Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alikua anataka .... Tigo ?
Aha yanabei gani hayo Sista? Nataka kununuaNi Tourmaline zinaitwa zinatoka Congo huko..
Hata Tanzania zipo ila aina zingine
Nzuguni gani hiyo ambayo iko chamwino
Siku hizi umekuwa kama kaka kuona unatokea na kutoweka[emoji23][emoji23][emoji23] midundo ya ngoma haijaeleweka?Ha ha ha naona attendance yako ipo vizuri sana..kweli tufuate nyuki tukule asali..Mie najifunza hapa mbinu za kufika huko.
Mkuu hiyo stori sio mbaya nawe ukishare nasi tukapata ya kujifunza zaidi coz zote zinahusu utafutaji katika swala zima la uchimbaji wa madini ya dhahabu. Naamini kuwa uchimbaji wa madini ya dhahabu unaendana na majini coz mdogo wangu aliokota pete ya dhahabu ina kidani chekundu juu yake baada ya dada wa kiarabu kufungua pochi yake ili atoe nauli na ile pete ikadondoka kwenye siti akiwa anaongea na konda huku akichokonoa chokonoa pochi yake. Dogo baada ya kuichukua alishuka kituo kinachofuata na break ya kwanza kwa bro wake ambaye ni mimi...
Sijui nami niseme nitaendelea Kama mkuu Kitoabu ?[emoji23][emoji23]
Basi bhana, baada ya kunieleza nikatoka nae mpaka kwa sonara wa kihindi. Yule sonara baada ya kumuonesha tu alipandisha mashetani, eh alipoanza kupiga kelele kwa maneno ya kiarabu na kutimua mbio na watu wengine wote waliokuwepo pale jumlisha na sisi wote mbio huku nimeishikilia mkononi.
Tukakaa sehemu na mdogo wangu nikimhoji maswali huku nami nikianza kuiogopa ile pete. To cut the story short tukaenda kwa sonara mwingine Kariakoo naye ni muhindi ofisi yake ikiwa inanuka ubani tupu, alipoiangalia akatuuliza mmeipata wapi huku akitukazia macho. Hapa nikaona yasijeyakatokea yaleyale ya kule Ila imani yakupata pesa ilikuwa imenijaa nikamkazia kwa kumdanganya kuwa mama ametupa tuje kuiuza kwasababu anaumwa. Akatuangaliaa Sana huku akiiangalia Ile pete, bila kuipima wala nini akasema nawapa laki 5 na elfu alobaini. Aisee sikutegemea, mi nilijua tutauza laki ikizidi sana laki moja na nusu, Sasa kusema laki tano nikakubali fastaa...
Text yangu hujaiona?Mkuu hapo mulimpa ulaji huyo muhindi.
Hapo mulikua munauza Pete kama yenyewe, na kidani munge kiuza chenyewe.
Tena hapo, kati ya Pete (dhahabu) na kidani chekundu (Ruby) hicho kidani ndio chenye thamani.
Hicho kidani kikifika points 4 tu ni zaidi ya Milioni moja.
Kwahiyo inamaana Muhindi alichukua kidani /Rubby halisi na kuwaachia jamaa jini lao?!Mkuu hapo mulimpa ulaji huyo muhindi.
Hapo mulikua munauza Pete kama yenyewe, na kidani munge kiuza chenyewe.
Tena hapo, kati ya Pete (dhahabu) na kidani chekundu (Ruby) hicho kidani ndio chenye thamani.
Hicho kidani kikifika points 4 tu ni zaidi ya Milioni moja.
Dom,hapo kabla au baada ya ikulu unachapuka kushoto juu milimani huko watu walichimba dhahabu maybe hata hujazaliwaNzuguni gani hiyo ambayo iko chamwino
Habari za asubuhi wakuu.. Naimani kila mtu yuko powa na familia yake siku ya leo na kwa mabachelor mmeamka salama. Kwa washabiki wa mpira tupeane pole maana Tunisia si level yetu, hakika walistahili kutufunga. Naendelea na stori Kama nilivyowaahidi.....Nifupishe... Ilipofika asubuhi pamoja na ukristo wao wazazi wetu lakini walikubaliana na mzee mmoja jirani yetu watupeleke kwa shekhe mmoja hivi. I can't differentiate him with mganga ila ye anachora chora kwenye karatasi alafu anawaambia nini hasa kilichotokea, kilichopo na nini chakufanya.
