Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Mkuu ndio nimemaliza kuupitia[emoji28][emoji28][emoji28]
Yule mvuvi ni tatizo, kwanza ye maswali anajibu yale tu anayoamua, halafu katika maswali 50 anaweza kujibu matatu tena juu juu au tofauti ya yalivyoulizwa,
Sema ule uzi umenifurahisha sana

Asante mkuu kwa kunipa burudani

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
😃😃 Ameniquote juu hapo. Alikua ananifurahisha tu
 
Part II
Nisahihishe jambo moja, maranyingi huwa sipendi kuandika kutokana na kazi zangu.

Mimi sio muajiliwa, mimi ni mchimbaji, kwa hiyo maisha yangu ni yakushea na washkaji.

Some time naweza nikawa naandika jambo mala anatokea mtu (rafiki) anaanza kuniongelesha, kwa hiyo inanibidi niache kuandika nimalizane nae kwanza.

Kwahiyo munisameh kwa hilo.


************************************************************************,,*************

Kwenye safari ile nakumbuka niliongozana na mdogo wangu (Mtanzania mwenzangu pia kabila letu ni moja ) Dogo Chiko.

Tulitoka Nanhupo kuelekea nairoto kwenye dhahabu.

Tulifika Nairoto kijijini kisha pakesho yake tukaelekea polini (machimbo)

Kwanza pale kijijini tulikutana na umati wa watu usipime.

Kila mtu akiwa na shauku ya kufika polini.

Kesho yake palipo pambazuka kila mtu alikua tayari kwa safari ya kuelekea polini, me na chama langu (dogo Chiko ) tuliukanyaga kwa mguu kutokana na kutokua na nauli ya piki piki.

Nauli kwa mtu mmoja kutoka pale kijijini kwenda polini ilikua 500 quinhento miticais sawa na 25000 ishirini na tano shilling.

Tuliukanyaga mwendo wa masaa 12 kwa mguu, nakumbuka tuliingia matandani kama mida ya saa moja usiku hivi.

Lakini kwa mgodini (japo ni polini) tulikuta kama tuko mtaa wa kongo.

Watu ni wengi mno, vijana wa kiume na wakike, mabibi na mababu, mpaka watoto wa miaka 7.

Kila aina ya laana ilikua inapatikana huku, Vifo (kuuana) ubakaji, kutiana vilema yani ni kama kupakaa mafuta tu.

Pombe gani unayo itaka utaikosa, Heineken,Savana, breezer na mapombe kibao ya gharama.

Malaya kutoka kila pembe ya Africa.
Wamalawi, Watanzania, na wenyewe Mocambique.

Kiufupi huu ulikua uwanjani wa madhambi.

Nakumbuka nilifanya kazi kama week mbili tu, mala ghafla ukaibuka ugonjwa wa ajabu matandani pale.

Watu walikua wakibadilika rangi na kuharisha mwisho kifo.

Yani unaweza kukaa na mshikaji mala ghafla akaanza kubadika rangi ya macho yake, akienda kujisaidia akirudi (wengine walikua hawarudi) unamuona mwili wote ume badilika rangi kawa wanjanoo, hapo amalizi saa munamkimbia.

Halii hii ilitamba siku mbili tu, siku ya tatu matanda yote nyeupe.

Watu wote tulikimbia kurudi kijijini, sasa balaaa lilikua njiani.
Watu wengi walifia njiani, tulio tusua ni wachache sana.

Nakumbuka msafara wetu (wakurudi kijijini) ulikua na watu 8, kati ya hao wawili tuliwaacha njiani, (walifia njiani).

Moja kati ya watu hao ni Rafiki yangu kipenzi (mdogo wangu) Dogo Chiko, na mshikaji alieitwa Wamisunjo (Mateas)

Nakumbuka tulikiamsha kutoka matandani pale mida ya saa4 asbuh, tulitembea umbali mrefu, mdogo wangu Chiko akatuambia tumngoje anaenda kukata gogo (kunya)

Tulimngoja, tulikaa chini mwenye sigara aliwasha, mwenye bange lake alilipua, mwenye maji alikunywa.

Muda ulipita mara Chiko akarudi, na safari kuendelea.
Lakini kila tulipo muangalia usoni, macho yote yame badilika rangi nakua yanjano.

Tukampa maji na safari ikaendelea.

Hatukufika mbali sana, Chiko akaomba tumsubiri anakwenda tena kujisaidia.

