Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Serikali haiwajibiki kulipia familia zisizoweza kulipia nauli za kurudishia maiti za ndugu zao Tanzania.

Ikifanya hivyo, bajeti za kuendesha balozi zote zitaishia kusafirisha miili ya watu kurudi Tanzania.

Kuna sehemu nyingine nauli hii ni zaidi ya $20,000.

Kwani nyie familia yenu yote mlishindwa kuchangishana kupata kiasi kilichohitajika?
Mzee mtu aliyekufa siyo kiloba cha mchele ni kweli bei ni $10,000-$20,000 inategemea ni wapi?
 
Kwanza pole sana kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Mungu ampe kauri thabiti huko aendako ambako ni kwetu sote but jamani hebu tuweni realistic hapa; hivi kwa uwezo wa nchi yetu inawezekana kweli kusafirisha kila anaekufa huko nje kweli? Nchi gani duniani huaga inasafirisha raia wake waliofia nje ya nchi, hasa kama raia huyo kafia huko nje ya nchini mwake but alikwenda kwa shughuli zake binafsi? Kuna nchi ya namna hiyo hapa duniani kweli? I dont think so. Umesema kuna wanafunzi waliwahi kukwama kwenye nchi X na wabara hawakusaidiwa but wa visiwani, SMZ iliwasaidia, huoni (kama ni kweli ) Wazanzibar mko vizuri zaidi kuliko sisi wabara? Again, not sure, hao wanafunzi huko nje ya nchi, walipelekwa na serikali huko au wazazi/walezi wao? Tusijaribu kutengeneza sheria ambazo sisi wenyewe hatuna uwezo wa kuzitekeleza. Hilo la Zanzibar kua na ubalozi nchi zingine, ni wazo zuri but itabidi kwanza ijulikane kimataifa kwamba Zanzibar is a sovernity state na ikifanyika hivyo, nikwambie tu ukweli, nyie hamna uwezo wa ku finance balozi zenu nje ya nchi kwasasa, uchumi wenu bado unaitegemea sana BARA. Angalia tena bajeti yenu, chief financer ni nani?
 
Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Labda mngemuomba balozi atoe pesa mfukoni mwake.
 
Duuh ,sehem gan iyo naur inazd na bei ya kununua na kuisafilisha vanguard
Marekani karibu kila mwezi naona michango ya rambirambi watu wanachangishana kurudisha maiti nyumbani.

Ku process maiti funeral home tu kabla ya gharama za ndege ni kati ya $1,000 na $3,000. Hapo hujaingia gharama za kusafirisha mwili ambazo almost always ni zaidi ya $10,000. Hapo ndipo umepata the lowest deal.Ukija ku add kila kitu tunaongelea around $20,000 hapo.

Wabongo nao kila siku wanaambiwa wanunue life insurance wabishi.

Marekani ukiwa unaishi unaweza kununua life insurance ya mpaka $500,000 kwa kiasi kidogo tu. Ukifa familia yako inalipwa wanakuwa hawana sababu ya kuhangaika.

Yani kama watu kutoa rambirambi inakuwa kiutamaduni tu, si kwa sababu familia inahitaji nauli ya kurudisha mwili na imewapa watu target ya kuifikia.

Tujiandae kwa haya mambo, tuache kutegemea serikali na michango ya rambirambi.
 
Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Watanzania wangapi wanafariki nje ya nchi?

Na kila mtu akitaka ubalozi umsafirishie ndugu yake, ubalozi utaweza?

Kumbuka balozi zimepigika tayari, na tunaona watu wanachangishana kila mwezi kusafirisha maiti za ndugu jamaa na marafiki.

Acha kujiona wewe special sana kama wewe tu ndiye utahitaji huo msaada.

Kuna familia nyingi sana zitahitaji huo msaada na serikali haina bajeti ya kuweza kusaidia hili.

Changishaneni kama familia, ubalozi unaweza kuwasaidia mawasiliano na kuwa na mtu wa kufuatilia mambo huko. Lakini hela mnatakiwa kutoa nyie kama familia.
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.
Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege ' Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Inasikitisha sana mkuu..

Lakini pia ungejiuliza kwann serikali ya SMZ iliwasaidia wanafunzi wa kizanzibar kwa pesa za kujikimu na kuwaacha wale wa bara bila msaada?

Wht comes around goes around mkuu..

Nadhani umeshapata majibu ya muungano wetu.

Hata SMZ kumbe pia wanabaguwa wa bara.

Pole kwa msiba.
 
