Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Mkuu umeahidiwa mbunye ikabidi uwe mpole[emoji23][emoji23][emoji23]
Baada ya kubembelezwa saaaana huko DM kwa kutumiwa hadi wadada kuniahidi tunu basi nimebadili mawazo sasa nitasimulia habari ya safari yetu ya kutafuta mali (RUPIA) humo msitu wa NYUMBANITU

(achaneni na utani wa hapo juu) sasa twende taratibu,matukio mengi nitafupisha tu kufanya story kueleweka

Kwa wasiojua...Nyumbanitu iko Njombe wilaya ya wanging’ombe kuna mahala panaitwa Mdandu huko,ni msitu wenye habari za kutisha sana wenyeji wa huko hakuna sehemu wanapaheshimu kama hapo

Huu msitu cha kwanza uko na wanyama wasio wa kawaida kabisa na wanapatikana huko tu,kuna kuku fulani weusi tiii na midomo myekundu,hawa wanaishi humo na hakuna anayewahudumia kwa chakula wala matunzo...pia kuna ng’ombe n.k wote hawa ni kwa ajili ya matambiko ya makabila mbalimbali ya mkoa wa Njombe,zamani ikiwa wilaya ya Iringa,,haswa wabena na wakinga.

Kuna ukoo kule unaitwa wa akina Mkongwa,hawa ndio wamiliki halisi wa huo msitu na inasemekana wao wakifa huwa wanageuka kuwa nyoka na wanaishi huko kwenye huo msitu...kwa waliofika kutalii kuna wazee wako nje huwa wanatoa maelekezo ya namna ya kuingia humo na mila za humo,kama una roho nyepesi unaweza ishia tu kufika mlangoni ukarudi zako ulikotoka...unapigwa mkwara mlangoni na moja kati ya issue unapaswa kujipanga ni kwamba kama mwanamke usiende ukiwa kwenye HEDHI sababu mizimu humo ikisikia tu harufu ya damu wote mlioongozana na huyo mnapotea na hamuwezi onekana hadi wazee wa mila wafanye yao...

achana na hayo...

kilichotutia tamaa sisi kuhusu humo ndani ni story za uwepo wa RUPIA za mjerumani bwanaaa...na hakika zipo na zilikuepo,tulichogundua wale wazungu washenzi sana,hii ya kujenga hofu watu wasiende humo kwa kujiamini ndio imefanikiwa kuziacha mali zao salama mule msituni...wazungu akili nyingi sana,humo wamepandikiza uchawi mkali sana na unalindwa na hao wazee wa mila bila wao kujua wanalinda mali za watu....

ilikua 2001 mwezi wa 12 sasa tukiwa na jamaa zangu tukapanga mkakati wa kuingia mule bila kufata sheria zao za kichawi...maana ukifata protocal kuna maeneo huruhusiwi kufika na ndio inasemekana yana mali

kuna mapango makubwa inasemekana yakitumika wakati wa vita...kwa story tulizopata ni kwamba hizi mali zimefichwa kwenye masanduku makubwa yananing’inia kwenye mapango/mahandaki yaliyoko ndani kabisaaaa wanakosemaga ndio anakaa mzee mwenye msitu,ingawa kikweli huko sababu ya giza na kutisha basi kumekua makazi salama ya nyoka wakubwa wa kila aina na hao kuku wa kichawi ndio chakula chao...

tukiwa tumejipanga,plan ilikua ni kazi ya usiku mmoja tu tunamaliza tunarudi na mali na utajiri wetu...kulikua na habari kwamba soko ya rupia ni uhakika...

nikirudi naanzia sasa kwenye safari yenyewe kuingia msituni nyumbanitu

..........
 
yale mauaji ya watoto mwaka jana yametajirisha wengi sana njombe.