Tilipu hii tulimngoja bila dogo kurudi, ikabidi mshikaji mmoja amfuate.
Alipo fika kule alimkuta chiko kesha kufa.
Jamaa akatuita tuje kumcheki, nikiwa mingoni mwao nilimkuta dogo amesha kauka pale alipo kaa.

Kwakua tangu tuna toka matandani tulishaambiana kua ugonjwa huu ni kipindu pindu, hivyo ukifa hakuna mtu alie thubutu kukushika.

Kwahiyo Dogo Chiko tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.

Nitarudi muda si mrefu.
 
Part III
Safari iliendelea huku kila mmoja sasa anamuogopa mwenzie, kila mtu anaamini kile ni kipindu pindu.

Baada ya mwendo mrefu Wamisunjo akaanza kukosa nguvu ya kutembea.
Tumbo lilianza kumuuma na kila baada ya hatua kadhaa jamaa alikua akituomba tumngoje akajisaidie.
Baada ya mwendo mrefu Wamisunjo alishindwa kutembea nakutuambia ambia tumuache yeye hawezi kutembea.

Kwakua kila mtu alikua na uoga wa kuambukizwa, hakuna alie thubutu kumbeba, tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.

Tulifika kijijini usiku kama saa 6 usiku.
Kijiji kulikua kumejaa huzuni tupu.
Nakumbuka kuna brother mmoja wa kinyakyusa (jina nimelisahau) nyumbani kwake kulikua na maiti kibao (kitu kama 19 hivi) zilikua zime tandazwa barazani.

Nyingi ya maiti hizo zilikua za watoto wa Mbeya.
Hawa walikua wanamiliki vingwendu (mashine za kusachia dhahabu)

Tulikaa pale kijijini kama week hivi, mwenye bahati ya kuwaona ndugu zao waliwaona wasio na bahati ndio basi tena

Kwa upande wangu nilipotezana na wengi, wengine walikufa, wengine ndio kama huyu mshikaji nilie kutana nae leo asbuh.

Yani ni miaka 5 ndio kwanza nakuta nae leo, mshikaji alikua kwenye misele hii hii yakwangu sema sehem nyingine.

Ndani ya week ile wengine walirudi walikotoka, wengine tuliendelea kubaki kwa kukosa nauli.

Mala zikaanza story za chini chini kutoka kwa wanakijiji wapale (nairoto)

****************************************************************************************
Wachimbaji wa mwanzoni kabisa baada ya kugundua dhahabu kwenye korongo lile, walienda mpaka kwa mwenye (chifu) wa kijiji kile na kumueleza azma yao ya kuchimba.

Chifu akawakubalia, ila kwa masharti ya kutovuta bange, sigara, pombe, wanawake wawapo polini.

Wachimbaji walikubali japo walijua kua masharti hayo kwa mchimbaji ni magumu na hayawezekani tu.

Jamaa wale walichimbaa na kila siku dhahabu ndio zilikua zikohowa tu.

Dhahabu zilitoka ile mbaya mpaka sisi wa mbali mlio ukatufikia.

Kama desturi ya mchimbaji, bila vileo (bombe, sigara, bange, wanawake) haendi.
Ikabidi washauriane kwenda kuomba kwa Mwenye, waruhusiwe kuishi maisha yao.

Walivyo fika kwa mwenye, Mwenye akakataa.
Akawaambia mizimu ya huko haitaki vitu hivyo, kwahiyo yeye haruhusu ila kama wanataka kutumia vitu hivyo ni hiari yao.

Wachimbaji walivyo rudi polini wakaanza kutumia vitu vyote.

Sigara, bange, gongo ndio vitu vya mwanzo kuingia.
Lakini kadili siku zilivyo kua zina songa ndio laana ikawa inaongeza polini.

Wanawake wakawa wengi, biashara ya ngono ikawa rasmi polini.

Polini kukawa mjini na kijijini kukageuka mstuni.
Ilifikia hatua mtu wa kijijini anakuja kutumia polini.

Baduka yakafunguliwa, bar zikawa zimezagaa.
Polini lakini mziki unagongwa utadhani uko lidas.
Mabanda ya video kama kawa.
Kiufupi poli liligeuka uwanja wa laana kwa muda mfupi tu.

Mpaka nafika mimi pale polini nilikuta kila kitu cha mjini kiko kule.

Nakuja kidogo.
 