Yule shekhe ndio akaanza kusema, aisee over alikuwepo na mdogo wangu kwa jinsi alivyokuwa anasimulia mpaka sonara wa kwanza kupandisha majini maana alikutana na jini lenye nguvu kuliko yeye likamuonya. Kumbe kile kidani chekundu juu ya pete ni jini lilikuwa limewekwa kwenye mfumo wa kidani kwenye Pete ya dhahabu kwaajili ya kazi za yule mwanamke (Hapa sitaingia into details maana hayahusu hii simulizi). Akamtaja mpaka jina la hilo jini kuwa hatatuacha kwasababu tumempeleka sehemu (kwa sonara yule wa pili) amefukuzwa so anatufuata sisi tumrudishe sijui wapi yule shekhe alisema.
Sisi tukaombewa ombewa pale na yule shekhe alafu tukapewa dawa ya kuoga kwa siku saba yaani unaichanganya kwenye maji ya kuoga. Sisi tukatolewa nje ndani wakabaki baba, yule mzee aliyemshauri baba twende kwa huyo shekhe na shekhe mwenyewe wakijadili jambo.
Kutoelewa hizo issue kulichangia mkuu. Mi laki tano niliona hela nyingi hata sikuuliza mara mbiliMkuu hapo mulimpa ulaji huyo muhindi.
Hapo mulikua munauza Pete kama yenyewe, na kidani munge kiuza chenyewe.
Tena hapo, kati ya Pete (dhahabu) na kidani chekundu (Ruby) hicho kidani ndio chenye thamani.
Hicho kidani kikifika points 4 tu ni zaidi ya Milioni moja.
Ikulu iko wilaya ya chamwino km Kama arobaini kutoka town,nzuguni ni town kabisa karibu na ihumwa kaka.dala dala mia nne tu labda umetoka kitambo dom na ulikuwa mdogoDom,hapo kabla au baada ya ikulu unachapuka kushoto juu milimani huko watu walichimba dhahabu maybe hata hujazaliwa
Yes na pia sikuwa mkaziwa Dom nilipita tu.Ikulu iko wilaya ya chamwino km Kama arobaini kutoka town,nzuguni ni town kabisa karibu na ihumwa kaka.dala dala mia nne tu labda umetoka kitambo dom na ulikuwa mdogo
hao jamaa ni dhaifu mkuu kuliko unavyoweza kudhani....na wana limitations nyingi kuweza kumdhuru mtu ila wakikukuta mwili uko free uko biased na maovu na takataka nyingine hakuna rangi wataacha kukuonesha..Yaani ninavyosimulia hapa, picha kamili inanijia kichwani kwasababu nakumbuka Kila kitu mpaka sura yake ingawa ilikuwa usiku. Mkuu acha kabisa kuonana na viumbe hivi
Banaaaaah mbona hvyio me ngoja me niende choon kwanz nikirud naic itakua tayar.Habari za asubuhi wakuu.. Naimani kila mtu yuko powa na familia yake siku ya leo na kwa mabachelor mmeamka salama. Kwa washabiki wa mpira tupeane pole maana Tunisia si level yetu, hakika walistahili kutufunga. Naendelea na stori Kama nilivyowaahidi.....
