Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Nairobi hawauzi Tecno moja moja. Zinapangwa kwa mafungu ya kuanzia tatu mpaka tano. Ukinunua fungu kubwa unaongezewa ka Tecno tochi🤣🤣
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nairobi hawauzi Tecno moja moja. Zinapangwa kwa mafungu ya kuanzia tatu mpaka tano. Ukinunua fungu kubwa unaongezewa ka Tecno tochi🤣🤣
😲😲Usirudi tena
😲😲Nisahihishe jambo moja, maranyingi huwa sipendi kuandika kutokana na kazi zangu.
Mimi sio muajiliwa, mimi ni mchimbaji, kwa hiyo maisha yangu ni yakushea na washkaji.
Some time naweza nikawa naandika jambo mala anatokea mtu (rafiki) anaanza kuniongelesha, kwa hiyo inanibidi niache kuandika nimalizane nae kwanza.
Kwahiyo munisameh kwa hilo.
************************************************************************,,*************
Kwenye safari ile nakumbuka niliongozana na mdogo wangu (Mtanzania mwenzangu pia kabila letu ni moja ) Dogo Chiko.
Tulitoka Nanhupo kuelekea nairoto kwenye dhahabu.
Tulifika Nairoto kijijini kisha pakesho yake tukaelekea polini (machimbo)
Kwanza pale kijijini tulikutana na umati wa watu usipime.
Kila mtu akiwa na shauku ya kufika polini.
Kesho yake palipo pambazuka kila mtu alikua tayari kwa safari ya kuelekea polini, me na chama langu (dogo Chiko ) tuliukanyaga kwa mguu kutokana na kutokua na nauli ya piki piki.
Nauli kwa mtu mmoja kutoka pale kijijini kwenda polini ilikua 500 quinhento miticais sawa na 25000 ishirini na tano shilling.
Tuliukanyaga mwendo wa masaa 12 kwa mguu, nakumbuka tuliingia matandani kama mida ya saa moja usiku hivi.
Lakini kwa mgodini (japo ni polini) tulikuta kama tuko mtaa wa kongo.
Watu ni wengi mno, vijana wa kiume na wakike, mabibi na mababu, mpaka watoto wa miaka 7.
Kila aina ya laana ilikua inapatikana huku, Vifo (kuuana) ubakaji, kutiana vilema yani ni kama kupakaa mafuta tu.
Pombe gani unayo itaka utaikosa, Heineken,Savana, breezer na mapombe kibao ya gharama.
Malaya kutoka kila pembe ya Africa.
Wamalawi, Watanzania, na wenyewe Mocambique.
Kiufupi huu ulikua uwanjani wa madhambi.
Nakumbuka nilifanya kazi kama week mbili tu, mala ghafla ukaibuka ugonjwa wa ajabu matandani pale.
Watu walikua wakibadilika rangi na kuharisha mwisho kifo.
Yani unaweza kukaa na mshikaji mala ghafla akaanza kubadika rangi ya macho yake, akienda kujisaidia akirudi (wengine walikua hawarudi) unamuona mwili wote ume badilika rangi kawa wanjanoo, hapo amalizi saa munamkimbia.
Halii hii ilitamba siku mbili tu, siku ya tatu matanda yote nyeupe.
Watu wote tulikimbia kurudi kijijini, sasa balaaa lilikua njiani.
Watu wengi walifia njiani, tulio tusua ni wachache sana.
Nakumbuka msafara wetu (wakurudi kijijini) ulikua na watu 8, kati ya hao wawili tuliwaacha njiani, (walifia njiani).
Moja kati ya watu hao ni Rafiki yangu kipenzi (mdogo wangu) Dogo Chiko, na mshikaji alieitwa Wamisunjo (Mateas)
Nakumbuka tulikiamsha kutoka matandani pale mida ya saa4 asbuh, tulitembea umbali mrefu, mdogo wangu Chiko akatuambia tumngoje anaenda kukata gogo (kunya)
Tulimngoja, tulikaa chini mwenye sigara aliwasha, mwenye bange lake alilipua, mwenye maji alikunywa.
Muda ulipita mara Chiko akarudi, na safari kuendelea.
Lakini kila tulipo muangalia usoni, macho yote yame badilika rangi nakua yanjano.
Tukampa maji na safari ikaendelea.
Hatukufika mbali sana, Chiko akaomba tumsubiri anakwenda tena kujisaidia.
Tilipu hii tulimngoja bila dogo kurudi, ikabidi mshikaji mmoja amfuate.