huyu jamaa wa madini msumbiji aseme ukweli kuhusu matumizi ya ushirikina kwenye uchimbaji wa madini msumbiji

mauaji ya watoto
vijana wasiooa
wazee
viungo vya wanawake
viungo vya albino
nywele za saluni
kucha za wale vijana wasafisha kucha
mabaki ya maji ya kuoshea maiti
kufukua makaburi

haya yote ni watu wa madini ndio chanzo na wale wasaka utajiri kishirikina

Kitoabu

Kitoabu

aseme kuhusu haya mambo na sababu sasa tunaweka ukweli tu anaweza pia kusema upande wake anatumia njia gani kiimani hapa maana HAKUNA mchimba madini au msaka RUPIA asiyehusika kwenye cycle ya mauaji au utumiaji wa ushirikina

yangu nitakuja kukiri siku moja
 
yale mauaji ya watoto mwaka jana yametajirisha wengi sana njombe.

huyu jamaa wa madini msumbiji aseme ukweli kuhusu matumizi ya ushirikina kwenye uchimbaji wa madini msumbiji

mauaji ya watoto
vijana wasiooa
wazee
viungo vya wanawake
viungo vya albino
nywele za saluni
kucha za wale vijana wasafisha kucha
mabaki ya maji ya kuoshea maiti
kufukua makaburi

haya yote ni watu wa madini ndio chanzo na wale wasaka utajiri kishirikina

Kitoabu

Kitoabu

aseme kuhusu haya mambo na sababu sasa tunaweka ukweli tu anaweza pia kusema upande wake anatumia njia gani kiimani hapa maana HAKUNA mchimba madini au msaka RUPIA asiyehusika kwenye cycle ya mauaji au utumiaji wa ushirikina

yangu nitakuja kukiri siku moja
Hii ya mwaka Jana Njombe pia imezimisha ndoto za utajiri na kuishi kikawaida was jamaa wengi sana. Kuna jamaa yangu wa Makambako ameishia kukaa rumande hadi leo na alikuwa na maisha safi tu.
 
yale mauaji ya watoto mwaka jana yametajirisha wengi sana njombe.

huyu jamaa wa madini msumbiji aseme ukweli kuhusu matumizi ya ushirikina kwenye uchimbaji wa madini msumbiji

mauaji ya watoto
vijana wasiooa
wazee
viungo vya wanawake
viungo vya albino
nywele za saluni
kucha za wale vijana wasafisha kucha
mabaki ya maji ya kuoshea maiti
kufukua makaburi

haya yote ni watu wa madini ndio chanzo na wale wasaka utajiri kishirikina

Kitoabu

Kitoabu

aseme kuhusu haya mambo na sababu sasa tunaweka ukweli tu anaweza pia kusema upande wake anatumia njia gani kiimani hapa maana HAKUNA mchimba madini au msaka RUPIA asiyehusika kwenye cycle ya mauaji au utumiaji wa ushirikina

yangu nitakuja kukiri siku moja
Aisee kuishi kwingi kuona mengi! kumbe yale mauaji ya watoto kule njombe ilikua ni dili la utajiri!!
 
Part III
nimerudi wadau,tusameheane...nimeandika habari yangu baada ya kusoma story mama ya huu uzi ukanifurahisha na kati ya vitu nimesuffer ni kutafuta mwendelezo kama hivi mnavyosuffer nyie[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

ila all in all nipo hapa...

....kati ya makosa tuliyofanya(haya nilikuja gundua baada ya mchakato kuisha na kupona kabisa,kuanza kuwaza ilikuaje hadi tukafanya tukio lile),lilikua ni kuchukulia lile tukio kama kitu rahisi tu,hatukufanya uchunguzi wa kutosha labda sababu ya ile haraka ya kufanikiwa na habari za kufata mkumbo kwamba kuna watu waliofanikiwa walivyoingia humo ndani,kule Njombe kulikua na tajiri aliyeitwa Mwanzinga(marehemu kafa 2017/18 kama sijakosea) huyu ni moja ya watu wanaodaiwa kutajirika baada ya kufanikiwa kuzama humo na kutoka na mali...story kama hizi ndio zilituchanganya na kujikuta tumebamia mapango ya watu bila kujipanga...pia baadae nilikuja ambiwa kwamba ile mali haisakwi kwa makundi,yaani unatakiwa kuwa man alone,peke yako ukifanikiwa kuzama ukatoka basi umetoboa,kosa letu lilikua kwenda kikundi...tuachane na hayo