Tuliambiwa ile dawa tuoge asubuhi na usiku kabla ya kulala na kunuia maneno flani ya kumfukuzia yule kiumbe. Ile laki mbili alivyokuwa nayo dogo baba aliamua kumpa yule shekhe (sijui aliitumia au aliichoma moto kama alivyodai?🤷 Vile vitu vingine shekhe alivifuata nyumbani ili akavichome Moto pia). Sasa ilipofika usiku wa ile siku mimi na mdogo wangu wote tunaogopa kwenda kulala chumbani. Hiyo ni j'tatu na chuo sikwenda kwa hofu ya lile dude kunitokea chuoni nikiwa peke yangu, pamoja na kupewa Ile dawa na kile kisomo bado nilikuwa nimejawa na hofu so nilitaka kuwa karibu na baba maana yeye ndio alikuwa anaonekana jasiri kuliko wote. Mama yeye baada ya kusimuliwa na mzee aliyosema yule shekhe alibaki kulia na kuomba tu huku akimwomba (kumlazimisha mzee atupeleke kwa Kakobe). Usiku ilipofika baba akaamua kulala na sisi chumbani, kwakweli usingizi haukuja, mapigo ya moyo yapo juu, nikimwangalia dogo nae dogo ananikodolea macho tukiwa kitandani mzee kalala chini, pembeni ya kitanda. Mida ya Kama saa saba sijui saa sita (sikumbuki muda sahihi) usingizi ukatupitia, nakuja kushtuka.....
Wanaoanzisha hizi story venye tunawabembeleza wanaenjoy kinoma ani
Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Unaenda Cabo del Gado kwa magaidi?![emoji44][emoji15]Pale nilipo kaa (kuwangoja washkaji) usingizi ulinipitia nililalaa mpaka nilipo amshwa na makelele ya washkaji.
Sijui nilitumia muda gani kwenye usingizi ule ila nilipo angalia saa ilikua ni saa 6 mchana.
Nilipo amka nilikutana na kijua kikali utadhani niko Sudan, yani mpaka nguo nilizo vaa zilishaanza kunyauka.
Chakwanza niliwauliza kuhusu yule mmalawi, nikaambiwa bado wako camp wanaendelea kungoja mvua iishe waanze kazi.
Nilipo wauliza vipi kama mvua imeisha huko walikotoka, wakaniambia mvua imenyamaza sasa hivi baada ya kuvuka lile korongo.
Yani kumbe mvua inaanzia kwenye korongo kwenda matandani, ila kulimaliza korongo mvua hakuna.
Tulitembea mpaka kijijini, hakuna alie jua kua mimi nina dhahabu mbeleni.
Tuliingia kijijini saa 2 usiku, hapo tukalala.
Ila kwakua tulisha fika kijijini, kila mtu aliendelea kimpango wake.
Pale kijijini kila mtu anaham ya kujua kulikoni huko porini.
Nakumbuka nilitulia kwenye kiosk cha jamaa flani hivi, kila mtu alikua ananiuliza kuhusiana na porini.
Usiku kucha nilikesha kwenye kile kiosk cha jamaa nikila Royal gin (hii ni pombe kali sana) mpaka kuna kucha.
Kwakua nilikua na pesa ya kutosha niliyo chukua kwenye lile duka la marehem, hivyo ilikua mwendo wa kujimiminia pombe.
Kuna dem alinitamani nika lale kwake, lakini nilikataa kwa kuhofea asiniibie dhahabu yangu.
Migodini wanawake ndio wanaongoza kutuibia wachimbaji.
Kilicho fanyika nikumpa pombe mpaka dem akakimbia.
Asubuhi, sikutaka kulemba, na pombe zangu kichwani, nikakamata piki piki mpaka Montepuez.
Montepuez, hapa ndio kuna soko la madini yote.
Nikaingia kwa msirilanka nikapima dhahabu.
Dhahabu ilikua na uzito wa gram 112, kila gram kwa kipindi kile ilikua 2000 miticais sawa na laki moja shilingi kwa wakati huo.
Nikachukua 224,000 miticais, hapo akili yote inamuaza mama Abuu (Shemeji yenu)
Nakumbuka nilinunua piki piki na mazaga mengine kama nguo.
Nikatuma kama 60,000 miticais (sawa na Milioni tatu kipindi hicho) kwa mama yangu Tanzania, maisha yakaendelea.
MWISHO.
Naahidi kuwahabarishine matukio mbali mbali yanayo / yatayo tokea hapa mgodini nilipo.
Kumbuka kwa sasa naishi Tete, Muatiz, ila kwa hizi mvua zilizo anza kunyesha, nategemea kurudi Cabo del Gado wilaya ya Montepuez, nikatafute Ruby.
Hapa nangoja hii kazi iishe, nione kama nitaokoa chochote kinisogeze kwenye Ruby.
Ahsanteni na kwaherini.