Alipo fika kule alimkuta chiko kesha kufa.
Jamaa akatuita tuje kumcheki, nikiwa mingoni mwao nilimkuta dogo amesha kauka pale alipo kaa.
Kwakua tangu tuna toka matandani tulishaambiana kua ugonjwa huu ni kipindu pindu, hivyo ukifa hakuna mtu alie thubutu kukushika.
Kwahiyo Dogo Chiko tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.
Nitarudi muda si mrefu.
Mkuu mbuguni pale maisha ni laini?!!!Machimbo ya mbali hata yatoe jiwe la thamani sikanyagi,mererani kunanitosha sana maisha lainiii maini yanasubiri
👍Maisha ya utafutaji ni magumu sana
....kasema kipindupindu!!Jamaa yako unumuacha porini badala ya kumzika?
Rip komredi chiko..Rip dogo chiko
Ni uzi gani mkuu?Wajua ye aliweka heading ambayo iko nje ya uwezo wake[emoji28][emoji28][emoji28]
Na kama unavyojua JF wajuaji ni wengi, ndio pale mtifuano ukaanza wa kutunishiana misuli[emoji28][emoji28]
Hata hivyo yale maswali mliyokuwa mnamuuliza yalikuwa magumu, nimesoma nikacheka sanaa
Nilichompendea mhusika ni kuwa hakuwa anachukia wala kukata tamaa, ye aliendelea tu na yale aliyoweza mengine anayakaushia kama hayaoni na kudai amejibu maswali yote na simu yake mbovu haiwezi kuandika ujumbe mrefu
Ule ni moja kati ya uzi ambao ukiwa down na ukaupitia basi lazima mood itabadilika na furaha itarejea
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
😲Mfyuuuu
😲😲 Yaani ni wasukuma tu ndo wanatamka hivyo?!!
😲2015 mkoa/nchi gani hiyo vilitokea vifo vingi ila havikuvuma kwenye mitandao ya kijamii?
👍Baada ya laana kukithiri polini, Mwenye (chifu) akawatangazia wanakijiji wenzie wawakataze vijana wao wasiingie polini.
Kwakua watu tulikua wengi hakuna alie jua kua wenye kijiji wametususia poli.
Laana iliendelea mpaka ulipo lipuka ule ugonjwa.
****************************************************************************************
Baada ya story hiyo kutapakaa karibu kwa kila mchimbaji, mala majadiliano yalianza.
Kwanza tulijiuliza kama ule ugonjwa ni kweli kipindu pindu mbona tulivyo fika kijijini pale na ugonjwa ulikoma?
Kulikua kuna watu walikua wanaeza habari za mzungu kutia sumu kwenye maji tuliyo kua tunatumia kwenye shughuli zetu mbali mbali.
Lakini swali likaja, kama nikweli sumu, mbona wanaokufa ni wanaume tu? ( na nikweli, kwenye kisanga hichi hakuna mwanamke alie kufa)
Tena ukizingatia walikua wanakufa wengi ni wanunua dhahabu, wafanya biashara wengine, na wanaozunguka na vingwendu.
Kumbuka watu hao wote, machimboni hunywa maji ya dukani.
Jibu likaja kua kuna masharti yamevunjwa.
Watu wakatiana moyo wa kwenda tena polini.
Ikapangwa siku, mwenye kutaka kwenda polini aungane twende.
Nikajifikilia, na mimi nikajipa ujasili wa kuungana na kikundi kitacho rudi tena polini.
Kilicho ni shawishi kikubwa niliamini kuna watu wengi walikua wamekufa na dhahabu mfukoni, hivyo niliamini lazima nirudi na dhahabu.
Pili nilikua nashauku ya kujua kama Wamisunjo alifia pale ama alitoboa mpaka kijijini?
Kulipo kucha safari ilianza.
Safari ilikua ya mtu kama 20+ hivi.
Ila kabla ya safari tulikubaliana hakuna mtu kubeba bange, sigara wala pombe.
Safari ilianza rasmi ya kuelekea polini, njiani tunapishana na maiti, upigi hatua kumi bila kukutana na maiti.
Asikuambie mtu binaadam akifa ananuka balaaa.
Yani ilikua ni mwendo wa kushikapua mpaka unataka kutapika.
Tulitembea mpaka pale tulipo muacha Wamisunjo, nikamkuta jamaa wamemjalia nzi tu, yani hata kumkalibia nilishindwa kwa huzuni.
Safari iliendelea mpaka tunafika matandani.