Nimeangalia Whatsapp group moja hapa kuna mtoto anahitaji 16,000 kupata matibabu India.

Huyo naye ndugu zake waidai serikali?

Kuna Mtanzania kafariki April 8 kwa seizure, huyo naye familia yake isaidiwe na serikali?

Kuna mtu mwingine kafariki watu wamechanga $9,000 kuwezesha mwili kurudishwa nyumbani. Kaja Marekani mwaka mmoja tu uliopita.

Hawa watu ni wengi sana.

Balozo zikilipia nauli za kurudisha miili wote hawa zitajiendesha vipi?
 
Hiyo ya travel documents ni issue nyingine balozi inawajibika.

Lakini kwenye kusafirisha miili balozi haiwajibiki. Familia iwajibike.

Kuna siku nilienda ubalozi wa Marekani, wakati haujapigwa bomu bado.Kunq vitu vilitumwa kimakosa ubalozi wa Nairobi nilikuwa naangalia kama wanaweza kuvi forward Dar.

Mbele pale kwenye mlango waliweka bango kubwa kwa raia wa Marekani wanaomaliza hela za matumizi na kwenda ubalozini kuomba hela.

Bango hilo lilisema wazi kwamba ubalozini si sehemu ya kwenda kuomba hela watu walioishiwa na hela nje ya nchi.

Inaonekana walikuwa wanapata Wamarekani wa aina hiyo wengi sana Tanzania mpaka ikawabidi waweke bango hilo mbele kabisa, kama Mmarekani ana shida hiyo asijisumbue hata kuendelea kuingia ndani.

Si kwamba ubalozi ulishindwa kuwa na akaunti ya kusaidia watu wanaomaliza hela wakiwa nje.

Ni suala la personal responsibility.

Watu wanatakiwa kubeba mizigo yao wenyewe, sio kuitwika serikali mizigo hiyo.

Kuna watu wanasafiri kwenda nje wananunua mpaka yravelers insurancd ku cover contingency planning wakiumwa au wakifa nchi za nje.

Tuqche hizi tqbia za kutaka swrikali itatue kila tatizo.

Tanzania ni nchinyenye watu wengi sana, wote hawa wakiitegemea swrikali hatutafanya kitu chochote cha kueleweka tutaishia serikali kulisha watu tu mpaka inafilisika.

Tusipende kulalamikia serikali hata kwenye kumzika ndugu.
Miaka ya nyuma sana alifariki mtoto wa general wa jeshi hapa SA ubalozi ulitoa hela na vitu vyote baada ya kujua ni mtoto wa Mkuu na mambo mengi walisimamia wao...
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.
Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege ' Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Ni uzembe wa viongozi wa nchi kwani tatizo hilo lingetakiwa kuchukuliwa na serikali na kusafirisha maiti huyo ni raia wa nchi kama amepata tatizo la kutojitakia, nchi inatakiwa kuhakikisha inalishughulikia, Hili sio Tatizo la muungano ni Tatizo la watu wote hivyo tuitake serikali kutengeneza sheria na ziwekwe wazi na namna watu wanaweza kufuatilia watu wanapopata matatizo nje ya nchi
 
Mwaka jana Nchiya Oman Illeta Ndege Kuchukua raia wake wote waliokwama kwa sababu ya Corona na kuwarudisha Oman Free of charge.
Hii ndio kujali kwa nchi na raia wake.
(PAKA ) alituma CHOPPER ya jeshi kuchukua raia wake majeruhi wa na maiti t AMBASSODOR CHOIR OF CHRIST Ya Rwanda.

Watatu kati yao wakafa.Manzi Philbert, Amos Phares, Gatare Jimmy Ephaim ,mjini Kahama walipopata ajali mbaya ya ya gari coaster.

Mtwara yalitokea mafuriko yaloleta madhara, ila uongozi wa juu ulipuuza wakati wa "MWENDAZAKE "🤣🤣🤣

Akauliza 😶😶😶 "NILILETA TETEMEKO LA ARDHI.."🤣🤣🤣

Bongo hamna issue kuhusu raia wanapopata majanga.

Watu walikula RAMBIRAMBI na Michango ya TETEMEKO LA ARDHI.🤨🤨😃😃
 
Nimeangalia Whatsapp group moja hapa kuna mtoto anahitaji 16,000 kupata matibabu India.

Huyo naye ndugu zake waidai serikali?

Kuna Mtanzania kafariki April 8 kwa seizure, huyo naye familia yake isaidiwe na serikali?

