sasa hitimisho...
baada ya matibabu na kila kitu kukaa sawa ikawa sasa siyo siri kwamba mimi nimepata ulemavu na wale jamaa wamepotezwa na tamaa ya kutaka rupia za wajerumani,ile habari iliongeza sana hofu kuhusu ule msitu pia sikuwa napenda sana simulia lakini watu walikua wanasimuliana habari nyingi sana za uongo kuhusu lile tukio letu...
wengi walikua wanazipata kwa mangi,baada ya kuwa chizi ilikua wanamwita wanampa hata ubwabwa kama mzee rungwe anafunguka lakini vyote anasema ni uongo uongo sababu ya kuwa chizi
mimi bahati sana kazini sikufukuzwa na kibarua changu kilikua hakina uhusiano sana na matumizi ya huu mguu so nikaendelea kupata kipato ila sasa ikabidi nianze utafiti wangu usio rasmi kuhusu nyumbanitu na mambo ya hizo mali za wazungu
...kama niliyoyaona mule ndani ni ya kweli basi hizi mali zipo,kama hazipo basi kuna kitu na uchawi upo kabisa real
mambo yasiyo kawaida niliyoona mule
zile chain kushuka shimoni
beacon
michoro mbalimbali ya ajabu
ule mwanga mkali
sauti ya ajabu
kusisimka nywele
haya tu yanatosha kusema kwamba kuna activities zilishafanyika huko miaka ya zamani sana lakini kuna uchawi mkubwa ulifanyika kuzilinda,kwanini kuwe na zile chain zimeshuka chini na kwanini haya maeneo mengi ya aina hii huwa yanaambatana na miiko gulani na vitisho kuhusu kulifikia eneo hilo?!!
.....haya maeneo mengi yanaambatanaga na uwepo aidha wa hifadhi au makanisa au shule / hospitali hasa makongwe especially ROMAN CATHOLIC,lutheran na moravian,makanisa mengi yamejengwa juu ya hizo mali na maeneo ambayo hakukua na uwezekano wa kujenga makanisa basi ndio walifanya uzushi wa kufanya yaogopwe.
Kuna sekondari ya moravian zamani inaitwa rungwe iko tukuyu mbeya,iko mission ya makao makuu ya kanisa la moravian kanda ya kusini...kuna habari za kutisha sana na kuna mahandaki ya wazi kabisa kuanzia baadhi ya vyumba yametokomea huko chini gizani ambako hakuna anayejua ni wapi,kuna kipindi moja lilishawahi titia assembly
Pia makanisa mengi ya roman mkoa wa Njombe(ndio nina uzoefu nako zaidi) yanafanana ramani kwa yake ya zamani na kuna maeneo ambayo ni restricted kufika,kunakua aidha na misitu mikubwa au kitu tu kinaogopwa bila sababu...nilipokuepo kila mwaka wazungu walikua wanakuja kuanzisha project fulani ambazo ni za kijinga hivi na hazidumu na zote lazima zihusishe kuchimba na hapo hawataki wasaidizi kabisa weusi na wanafanya kazi usiku na mchana.
Pale Rungwe kila mwaka lazima mwanafunzi apotee na tukio la karibuni nililosikia na kuhakiki kuhusu pale ni kifo cha utata cha dogo wetu mmoja wa njombe iliripotiwa 2011/2012...mwaka huo huo alipotea mtoto wa kidato cha tano porini lakini huyu alifanikiwa kupatikana akiwa hai amechoka sana baada ya kufanywa mila na wazee wa kwao sumbawanga,baada ya siku kama saba hivi.
Kuna mahala kijijini Njombe huko alikuja mzungu akaanzisha project ya kulima kabichi,alikaa miaka mitatu hivi na aliwekeza vifaa vya gharama sana...siku ya siku usiku aliondoka yeye na briefcase zake kadhaa chini ya escort na aliacha kila kitu hapo watu walijiokotea tu vitu...hajawahi rudi hadi leo.
Nina mifano kadhaa...sababu baada ya ile nimekua mtu wa kudadisi sana kuhusu haya mambo ndio maana pia nilivutiwa kusoma uzi wa
Kitoabu.