sikumbuki masaa exactly lakini siyo chini ya saa sita hivi tukawa ndio huko pango kubwa...kutembea kwenda mbele ndio ilikua mtihani sababu nje mvua ilikua inanyesha na hilo pango ndio iliku njia ya maji yanaingia halafu yanapotelea huko ndani ndani yanatokea upande wa pili wa msitu kwenye miteremko kuunda mikondo ya maji

maji yalikua mengi na yanaenda kwa kasi sana so tulikua tunatembea kwa kujishikilia pembeni kwa tahadhari sana,giza ni kubwa bila zile tochi hufanyi kitu chochote kule...ukiongea sauti kidogo tu inakua multiplied sababu ya mwangwi,lile pango linaenda linashuka chini...ni kama shimoni,umbali wa kama viwanja viwili vya mpira ndio mauzauza yakipoanza

sisi kwetu kule huwa wanasema ukisikia hofu sana ghafla kwa kitu ambacho ulianza fanya kwa ujasiri basi acha mara moja...mimi hofu ikaanza kuniingia,lbda sababu sikua na moto sana kuhusu hizi rupia kuliko wenzangu(ikumbukwe nilikua na kibarua) nilikuaga naambiwa kuhusu nywele kusimama sikuwahi experience kabla,,,mara nikahisi mapigo ya moyo yako kazi sana hofu ni kubwa na nywele zinawasha sana ndio nywele kusimama huko...kutetemeka sababu ya baridi kukazidi ,sikumwambia mtu yeyote..kwa kadri ya ramani ya mangi alisema tumefika hayo maeneo yenye masanduku,kwa maelezo yake tulitakiwa fika kwenye korongo liko ndani ya pango...kwamba kwenye korongo juu kumeunganishwa minyororo mirefuuuuu imefungwa juu kabisa imeshuka chini huko ndio imeungwa kiustadi kwenye mashanduku imara kabisa,kwa uhandisi ule hayawezi anguka leo wala kesho...ni kweli binafsi niliona sasa sijui huwa ni wenge au nini,sababu humo ni kuchafu na kuna mizizi sana huwezi confirm kuwa ni kweli ni minyororo au ni mizizi,jamaa pia alituambia kuhusu beacon,ni kweli tuliona beacon zikiwa na maelezo ya lugha hatuifahamu kwa maelezo ya mangi hizo ni code wameandikiana wao siku wakija wanazitumia kufata mali....na zile zimeandikwa katika namna ukizitumia bila kujua ndio zinakupoteza zaidi (wazungu washenzi sana)...yaani unaweza kuta mshale umeenda kusini mita 2 kumbe wanamaanisha aendee kusini ya nchi,unakuta ni songea huko au vyovyote na mali haipo hapo unapodhani wewe,ni anayeweza chukua zile mali ni lazima awe na taarifa za kutosha sanaaaa...sababu hata wao huwa wanakuja na wanarudi patupu sometimes wakikosea maelezo.

nimeongea kuhusu mangi(huyu bwana kumbe yeye alikua keshawahi kuja fanya jaribio ila hakuweza mwenyewe ndio maana akaamua kutafuta kampani)

sasa ndio akatuambia tukiwa hapo kwamba...huko chini kushuka lazima watu washushwe kwa kamba(tulibeba kwa urefu wanaotosha sana,kama marufu kule njombe zinaitwa TANTAN) nani anashuka ikawa sasa wajitolee wawili akiwemo mangi mbeba maono...alikua pamoja na usungilo,mobu na mwaikambo wawashikilie kamba na mimi nikawa tu pending nimewashikia vitu pamoja na kucheki cheki usalama tu...wakajifunga kikomando tayari kushuka,kushuka kwenyewe hujui unashuka wapi...unafata tu mizizi maana huwezi jua kama ni ndio mnyororo au nini kisa msongamano wa taka.