Kuna mtu mwingine kafariki watu wamechanga $9,000 kuwezesha mwili kurudishwa nyumbani. Kaja Marekani mwaka mmoja tu uliopita.

Hawa watu ni wengi sana.

Balozo zikilipia nauli za kurudisha miili wote hawa zitajiendesha vipi?
Ni vitu ambavyo vinawezekana sema kwa Nchi zetu ikiwepo hela ya dharula wahusika hawataweza kupata kutokana na ubinafsi uliokuwepo...
 
Mwaka jana Nchiya Oman Illeta Ndege Kuchukua raia wake wote waliokwama kwa sababu ya Corona na kuwarudisha Oman Free of charge.
Hii ndio kujali kwa nchi na raia wake.

Shida sio sababu ni mzanzibar. Tunaweza kuwalaumu ubalozi kwa kosa ambalo wala sio lao. Je balozi zetu wana bajeti ya dharura kama hizo? Oman ni nchi tajiri. Inaweza kufanya hivyo. Sisi bado tunaenda mdogo mdogo. Tumeshasogea sana mpaka tunaanza kununua meli na kufanya maendeleo kwa hela za sikukuu ya Muungano. Ni hatua ya kusifiwa. Ipo siku inshallah, maendeleo yetu yatatufanya wenye uwezo wa kufanya mambo kama wenzetu.
Hata kama tukivunja muungano sasa, tusijidanganye kama ipo njia ya mkato ya kutupa maendeleo. Pia tusisahau kidole kimoja hakivunji chawa...na majuto mjukuu

Udumu udugu wetu katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Pole kwa matatizo, lakini sio jukumu la serikali kusafirisha maiti za Watanzania kuja kuzika hapa nchini. Ikitokea ni msaada, ukikosa usilalamike. Consular services sana sana ni kukusaidia kuhusu utaratibu etc, ila kurudisha maiti ni la kwenu.
 
Ni vitu ambavyo vinawezekana sema kwa Nchi zetu ikiwepo hela ya dharula wahusika hawataweza kupata kutokana na ubinafsi uliokuwepo...
Vinawezekana vipi bila kuwa na hela? Hizi ni dalili ya kuwa na DNA ya kufanya mazingaombwe
 
Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Sijui unalalamika kitu gani ilhali hata SMZ nayo hapo kwenye suala la wanafunzi imeonyesha ubaguzi, kwanini SMZ ilishindwa kuwasaidia masurufu hao wanafunzi kutoka bara??.

Juu ya yote hutakiwi kuanza kulaumu ubalozi kutokana na hiyo kadhia iliyokufika kabla hujajua kwamba ni kweli wanayo au hawana FUNDS kwa ajili kadhia hiyo.

Pole sana kwa yaliyokukuta.
 
Mzee mtu aliyekufa siyo kiloba cha mchele ni kweli bei ni $10,000-$20,000 inategemea ni wapi?
USA tunawachangia watu kila mwezi nauli ndizo hizo.

Kabla hata ya kufika kwenye kulipa nauli uwe na $1,000 mpaka $3,000 ya funeral home.
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.
Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege ' Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Umefiwa na una uchungu lakini isikufanye uanze kukamata wenye makosa. Nijuavyo mimi hiyo ilikuwa ni taratibu za shirika la ndege liliomshusha njiani. Shirika la ndege lina dhamana ya kumsafirisha abiria hadi mwisho wa safari yake. Njiani chakula na kila kitu ni juu yao. Yawezekana mauti ukatokana na huduma yao mbovu; Chakula, maji, hewa, nk. Ndo maana ukiwa mgonjwa lazima shirika litaarifiwe ili waweze kuona kama unastahili kusafirishwa kwa ndege yao. Hata mjamzito lazima athibitishe uwezo wake wa kusafiri.

Usianze kusukumia mambo ya Zanzibar na Bara, itakuwa ndo kudeka huko! Kuamini Zanzibar inakupenda sana kuliko Tanzania. Maoni kama hayo ndo yanawazuia watu wa bara kupata ajira ndani ya SMZ lakini wanzanzibari wako huru kuajiliwa kokote bara! Mfano wako wa wanafunzi ni feki tu, kwani aliyewapeleka ni nani? Huyo ndo ana dhamana ya kuwahudumia. Na kwa mfano huo pia huo ni ubaguzi, Kwa nini SMZ ilihudumia watokao Z'bar ikawaacha watokao Bara? Kama BAra hawana pesa kwa nini SMZ haikuwapa support?
 
Back
Top Bottom