Kwahiyo hizi mali zipo ila sasa wazungu kama ambavyo walitutangulia kwenye kila kitu basi hata uchawi pia walitutangulia..wao uchawi wao ni mkali sana kuliko huu wetu na kwa sasa uchawi wao uko next level,huwa nawaza hivi inawezekana vipi eti nyimbo zinakaa kwenye simu jamani[emoji1][emoji1] eti picha unaweza print kwenye karatasi na kila rangi ikatoka hapo bila utata...na teknolojia zote hizi za ajabu,siku hizi wanaprint hadi nyumba[emoji1787][emoji1787][emoji1787](utani huu lakini unafikirisha)....wazungu wako mbali kwenye kila kitu,huu uchawi sisi tunafanya leo wao walifanya wakati wa biblia zinatungwa so ipo siku na sisi tutafika huko lakini watakua tayari mali zao wamebeba kitambo sana.
Hizi mali wamezifanyia ushirikina mkuu sana ambao hakuna huko bongo au kama wapo basi wachache,imagine mtu kuona tu hayo masanduku unaishia kuwa kichaa...hii kupata kichaa ni kukupumbaza usirudi tena huko kufanya tena ujinga uliojaribu kuufanya...ni kama wanakupa second chance kuishi lakini sasa na onyo kwamba tafuta mali zako acha kuvizia walizotafuta wenzio...kwangu ni mila zimenisaidia ila wameniacha na onyo pia,ndio maana nikiona hata watu wanazungumzia habari za kwenda kuiba rupia au madini ya wazungu wanasikiliza nawaacha hapo nahama kijiwe.
Kwenye mkoa wetu ni ndoto ya kila kijana,sasa ni sabBu kila tajiri kule inasemekana lakima awe ameingia kuzindikwa humo...Njombe huwezi kuwa na fedha ukaishi kama siyo mshirikina,kule ni kawaida kujua mtu kaua hata mzazi kwa panga na kila mtu anajua na kijana anakua na fedha mbaya...kule kukuta tajiri analala chini kawaida ,tajiri hazai ndio ilikua maarufu sana,unakua na mtoto mmoja tu kwenye huu ulimwengu wa nyama na wengine wote unazaa na majini ila mkeo akishika tu mimba lazima afe na hiyo mimba(nina ushahidi na hili,yuko tajiri mmoja huko ndio aliporogea)
Wazungu huwa wanakuja,nilisema wakati naanza moja ya masharti waliwapa watawala wetu ili waachie uhuru wa kujitawala ni kuwaachia mali zao na pindi watakuja kufata hakuna wa kuwabugudhi hata baada ya miaka milioni(haya mambo ya siri kubwa sana za nchi,ndio zile ambazo kiongozi mkuu anatakiwa kuijua yeye tu) na mengine mengi...hii ni sababu wao wakirudi wanazichukua kirahisi kabisa tena kwa ulinzi mahususi chini ya watu wa intelijensia.
Nilipoteza mguu kipande lakini nikapata maarifa na akili kwamba hakuna mali za shortcut,ili tufanikiwe lazima tupambane kupata vyetu kwa njia halali(kama unataka kula na kuvaa ili usife)
Ila ili uwe tajiri lazima uchague imani unasimamia
1.kama ni kwa Mungu(dini) basi shikana nayo haswaaa ,hili kundi matajiri wachache au hawapo kabisa,wengi wanajificha makanisani kujiosha ila ni wachawi wakubwa...walio pure na imani na ni matajiri kwa imani hizi haba ni kama hawapo kabisa.
2.kama ni kwa ushirikina basi shikana nao haswa na hapa ndio matajiri na utajiri uko nje nje,ngumu sana kutenganisha utajiri na uchawi..hela ni za shetani kwahiyo huwezi kukaa nazo kama huna ushetani,hapa ndio wale wauza viungo wanakuja.
Kuhusu Njombe watu walikua wanauliwa kwa imani ukienda mgodini lazima utatema...wavuvi wa ziwani ndio wanatumia sana vipande na miili ya binadamu kufanya uvuvi na wanatoboa.
Tutaendelea kupiga soga hapa hapa ila kwa ipande wangu nimemaliza.
Nilitaka mali nikaishia kupoteza kipande cha mguu na marafiki wapendwa wanne katika mazingira ya kutisha na kuogofya.
#tufanye kazi.
[emoji1317]