jamaa wakaanza kushuka chini...kimya kikatawala pale sababu ya hofu tu.

dakika kama tano za kushuka kwa tahadhari ndio ikatokea shida,kikweli huwa sijui ni nini hasa kilitikea sababu mimi ni ghafla sana nikaona mwanga mkali mno,mkali saaaana kama radi kutoka kule shimoni ni kama zikanipoteza fahamu kwa muda,mwanga uliambatana na sauti za kilio kule chini as if mtu kakamatwa ghafla na mnyama mkali,nadhani alikua usungilo sababu baadaye mangi alifanikiwa kutoka(nitasema baadae tulikutana vipi)

nilichoweza kufanya haraka kwa muda ule ilikua ni kulala chini haraka sana,kule chini sauti jamaa ilikua inazidi kupungua ikimaanisha keshazidiwa nguvu...sikujua chochote kuhusu wenzangu washika kamba pale juu sababu kila mtu nadhani alianza kujitetea kivyake..

nikaanza kukimbia nikiwa na ule upofu wa kupigwa na mwanga mkali ghafla ukiwa gizani....kimbia bila mwelekeo,nikajigonga vibaya kichwani kwenye sehemu ya juu ya pango,na kilichoniokoa ni kwamba nilikua naelekea mbele zaidi ambako ni jirani kutoka nje kuliko kule tulikotoka...wenzangu hapo sijui wameelekea wapi...ile kujigonga ikanimaliza nguvu kabisa nikajikuta nimelala hapo hapo damu zinanitoka(ile fact ya damu nadhani ndio inaaply hapa) ghafla mbele yangu,ule upande niliowaacha jamaa sasa nikaona bonge ya nyoka ila siyo wa kumeza,mkubwa kwa hawa nyoka tumewazoea ila siyo chatu..kujivutavuta nadhani nikamkanyaga ndio akanigonga,akili hapa ndio zikaja baada ya kujua kifo ndio kimefika,chap nikatoa kiatu nikafungua kamba za viatu vyote viwili,nikafunga juu ya goti na chini ya goti sababu alinigonga kwenye hii nyama ya nyuma ya mguu...nikajikamua kamua kizushi nikawa napambana sasa kuelekea nje ,ambacho sikujua(labda ni mungu tu) kwamba kumbe tulikua nje kabisa hata ya msitu ambako sasa ni karibu na barabara kabisa watu ambako watu wanapita..tena karibia na kijijini...cha mwisho nakumbuka niliweza fanya ni kupiga kelele ya mwito kule njombe inaitwa ngoro....nikapiga za vilio kama mara tano hivi pumzi ikakata sikuelewa kilichofata baada ya hapo aiseee...hadi siku nazinduka nikiwa hospitali ya kibena....mguu ukiwa na hali mbaya sana umeharibika lakini pia ngozi yangu karibia mwili mzima ikiwa na upele fulani wa kuwasha sana...

nikaanza matibabu huku nikiwa sijui nimefikaje,sijui kuhusu jamaa zangu na hapo nimetulia sijauliza mtu yoyote sababu hakuna hata aliyeniuliza kulikoni

nitarudi sasa na habari ya matibabu yang na kuujua ukweli kuhusu vifo vya jamaa zangu na yule mwengine aliyegeuka mwehu...kisha mtazamo wangu kuhusu hizi mali za wachawi wazungu...

mnisamehe kwa mpangilio mbovu,naandika haraka sana niendane na muda kupambania kombe watoto wapate chochote kitu...


nitakuja....
 
