvi,, mabaharia
 
Sana
 
Yani unavokaongea ni chinga ntupu!
 
Yaani yule jamaa alinidissapoint sana
Nilitegemea kujua mengi nikaishia kusoma malumbano ya mabaharia
Wajua ye aliweka heading ambayo iko nje ya uwezo wake[emoji28][emoji28][emoji28]

Na kama unavyojua JF wajuaji ni wengi, ndio pale mtifuano ukaanza wa kutunishiana misuli[emoji28][emoji28]

Hata hivyo yale maswali mliyokuwa mnamuuliza yalikuwa magumu, nimesoma nikacheka sanaa

Nilichompendea mhusika ni kuwa hakuwa anachukia wala kukata tamaa, ye aliendelea tu na yale aliyoweza mengine anayakaushia kama hayaoni na kudai amejibu maswali yote na simu yake mbovu haiwezi kuandika ujumbe mrefu
Ule ni moja kati ya uzi ambao ukiwa down na ukaupitia basi lazima mood itabadilika na furaha itarejea

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Umeanza vizuriii umemaliza vibaya!kutunga tena
 
Mkuu umemsahau chongoe all the way from Mafia na mambo yake ya baharini



Cc travis 1 na fyddell

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Baharini jinai nyingi ndio maana mengine kuyajibu nafiliria
 
Mkuu mbona hueleweki, Post za zamani ulisema mwenzio huyo ni mmalawi saizi tena mrundi
 
Nilichomoka camp kwa tahadhari, sikutaka mtu ajue tena zaidi yule mmalawi (huyu ni mmalawi sio mrundi )

Mdogo mdogo huku mvua ikinichapa, nilipo hakikisha nime ziacha hatua kadhaa zile camp nikawasha tochi yangu ya kichwani moko yangu begani taratibu nasonga na njia.

Nilitembea mwendo wa masaa kama mawili hivi, mvua ikinyesha, uoga ukaanza kuniingia, japo tuchi yangu ilikua ikiwaka vizuri tu, lakini nilipata tabu kuona mbele.

Kuna muda nilikua natoka nje ya barabara, yani napotea njia, mara nimeingia kwenye mashimo, uoga ukanizidi.

Nimelowa mpaka boxa ya ndani, meno yana tetema mpaka yanauma, hapo natamani atokee mtu na bange lake anitembezee.

Nilizidi kutembea huku nikitetema, mkono nilio shika moko vidole vyote vimekufa ganzi, Kiufupi nilijiihisi naota.

Mbele kidogo kuna korongo limezunguka, kikawaida makorongo haya hupitishaga maji, natangu naiwaza hii safar akili yangu ilikua hapa kwenye korongo, sababu kwa mvua ile ni lazima ningeyakuta maji yame jaa, na hakuna njia nyingine.

Chaajabu nililikaribia korongo nakulikuta korongo kavu, yani kuna vimaji tu vya ugoko, yani hata suruali hukunji.

Hapa nili shangaa sana, maana si rahisi kwa mvua ile, sehem ile isijae maji.

Nilitambuka mpaka ng'ambo ya korongo, hapo nikaendelea na safari.

Kadri nilivyo kua natembea ndivyo sasa mvu ikawa inapungua na hata ka mwanga nikawa nakaona kwa mbaali.

Hapa nikaona ngoja sasa nitwete niwasubiri wale jamaa waolikusudia kurudi kijijini.

Nilipo kaa pale, usingizi ukanipitia (kati ya vitu ambavyo hatuwezi kuviamrisha sisi wenyewe ni usingizi na haja kubwa, binaadam anaweza kulala hata kwenye dimbwi la maji ) nililalaaaaaaaaaaaa

Nitarudi muda si mrefu
Ndugu zangu sifanyi kusudi sema ndio vivyo tusamehane.
 
Aisee mwamba umenikumbusha chimbo moja huko Katoro.

Kuna mzee alikua na eneo lake afu lina mali (dhahabu). Tumeenda kwa mtaalamu (mganga), akatupa masharti tusivute sigara, bange, kulala na mwanamke na mzee mwenye eneo alikatazwa asiguse chochote kitokacho ndani ya duara (shimo) .

Lile duara lilikua na miujiza sana ukizingatia haya mambo ya madini yanaendana sana na mambo ya kishirikina,,kuna watangulizi wetu waliwahi kuchimba hapo wakakosea masharti duara likaanza kutetemeka kila mtu akakimbia hakuna aliyerudi.

Tulipiga piga pale, aliyekuja kuharibu ni yule mzee mwenye eneo yaani....

Huu uchimbaji hasa wa dhahabu unamambo sana.

*Hapo kwenye masharti waliyokua wamepewa huko kwenu wasivute sigara, bange na wanawake ndo yamefanya nikumbuke hili jambo.
 
Yaaani...Pesa bhana...watu wanakufa Kama kuku wa mdondo...alafu mnawapekua wakati hamkutakiwa kuwashika Kwasababu ya Ugonjwa.

Duuuuh

Mimi namikasa Yangu yamaisha Yangu natamani kuhadithia....siku ntakuja na ID Feki
Tunasubir
 
Hivyo vitu vitatu hata ktk Maisha ya kawaida ukiachilia Mbali Machimboni.. havifai kbs.. hasahasa Pombe na wanawake.. Laana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…