dumbi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2018
- 988
- 1,542
Mbona na wewe umekausha malizia basi huku tunagoja mzee wa madiniTamu lakini ina machungu yake ambayo nimeyapitia. Ilikuwa kidogo nidisco 2nd year Ila ni kudra za Mungu tu alinivusha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona na wewe umekausha malizia basi huku tunagoja mzee wa madiniTamu lakini ina machungu yake ambayo nimeyapitia. Ilikuwa kidogo nidisco 2nd year Ila ni kudra za Mungu tu alinivusha.
Nimeweka kambi na mimi kujua kisa kilipoishia.Nipo ofisini mkuu, ni half day so kuanzia saa sita nitakuwa free, utaenjoy
Kwahiyo mkuu ukapiga kama million 11 ... Je vipi mkuu unamawazo ya siku 1 kuja kuachana na kazi ya uchimbaji kufanya biashara zingine au haujafikiria kuhusu hiloPale nilipo kaa (kuwangoja washkaji) usingizi ulinipitia nililalaa mpaka nilipo amshwa na makelele ya washkaji.
Sijui nilitumia muda gani kwenye usingizi ule ila nilipo angalia saa ilikua ni saa 6 mchana.
Nilipo amka nilikutana na kijua kikali utadhani niko Sudan, yani mpaka nguo nilizo vaa zilishaanza kunyauka.
Chakwanza niliwauliza kuhusu yule mmalawi, nikaambiwa bado wako camp wanaendelea kungoja mvua iishe waanze kazi.
Nilipo wauliza vipi kama mvua imeisha huko walikotoka, wakaniambia mvua imenyamaza sasa hivi baada ya kuvuka lile korongo.
Yani kumbe mvua inaanzia kwenye korongo kwenda matandani, ila kulimaliza korongo mvua hakuna.
Tulitembea mpaka kijijini, hakuna alie jua kua mimi nina dhahabu mbeleni.
Tuliingia kijijini saa 2 usiku, hapo tukalala.
Ila kwakua tulisha fika kijijini, kila mtu aliendelea kimpango wake.
Pale kijijini kila mtu anaham ya kujua kulikoni huko porini.
Nakumbuka nilitulia kwenye kiosk cha jamaa flani hivi, kila mtu alikua ananiuliza kuhusiana na porini.
Usiku kucha nilikesha kwenye kile kiosk cha jamaa nikila Royal gin (hii ni pombe kali sana) mpaka kuna kucha.
Kwakua nilikua na pesa ya kutosha niliyo chukua kwenye lile duka la marehem, hivyo ilikua mwendo wa kujimiminia pombe.
Kuna dem alinitamani nika lale kwake, lakini nilikataa kwa kuhofea asiniibie dhahabu yangu.
Migodini wanawake ndio wanaongoza kutuibia wachimbaji.
Kilicho fanyika nikumpa pombe mpaka dem akakimbia.
Asubuhi, sikutaka kulemba, na pombe zangu kichwani, nikakamata piki piki mpaka Montepuez.
Montepuez, hapa ndio kuna soko la madini yote.
Nikaingia kwa msirilanka nikapima dhahabu.
Dhahabu ilikua na uzito wa gram 112, kila gram kwa kipindi kile ilikua 2000 miticais sawa na laki moja shilingi kwa wakati huo.
Nikachukua 224,000 miticais, hapo akili yote inamuaza mama Abuu (Shemeji yenu)
Nakumbuka nilinunua piki piki na mazaga mengine kama nguo.
Nikatuma kama 60,000 miticais (sawa na Milioni tatu kipindi hicho) kwa mama yangu Tanzania, maisha yakaendelea.
MWISHO.
Naahidi kuwahabarishine matukio mbali mbali yanayo / yatayo tokea hapa mgodini nilipo.
Kumbuka kwa sasa naishi Tete, Muatiz, ila kwa hizi mvua zilizo anza kunyesha, nategemea kurudi Cabo del Gado wilaya ya Montepuez, nikatafute Ruby.
Hapa nangoja hii kazi iishe, nione kama nitaokoa chochote kinisogeze kwenye Ruby.
Ahsanteni na kwaherini.
mkuu kila la kheri angalia duara likijikopa lisilale na wewe mbele.....mambo yakiwa mabaya jifiche kwenye fonka....huko mkiwa mnashuka chini mnavaa koboko?!....na ukitaka kumsemesha mtu aliyeko duarani unamwambia "hapo chini, achama!!!!" au?!..
usisahau kupiga sample kabla hujafanya maamuzi na mwisho uwe makini na matufe ukihila ni bahati yako.....ukichumera au ukiporora ndo maisha.....ukienda maluja angalia kulia na kushoto kwanza ...
kila la kheri murah...