Yaani ninavyosimulia hapa, picha kamili inanijia kichwani kwasababu nakumbuka Kila kitu mpaka sura yake ingawa ilikuwa usiku. Mkuu acha kabisa kuonana na viumbe hivi

Ddduuuh mtihani, wakati mwengine ukihadithiwa mikasa kama hii unaona kama story tu, lkn kwa yaliyompata ndio anajua effect yake. Phobia, naona mpk dhahabu huna hamu nayo.....
 
@kitoabu
yale mauaji ya watoto mwaka jana yametajirisha wengi sana njombe.

huyu jamaa wa madini msumbiji aseme ukweli kuhusu matumizi ya ushirikina kwenye uchimbaji wa madini msumbiji

mauaji ya watoto
vijana wasiooa
wazee
viungo vya wanawake
viungo vya albino
nywele za saluni
kucha za wale vijana wasafisha kucha
mabaki ya maji ya kuoshea maiti
kufukua makaburi

haya yote ni watu wa madini ndio chanzo na wale wasaka utajiri kishirikina

Kitoabu

Kitoabu

aseme kuhusu haya mambo na sababu sasa tunaweka ukweli tu anaweza pia kusema upande wake anatumia njia gani kiimani hapa maana HAKUNA mchimba madini au msaka RUPIA asiyehusika kwenye cycle ya mauaji au utumiaji wa ushirikina

yangu nitakuja kukiri siku moja
 
Ddduuuh mtihani, wakati mwengine ukihadithiwa mikasa kama hii unaona kama story tu, lkn kwa yaliyompata ndio anajua effect yake. Phobia, naona mpk dhahabu huna hamu nayo.....
Acha kabisa, nikiona hata pete ya English gold kumbukumbu za hili tukio zinanijaa. Kuna muda mpaka nilikuwa nateseka bila kumwambia mtu yeyote lakini imefikia kipindi nilikubaliana na hali mpaka sasa zimekuwa kumbukumbu za kawaida
 
matajiri wengi wa njombe story zao za kutisha sana,Njombe ndio uchawi wa utajiri ulikolala...nashangaaga wanaosema kuna sehemu ni wachawi kuliko Njombe.

kule mauaji ya kichawi yameshamiri sana na wachawi wako wazi wazi,tena uchawi wa kule ni wa misukule
Uchawi na Ukimwi ni vitu vya kawaida sana

Kijana anajulikana kabisa huyu kaua mama yake au kafanya msukule mdogo wake halafu fresh tu ingawa yapo sehemu nyingi lakini kule ni kawaida yaani haishtui kama watu wa maeneo mengine wanashtuka kusikia habari za tajiri fulani

Ukimwi kawaida tu watu hawashtuki juu ya ngoma, yaani kawaida kabisa

Mkuu stori yako imenisisimua sana ikiisha nikaribishe inbox

Nimeishi mkoa ule miaka kumi lakini nasikia tu kwa watu haya unayoandika
 
yale mauaji ya watoto mwaka jana yametajirisha wengi sana njombe.

huyu jamaa wa madini msumbiji aseme ukweli kuhusu matumizi ya ushirikina kwenye uchimbaji wa madini msumbiji

mauaji ya watoto
vijana wasiooa
wazee
viungo vya wanawake
viungo vya albino
nywele za saluni
kucha za wale vijana wasafisha kucha
mabaki ya maji ya kuoshea maiti
kufukua makaburi

haya yote ni watu wa madini ndio chanzo na wale wasaka utajiri kishirikina

Kitoabu

Kitoabu

aseme kuhusu haya mambo na sababu sasa tunaweka ukweli tu anaweza pia kusema upande wake anatumia njia gani kiimani hapa maana HAKUNA mchimba madini au msaka RUPIA asiyehusika kwenye cycle ya mauaji au utumiaji wa ushirikina

yangu nitakuja kukiri siku moja
Sisi wenye upara vipi mkuu
 
Back
Top Bottom