Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Basi ngoja niishie hapa then nitaianzishia uzi wake
Jimena
Mkuu vipi malizia hapa hapa, mbona kila kitu kinaeleweka, sema labda kama unataka kuanzisha uzi wako tu mwingine ila hata hapa mambo yameenda poa tu. Kama utaamua kuanzisha uzi basi tupe taarifa humu kua umeuanzisha au utaunzisha lini tuje tumalizie hapa ulipoishia.
 
Zamani sana pale jirani na kwa bamkubwa Chamwino kuna kakijiji kanaitwa nzuguni,kuliibuka Chimbo dhahabu inatema mi dogo tu wa 12-14,
nilikua najichanganya sana na maanko wangu alafu walikua watu wa vagi na ubwiii ile mbaya,
sasa walinipenda kwasababu mlinzi wao huko wakipakaza,likianzishwa nzegembe mi nachukua wallet na mali zote zinazohamishika kisha nayeya home.
Machimbo yalipoanza Nzuguni tulienda hawakuniacha bodyguard wao.
Duh kufika kule nilichoka jamaa anachosimulia ni kweli kabisa.
uzinzi,pombe,bangi, kila aina ya uasi unaukuta .ushangae sasa machimbo hata mwezi hayana.
sisi tulikua na kagroup ketu mtu nne wote mayanki tu na tulikua tunachakata vumbi tu lile.
siku kadhaa tukapatapata vimawe viduuchu yani kwenda kuuza tukagawana kahela kadogodogo tu.
Ila mi niliridhika nikasepa nikawaacha maanko maana wao hata ndoto ya kurudi hawana ilikua km wamefika nyumbani,sio hata wachimbaji wao ilikua ni pary pary tu.bangi pombe mabibi na daily wana hela wale jamaa aisee
Ila walikua mafundi malori wazuri sana KAUDO pale na Madereva.
Ule mgodi ulikatika ghafla tu,upo hapo Chamwino pembeni kushoto ukiwa unaenda kwa baba mkubwa.
sawa kabisa mwaha, eneo hilo ni la JWTZ kambi ya Ihumwa, yaani unapopanda ule Mlima wa Nzuguni unachepukia kushoto, ukiacha kulia ni barabara ya kwenda UDOM, maeneo hayo ya kushoto ndipo kwenye dhahabu, kuna jamaa mmoja mpaka leo alilinunua eneo hilo ana kaofisi pale Airport kaofisi ka zamani kwenye puto, hayo machimbo enzi hizo nilienda kibiashara kupeleka soda, mama mzazi akipeleka msosi wa kuuza. Umenikumbusha mbali
 
Story ya jamaa inanikumbusha 2005/2006 Nyakahura katikati ya msitu mzito Sana na 2016 October pale msitu wa council Ushirombo Bukombe...waliowahi kaa machimboni au miji ya machimbo tunamwelewa jamaa...ingawa anaweza kuwa ametunga story yake lakini inaakisi uhalisia wa maisha ya migodini
Nyakahura miaka hii kumejaa watu ,shule ,mnada na miembe hmn Poli by 2015 mpk sasa hii 2020
 
Mbona me show niliimaliza kitambo.
Labda siku nyingine nikifurahi ama nikilikumbuka tukio lolote nitawawekea.
Kweli Mkuu uliimaliza post # 621
Dunia hii mwanamume ni kutafuta na kuhangaika, na mm Kitoabu nina kastori nitakatengeneza nikalete, niliingia machimbo huko Kilosa Kijiji cha Mkadage tukakuta pango eti Mjerumani kaacha mali Dhahabu, alimas magari, mafaili yakeya utawala mpaka na nyuklia, acha tuchimbe km mita 50 chini zaidi na oxygen unahisi kukosa, sina hamu hatukupata mpaka leo, na bado nimeacha wenzangu wanachimba upande mwingine kwani pale walikosea, ni kambi hasa inajulikana huko Kilosa
 
Nilichomoka camp kwa tahadhari, sikutaka mtu ajue tena zaidi yule mmalawi (huyu ni mmalawi sio mrundi )

Mdogo mdogo huku mvua ikinichapa, nilipo hakikisha nime ziacha hatua kadhaa zile camp nikawasha tochi yangu ya kichwani moko yangu begani taratibu nasonga na njia.

Nilitembea mwendo wa masaa kama mawili hivi, mvua ikinyesha, uoga ukaanza kuniingia, japo tuchi yangu ilikua ikiwaka vizuri tu, lakini nilipata tabu kuona mbele.

Kuna muda nilikua natoka nje ya barabara, yani napotea njia, mara nimeingia kwenye mashimo, uoga ukanizidi.

Nimelowa mpaka boxa ya ndani, meno yana tetema mpaka yanauma, hapo natamani atokee mtu na bange lake anitembezee.

Nilizidi kutembea huku nikitetema, mkono nilio shika moko vidole vyote vimekufa ganzi, Kiufupi nilijiihisi naota.

Mbele kidogo kuna korongo limezunguka, kikawaida makorongo haya hupitishaga maji, natangu naiwaza hii safar akili yangu ilikua hapa kwenye korongo, sababu kwa mvua ile ni lazima ningeyakuta maji yame jaa, na hakuna njia nyingine.

Chaajabu nililikaribia korongo nakulikuta korongo kavu, yani kuna vimaji tu vya ugoko, yani hata suruali hukunji.

Hapa nili shangaa sana, maana si rahisi kwa mvua ile, sehem ile isijae maji.

Nilitambuka mpaka ng'ambo ya korongo, hapo nikaendelea na safari.

Kadri nilivyo kua natembea ndivyo sasa mvu ikawa inapungua na hata ka mwanga nikawa nakaona kwa mbaali.

Hapa nikaona ngoja sasa nitwete niwasubiri wale jamaa waolikusudia kurudi kijijini.

Nilipo kaa pale, usingizi ukanipitia (kati ya vitu ambavyo hatuwezi kuviamrisha sisi wenyewe ni usingizi na haja kubwa, binaadam anaweza kulala hata kwenye dimbwi la maji ) nililalaaaaaaaaaaaa

Nitarudi muda si mrefu
Ndugu zangu sifanyi kusudi sema ndio vivyo tusamehane.
Kwa kweli hii si story tu bali ni elimu pia

Sent from my itel A11 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa natumia simu. Itabidi nianzishe uzi wake hili jambo. Mwanzo nilijua nitaweza kuifupisha lakini kadri niendeleavyo nashindwa kuifupisha kama nilivyotaka
tutajuaje km umeuhamisha huu uzi wa pete ya dhahabu ba kidani chekundu
hebu malizia humuhumu itanogo
sasa hali ya mitandao sio mizuri kila kitu wanadhani ni siasa kwa hiyo kugundua wapi kuna uhondo ni shida, labda utatuhamisha kwa link au kutag
Hongera kwa kutuweka sawa

Heisenberg

 
Back
Top Bottom