Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Mkuu hapo mulimpa ulaji huyo muhindi.
Hapo mulikua munauza Pete kama yenyewe, na kidani munge kiuza chenyewe.

Tena hapo, kati ya Pete (dhahabu) na kidani chekundu (Ruby) hicho kidani ndio chenye thamani.

Hicho kidani kikifika points 4 tu ni zaidi ya Milioni moja.
 
Kwahiyo inamaana Muhindi alichukua kidani /Rubby halisi na kuwaachia jamaa jini lao?!
 
Daaah, wana ndugu tusamehane, siunajua mishe za kazi!?
Jana mchana kutwa nilikua kazini kumtumia Shetani ili chati yangu ipande.

Kama unavyo jua kazi zetu, ukiingia shimoni asubuhi, ni kazi tu mpaka shift yako imalize.
Hakuna atakae kusaidia kazi zako eti kisa ulikua JF una piga story.

Ila leo nina shift ya usiku, kwahiyo mchana kutwa nitakuwepo hapa.

Ahsanteni, na Asubuhi njema.
 
Habari za asubuhi wakuu.. Naimani kila mtu yuko powa na familia yake siku ya leo na kwa mabachelor mmeamka salama. Kwa washabiki wa mpira tupeane pole maana Tunisia si level yetu, hakika walistahili kutufunga. Naendelea na stori Kama nilivyowaahidi.....
Tuliambiwa ile dawa tuoge asubuhi na usiku kabla ya kulala na kunuia maneno flani ya kumfukuzia yule kiumbe. Ile laki mbili alivyokuwa nayo dogo baba aliamua kumpa yule shekhe (sijui aliitumia au aliichoma moto kama alivyodai?🤷 Vile vitu vingine shekhe alivifuata nyumbani ili akavichome Moto pia). Sasa ilipofika usiku wa ile siku mimi na mdogo wangu wote tunaogopa kwenda kulala chumbani. Hiyo ni j'tatu na chuo sikwenda kwa hofu ya lile dude kunitokea chuoni nikiwa peke yangu, pamoja na kupewa Ile dawa na kile kisomo bado nilikuwa nimejawa na hofu so nilitaka kuwa karibu na baba maana yeye ndio alikuwa anaonekana jasiri kuliko wote. Mama yeye baada ya kusimuliwa na mzee aliyosema yule shekhe alibaki kulia na kuomba tu huku akimwomba (kumlazimisha mzee atupeleke kwa Kakobe). Usiku ilipofika baba akaamua kulala na sisi chumbani, kwakweli usingizi haukuja, mapigo ya moyo yapo juu, nikimwangalia dogo nae dogo ananikodolea macho tukiwa kitandani mzee kalala chini, pembeni ya kitanda. Mida ya Kama saa saba sijui saa sita (sikumbuki muda sahihi) usingizi ukatupitia, nakuja kushtuka.....
 
Kutoelewa hizo issue kulichangia mkuu. Mi laki tano niliona hela nyingi hata sikuuliza mara mbili
 
Yaani ninavyosimulia hapa, picha kamili inanijia kichwani kwasababu nakumbuka Kila kitu mpaka sura yake ingawa ilikuwa usiku. Mkuu acha kabisa kuonana na viumbe hivi
hao jamaa ni dhaifu mkuu kuliko unavyoweza kudhani....na wana limitations nyingi kuweza kumdhuru mtu ila wakikukuta mwili uko free uko biased na maovu na takataka nyingine hakuna rangi wataacha kukuonesha..
 
Pale nilipo kaa (kuwangoja washkaji) usingizi ulinipitia nililalaa mpaka nilipo amshwa na makelele ya washkaji.

Sijui nilitumia muda gani kwenye usingizi ule ila nilipo angalia saa ilikua ni saa 6 mchana.

Nilipo amka nilikutana na kijua kikali utadhani niko Sudan, yani mpaka nguo nilizo vaa zilishaanza kunyauka.

Chakwanza niliwauliza kuhusu yule mmalawi, nikaambiwa bado wako camp wanaendelea kungoja mvua iishe waanze kazi.

Nilipo wauliza vipi kama mvua imeisha huko walikotoka, wakaniambia mvua imenyamaza sasa hivi baada ya kuvuka lile korongo.

Yani kumbe mvua inaanzia kwenye korongo kwenda matandani, ila kulimaliza korongo mvua hakuna.

Tulitembea mpaka kijijini, hakuna alie jua kua mimi nina dhahabu mbeleni.

Tuliingia kijijini saa 2 usiku, hapo tukalala.
Ila kwakua tulisha fika kijijini, kila mtu aliendelea kimpango wake.

Pale kijijini kila mtu anaham ya kujua kulikoni huko porini.
Nakumbuka nilitulia kwenye kiosk cha jamaa flani hivi, kila mtu alikua ananiuliza kuhusiana na porini.

Usiku kucha nilikesha kwenye kile kiosk cha jamaa nikila Royal gin (hii ni pombe kali sana) mpaka kuna kucha.

Kwakua nilikua na pesa ya kutosha niliyo chukua kwenye lile duka la marehem, hivyo ilikua mwendo wa kujimiminia pombe.

Kuna dem alinitamani nika lale kwake, lakini nilikataa kwa kuhofea asiniibie dhahabu yangu.

Migodini wanawake ndio wanaongoza kutuibia wachimbaji.

Kilicho fanyika nikumpa pombe mpaka dem akakimbia.

Asubuhi, sikutaka kulemba, na pombe zangu kichwani, nikakamata piki piki mpaka Montepuez.

Montepuez, hapa ndio kuna soko la madini yote.

Nikaingia kwa msirilanka nikapima dhahabu.

Dhahabu ilikua na uzito wa gram 112, kila gram kwa kipindi kile ilikua 2000 miticais sawa na laki moja shilingi kwa wakati huo.

Nikachukua 224,000 miticais, hapo akili yote inamuaza mama Abuu (Shemeji yenu)

Nakumbuka nilinunua piki piki na mazaga mengine kama nguo.

Nikatuma kama 60,000 miticais (sawa na Milioni tatu kipindi hicho) kwa mama yangu Tanzania, maisha yakaendelea.

MWISHO.

Naahidi kuwahabarishine matukio mbali mbali yanayo / yatayo tokea hapa mgodini nilipo.

Kumbuka kwa sasa naishi Tete, Muatiz, ila kwa hizi mvua zilizo anza kunyesha, nategemea kurudi Cabo del Gado wilaya ya Montepuez, nikatafute Ruby.

Hapa nangoja hii kazi iishe, nione kama nitaokoa chochote kinisogeze kwenye Ruby.
Ahsanteni na kwaherini.
 
Banaaaaah mbona hvyio me ngoja me niende choon kwanz nikirud naic itakua tayar.
 
Mkuu, wengine bila kufanya kazi hatuli.
Hivyo ni mjinga tu pekee atakae acha kazi yake, akae akuhadithie wewe story.

Usishangae mwenzangu mwisho wa mwezi unakinga mishahara, alafu kwa ku sign tu.

Me bila kushika sururu na chepe, sijala, wala shemeji yako havai tentemente, wajomba zako watarudishwa home kisa ada.
Kwa hiyo kua mvumilivu.
Wanaoanzisha hizi story venye tunawabembeleza wanaenjoy kinoma ani

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Unaenda Cabo del Gado kwa magaidi?![emoji44][emoji15]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…