Kifo ni kitu ambacho kila mtu anajua atafariki, sasa kinakuwaje dharula?
Kila mtu aliye nje akifa tukisema ni dharula serikali ilmsaidie, itaweza kusaidia?
Ikisaidia wengine na kuacha wengine, hapo si ndiyo mwanzo wa malalamiko ya kwamba watu fulani wanapendelewa?
Hakuna logic ya serikali kulipia nauli ya maiti kutoka nje, hili ni jambo lenye gharama kubwa sana na mara nyingine watu ambao si wasafiri hawajui kwamba nauli ya maiti ina gharama mara nyingi sana kuzidi nauli ya mtu hai.
Watu wajiwekee akiba, wakate bima, wachangishane rambirambi, wasaidiane, serikali labda itasaidia ku coordinate mambo na kufuatilia lakini kuipa serikali mzigo wa gharama hizi ni jambo lisilowezekana kwa bajeti hafifu za balozi zetu hizi.