Tulipo fika matandani, maiti zenyewe hizo! Kama kwenye movies vile.
Kila upande zime jazana maiti tu, kuna harufu mbaya, kama huna moyo wa ujasili lazima utapike.
Tulizunguka polini pale lakini tulishindwa kufanya kazi kutokana na hali halisi.
Tukajadiliana kwamba watu kumi wafuate petrol watu wengine tubaki tukizisomba maiti na kuzi weka sehem moja kisha tuzitie moto.
Kwa wingi wa maiti zile na kuharibika vile ilikua ngumu kuzizika, hivyo wazo wa kuzichoma moto lilikua wazo zuri.
Tukatafuta sehem mbali kidogo na matandani, tukalala.
Hapo uliwashwa moto mkubwa, hapo ni story za kupeana moyo tu husu maisha, kila mtu anaongea lake mpaka asubuhi.
Kulipo kucha wale kumi walielekea kijijini kufuata petrol, na sisi wengine tukaanza kuzisogeza maiti sehem moja (zile zilezo kalibiana.
Mfano fungu moja unakuta maiti tano, fungu lingine watatu kutokana na ukaribu walipo fia.
Nakumbuka mimi na brother mmoja (huyu ni mmalawi) tuliingia ndani ya duka moja hivi, tukamkuta mwenye duka kafa kwenye kiti chake kaa tu.
Tulipekua duka lote (japo kunanuka)mara ya kwanza tuliambulia pesa tu, jamaa nilie nae akania huyu maiti alikua ananunua dhahabu pia hivyo tuwe makini katika kusachi kwetu tusije pishana na dhahabu.
Harakati za kumsachi mfukoni, tukamvua viatu, wapi?
Tukamvua nguo zote (kwa tahadhari ya hali ya juu) hapa tukamkuta na donge la dhahabu kwenye kipochi kidogo cha shingoni, ila marehem alikua kakivaa kiunoni.
Uwezi amini huyu marehem alikufa na biashara yake ikiwa imejaa.
Nakumbuka tulibeba Dragon baadhi ya kasha na kwenda kunywa mbele (hapa tuliapa hakuna mtu kugusa pombe )
Siku ilisha tukizikusanya maiti tu na kuzisachi, mwenye bahati ya kukutana na dhahabu ni ya kwake.
Tulipo gundua kua maiti nyingi zimekufa na dhahabu mikoni, kazi ya kuzikusanya haikua ngumu tena, wala kile kinyaa kikapotea.
Tukaanza kuzigombania maiti kila mtu anataka kusachi, mwisho wa siku tukaingiwa na kama wazimu hivi.
Nakumbuka kuna jamaa walizichapa (nusura wauwane ) wakiigombania maiti moja hivi.
Kuna mmoja kati yao anadai anamfaham malehemu, hivyo yeye ndie mwenye haki ya kuchua dhahabu ya marehem......
Narudi muda si mrefu.
🤣🤣🤣 Haataree...Halafu wengine wanawaambia watume na yakutolea kwa sababu Wana samaki
Mnachanganya wadau kwa kupandikiza story tusome kipi tuache kipi ,miluzi ming inampoteza mbwaNaendelea na sakasaka la Pete ya dhahabu na kidani chekundu (kwa maelezo ya Kitoabu ni Ruby) Baada ya kushtuka usiku nilihisi baridi sana likitambaa kwenye mwili, kuangalia chini alipolala baba hayupo. Hofu iliongezeka ndani yangu nikifikiria yule mzee anaweza akaja tena na tuliyokuwa tunamtegemea ni baba kuwepo pale. Nikamuamsha mdogo wangu ili kujipa moyo wa uwepo wa pamoja katika hali niliyoihisi. Nikawa nasikia sauti mtu akilia na kusema "siondoki mpaka mnipe (Kuna neno lilitajwa ambalo sikulijua) vinginevyo nitaendelea kuwafuatilia mpaka wanirudishe kwa (akataja jina jingine la kike, nadhani ni jina la yule mwanamke aliyedondosha Pete). Nikamuuliza dogo unamsikia huyo mtu anayelia? Sauti inatokea wapi? Hakuna aliyekuwa na jibu kwasababu sauti ilikuwa inajaa madikioni mwangu bila kudhihirisha sehemu inayotokea, yaani ni Kama vile nimevaa earphone alafu mtu aongee.