Mkuu ndio nimemaliza kuupitia[emoji28][emoji28][emoji28]
Yule mvuvi ni tatizo, kwanza ye maswali anajibu yale tu anayoamua, halafu katika maswali 50 anaweza kujibu matatu tena juu juu au tofauti ya yalivyoulizwa,
Sema ule uzi umenifurahisha sana

Asante mkuu kwa kunipa burudani

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Yaani yule jamaa alinidissapoint sana
Nilitegemea kujua mengi nikaishia kusoma malumbano ya mabaharia
 
Part IV
Baada ya laana kukithiri polini, Mwenye (chifu) akawatangazia wanakijiji wenzie wawakataze vijana wao wasiingie polini.

Kwakua watu tulikua wengi hakuna alie jua kua wenye kijiji wametususia poli.

Laana iliendelea mpaka ulipo lipuka ule ugonjwa.

****************************************************************************************

Baada ya story hiyo kutapakaa karibu kwa kila mchimbaji, mala majadiliano yalianza.

Kwanza tulijiuliza kama ule ugonjwa ni kweli kipindu pindu mbona tulivyo fika kijijini pale na ugonjwa ulikoma?

Kulikua kuna watu walikua wanaeza habari za mzungu kutia sumu kwenye maji tuliyo kua tunatumia kwenye shughuli zetu mbali mbali.

Lakini swali likaja, kama nikweli sumu, mbona wanaokufa ni wanaume tu? ( na nikweli, kwenye kisanga hichi hakuna mwanamke alie kufa)

Tena ukizingatia walikua wanakufa wengi ni wanunua dhahabu, wafanya biashara wengine, na wanaozunguka na vingwendu.

Kumbuka watu hao wote, machimboni hunywa maji ya dukani.

Jibu likaja kua kuna masharti yamevunjwa.

Watu wakatiana moyo wa kwenda tena polini.
Ikapangwa siku, mwenye kutaka kwenda polini aungane twende.

Nikajifikilia, na mimi nikajipa ujasili wa kuungana na kikundi kitacho rudi tena polini.

Kilicho ni shawishi kikubwa niliamini kuna watu wengi walikua wamekufa na dhahabu mfukoni, hivyo niliamini lazima nirudi na dhahabu.
Pili nilikua nashauku ya kujua kama Wamisunjo alifia pale ama alitoboa mpaka kijijini?

Kulipo kucha safari ilianza.
Safari ilikua ya mtu kama 20+ hivi.

Ila kabla ya safari tulikubaliana hakuna mtu kubeba bange, sigara wala pombe.

Safari ilianza rasmi ya kuelekea polini, njiani tunapishana na maiti, upigi hatua kumi bila kukutana na maiti.

Asikuambie mtu binaadam akifa ananuka balaaa.

Yani ilikua ni mwendo wa kushikapua mpaka unataka kutapika.

Tulitembea mpaka pale tulipo muacha Wamisunjo, nikamkuta jamaa wamemjalia nzi tu, yani hata kumkalibia nilishindwa kwa huzuni.

Safari iliendelea mpaka tunafika matandani.

Tulipo fika matandani, maiti zenyewe hizo! Kama kwenye movies vile.
Kila upande zime jazana maiti tu, kuna harufu mbaya, kama huna moyo wa ujasili lazima utapike.

Tulizunguka polini pale lakini tulishindwa kufanya kazi kutokana na hali halisi.

Tukajadiliana kwamba watu kumi wafuate petrol watu wengine tubaki tukizisomba maiti na kuzi weka sehem moja kisha tuzitie moto.

Kwa wingi wa maiti zile na kuharibika vile ilikua ngumu kuzizika, hivyo wazo wa kuzichoma moto lilikua wazo zuri.

Tukatafuta sehem mbali kidogo na matandani, tukalala.

Hapo uliwashwa moto mkubwa, hapo ni story za kupeana moyo tu husu maisha, kila mtu anaongea lake mpaka asubuhi.

Kulipo kucha wale kumi walielekea kijijini kufuata petrol, na sisi wengine tukaanza kuzisogeza maiti sehem moja (zile zilezo kalibiana.

Mfano fungu moja unakuta maiti tano, fungu lingine watatu kutokana na ukaribu walipo fia.

Nakumbuka mimi na brother mmoja (huyu ni mmalawi) tuliingia ndani ya duka moja hivi, tukamkuta mwenye duka kafa kwenye kiti chake kaa tu.