Asante kwa story nzuri na ya kusisimua. So hujawahi rudi Nairoto tena? Yule mmalawi hukuwahi kutana nae tena? Je ile mvua iliwahi isha na jamaa wakaendelea kupiga kazi? Vip sasa upatikananaji wa dhahabu huko Nairoto? Kuna sehem nimesoma kuna wazungu wamewekeza huko wanadai bado wanafanya utafiti wa dhahabu!!
Hiyo ni lugha ya kichimbaji hiyoHii lugha gani [emoji3][emoji3]
Sio kwamba baba mkubwa anachimba kisirisiri?Zamani sana pale jirani na kwa bamkubwa Chamwino kuna kakijiji kanaitwa nzuguni,kuliibuka Chimbo dhahabu inatema mi dogo tu wa 12-14,
nilikua najichanganya sana na maanko wangu alafu walikua watu wa vagi na ubwiii ile mbaya,
sasa walinipenda kwasababu mlinzi wao huko wakipakaza,likianzishwa nzegembe mi nachukua wallet na mali zote zinazohamishika kisha nayeya home.
Machimbo yalipoanza Nzuguni tulienda hawakuniacha bodyguard wao.
Duh kufika kule nilichoka jamaa anachosimulia ni kweli kabisa.
uzinzi,pombe,bangi, kila aina ya uasi unaukuta .ushangae sasa machimbo hata mwezi hayana.
sisi tulikua na kagroup ketu mtu nne wote mayanki tu na tulikua tunachakata vumbi tu lile.
siku kadhaa tukapatapata vimawe viduuchu yani kwenda kuuza tukagawana kahela kadogodogo tu.
Ila mi niliridhika nikasepa nikawaacha maanko maana wao hata ndoto ya kurudi hawana ilikua km wamefika nyumbani,sio hata wachimbaji wao ilikua ni pary pary tu.bangi pombe mabibi na daily wana hela wale jamaa aisee
Ila walikua mafundi malori wazuri sana KAUDO pale na Madereva.
Ule mgodi ulikatika ghafla tu,upo hapo Chamwino pembeni kushoto ukiwa unaenda kwa baba mkubwa.
Watt wa kishua hao matifu ya kijesh hawayawezi wameshazoea kudekezwa na dady na mamy hata ukimpiga na ukubwa wake wanaenda kukusemea kwa mummyyyhuna hata haya kusimulia kutoroka jeshi jinga wewe. kwa hiyo hapo umeridhika kula ugali wa shikamoo mama
ndio nyie tunawaimbaga kwenye chenja mananga wakubwa
Saa sita tayari mkuu endelea.Nipo ofisini mkuu, ni half day so kuanzia saa sita nitakuwa free, utaenjoy
Matufe yamenitishaHiyo ni lugha ya kichimbaji hiyo
Maloja-kujisaidia porin
Kuhila - kupata madini
Duarani - shimo
Moko - sururu
Matufe - udongo unao meguka kwenye kuta za shimo na unaweza kukujeruhi vibaya au kukuuwa kabisa ukikukuta huko chini
Nmepata bahat ya kukaa na wachimbaji sehem tofaut ila naona lugha yao ni moja labda kwakua wanahamahama na wanakutana
Hilo jimbo si ndo Alshabab wamelitwaa? Utayaweza mazingira ya mchakamchaka na milio ya risasi mara kwa mara?
Angalia tu usije ukahisiwa wewe ni miongoni mwao wakakumaliza askari wa Msumbiji
Cabo Delgado huko ndio eneo la mapigano. Huko watakumaliza mkuu bora urudi tena Nairoto ukaangalie upya
Umesahau fonka-shimo linalochimbwa ndani linaelekea pembeni horizontally kama mwanandani wa pembeni.Hii linatinduliwa kwa poncho na mtindo imaraHiyo ni lugha ya kichimbaji hiyo
Maloja-kujisaidia porin
Kuhila - kupata madini
Duarani - shimo
Moko - sururu
Matufe - udongo unao meguka kwenye kuta za shimo na unaweza kukujeruhi vibaya au kukuuwa kabisa ukikukuta huko chini
Nmepata bahat ya kukaa na wachimbaji sehem tofaut ila naona lugha yao ni moja labda kwakua wanahamahama na wanakutana
Kwa nilivyokusoma naona umeshapata migao mingi sana pesa tena pesa kubwakubwa kwanini usirudi Tz ubadili maisha
hahaah mkuu nimejikaza nimestaafu hizo habari kwa lazima.....huko msumbiji maduara marefu kabisa yameenda mizamo mingapi?!...Ahsante mponcha.
Ushawahi kuingia ndani ya fonka?
Mule ni kama umeshajizika tayari.
Usiku wa leo nitakua humo.