Yule shekhe Kuna maneno alituambia kuwa tukiona Hali ambayo hatuielewi tuyatamke hayo maneno. Nayakumbuka lakini hapa sitayataja. Basi nikaanza kuyatamka yake maneno huku nikitetemeka mdogo wangu akilia kwa kwikwi. Bila kujielewa tulipitiwa na usingizi na kushtuka asubuhi kumeshakucha. Ile Hali haikujirudia kwa muda wa siku tano yaani it was like nothing happened before. Sasa nilikuwa nimesharudi kwenye hali ya kawaida na chuo nilikuwa nikienda na kufurahi na washkaji kama kawaida bila kuwaambia kwanini siku tatu sikuwepo mazingira ya chuo. Ile siku ya sita nilisahau kuoga Ile dawa kuanzia asubuhi mpaka jioni, kilichokuja kutokea usiku wakati natoka seminar room kujisomea haaa.......
🤣🤣Jamani mwenye mawasiliano na huyu jamaa hebu amcheki,maaanake inaonekana anenda kuhara kila baada ya kuandika mistari kadhaa,isije kuwa nae keshafarikia chooni
🤣🤣Wakenya sijui wana akili za namna gani,amesikika mkenya mmoja akiwaomba mods wabadilishe jina Nairoto kuwa Nairobi hapo kwenye kichwa cha uzi wako
Oya Delgado kuna IS kuwa makiniPale nilipo kaa (kuwangoja washkaji) usingizi ulinipitia nililalaa mpaka nilipo amshwa na makelele ya washkaji.
Sijui nilitumia muda gani kwenye usingizi ule ila nilipo angalia saa ilikua ni saa 6 mchana.
Nilipo amka nilikutana na kijua kikali utadhani niko Sudan, yani mpaka nguo nilizo vaa zilishaanza kunyauka.
Chakwanza niliwauliza kuhusu yule mmalawi, nikaambiwa bado wako camp wanaendelea kungoja mvua iishe waanze kazi.
Nilipo wauliza vipi kama mvua imeisha huko walikotoka, wakaniambia mvua imenyamaza sasa hivi baada ya kuvuka lile korongo.
Yani kumbe mvua inaanzia kwenye korongo kwenda matandani, ila kulimaliza korongo mvua hakuna.
Tulitembea mpaka kijijini, hakuna alie jua kua mimi nina dhahabu mbeleni.
Tuliingia kijijini saa 2 usiku, hapo tukalala.
Ila kwakua tulisha fika kijijini, kila mtu aliendelea kimpango wake.
Pale kijijini kila mtu anaham ya kujua kulikoni huko porini.
Nakumbuka nilitulia kwenye kiosk cha jamaa flani hivi, kila mtu alikua ananiuliza kuhusiana na porini.
Usiku kucha nilikesha kwenye kile kiosk cha jamaa nikila Royal gin (hii ni pombe kali sana) mpaka kuna kucha.
Kwakua nilikua na pesa ya kutosha niliyo chukua kwenye lile duka la marehem, hivyo ilikua mwendo wa kujimiminia pombe.
Kuna dem alinitamani nika lale kwake, lakini nilikataa kwa kuhofea asiniibie dhahabu yangu.
Migodini wanawake ndio wanaongoza kutuibia wachimbaji.
Kilicho fanyika nikumpa pombe mpaka dem akakimbia.
Asubuhi, sikutaka kulemba, na pombe zangu kichwani, nikakamata piki piki mpaka Montepuez.
Montepuez, hapa ndio kuna soko la madini yote.
Nikaingia kwa msirilanka nikapima dhahabu.
Dhahabu ilikua na uzito wa gram 112, kila gram kwa kipindi kile ilikua 2000 miticais sawa na laki moja shilingi kwa wakati huo.
Nikachukua 224,000 miticais, hapo akili yote inamuaza mama Abuu (Shemeji yenu)
Nakumbuka nilinunua piki piki na mazaga mengine kama nguo.
Nikatuma kama 60,000 miticais (sawa na Milioni tatu kipindi hicho) kwa mama yangu Tanzania, maisha yakaendelea.
MWISHO.
Naahidi kuwahabarishine matukio mbali mbali yanayo / yatayo tokea hapa mgodini nilipo.
Kumbuka kwa sasa naishi Tete, Muatiz, ila kwa hizi mvua zilizo anza kunyesha, nategemea kurudi Cabo del Gado wilaya ya Montepuez, nikatafute Ruby.
Hapa nangoja hii kazi iishe, nione kama nitaokoa chochote kinisogeze kwenye Ruby.
Ahsanteni na kwaherini.