Tulipekua duka lote (japo kunanuka)mara ya kwanza tuliambulia pesa tu, jamaa nilie nae akania huyu maiti alikua ananunua dhahabu pia hivyo tuwe makini katika kusachi kwetu tusije pishana na dhahabu.

Harakati za kumsachi mfukoni, tukamvua viatu, wapi?
Tukamvua nguo zote (kwa tahadhari ya hali ya juu) hapa tukamkuta na donge la dhahabu kwenye kipochi kidogo cha shingoni, ila marehem alikua kakivaa kiunoni.

Uwezi amini huyu marehem alikufa na biashara yake ikiwa imejaa.

Nakumbuka tulibeba Dragon baadhi ya kasha na kwenda kunywa mbele (hapa tuliapa hakuna mtu kugusa pombe )

Siku ilisha tukizikusanya maiti tu na kuzisachi, mwenye bahati ya kukutana na dhahabu ni ya kwake.

Tulipo gundua kua maiti nyingi zimekufa na dhahabu mikoni, kazi ya kuzikusanya haikua ngumu tena, wala kile kinyaa kikapotea.

Tukaanza kuzigombania maiti kila mtu anataka kusachi, mwisho wa siku tukaingiwa na kama wazimu hivi.

Nakumbuka kuna jamaa walizichapa (nusura wauwane ) wakiigombania maiti moja hivi.
Kuna mmoja kati yao anadai anamfaham malehemu, hivyo yeye ndie mwenye haki ya kuchua dhahabu ya marehem......

Narudi muda si mrefu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Nimekuelewa mkuu.
Tatizo maisha ninayo ishi ni mchaka mchaka kinoma.
Mfano jana usiku kucha tumekesha hospital, kuna mtanzania mwenzetu (mtoto wa songea) kapigwa shoka na mrundi.

Hivi ninavyo andika, mtanzania mwenzetu ishakula kwake, akipona sijui!!!

Kitacho tokea hapa, ni mapambano ya Wabongo na warundi hapo baadae, maana Wabongo wameapa kutokukubali.

Kwahiyo Kiufupi muda wa kukaa na kuandika kwa utulivu nakua sina.

Cha muhimu tuvumiliane.
 
Mzee Kitoabu nawe upo kwenye list ya waleta faraja humu jf japo Kuna wengine tunawadai mastori wa Kwanza

jerrybanks na stori yake ya Mambo ya giza mwingine yule msimuliaji wa Vita ya Rwanda

Bossless sema simu yake ilipasuka stori ikaanza kuwa na utata japo tunamdai aje mwingine mzee wa Swizz

Parabora huyu Mwamba naomba uje na ID nyingine alete vitu vya Europe na malysia, Singapore huko, mwingine n

digba sowey na stori ya kushuudia uchawi sema ule Uzi ulivamiwa na walolokole mbaya zaid n single mamaz waliaribu Uzi, yule

jooohs na story yake ya masharti ya kutumia Dawa kutoka jwa mganga ili pesa zimtafute

Habibu B. Anga aendelee kuwauzia tuu wasioelewa stori za kucopy na kutafsir japo kutafsir n Kaz Ila kuuza sio mzee.

Kwa ujumla mnatupa vitu ambacho vipo Ila kwa maana nyingine sie wengine hatujakutana navyo na vinatupa funzo zuri katka maisha hvyo msisite kuleta stori Kama hzo Kwan usisimua akili na funzo pia hvyo tunawaomba mrejee kwenye nyakati za dhama zetu
 
Shukrani mkuu

 
Aisee!
mkuu hapo tumeisoma namba sana.....mimi nimepambana migodi mingi tumelala nje maporini saaana.....kuna pori moja tuliwahi kwenda baada ya kuskia mlio ebwana kulikuwa na baridi kali njombe kukasome.....kiasi kwamba baridi ya pale jamaa tunalala tunapangana kama 7 hivi miguu inaelekea porini vichakani....sasa ukali wa ile baridi mpaka mtu anaota anavutwa miguu na fisi.....unashangaa mmelala usiku wa manane mtu anaamka anapiga yowe "yalaaaaaaaah fisiiiii" yan ananyanyuka watu wote wanaamka wanasimama wanasukumana oya nini nini! huku wametupa mashuka af aliyepiga kelele kumbe yuko usingizini anarudi kulala na haelewi kilichotokea....basi hapo hakuna kulala tena..
geomex
 
Back
Top Bottom