Kuniita mimi mjinga haimaanishi kwamba wewe sio mjinga mara elfu moja zaidi.,
sasa ahadi ya marehemu imemtokea kwenye ndege tena fly dubai na kwa ihsani ya flay dubai wakatua Ethiopia kwa dharura kwa vile ni karibu na Tanzania sasa huoni kwamba ubalozi wenu umeacha jukumu lake kusaidia palipo bakia ili mwili wa mtanzania huyu ufike nyumban salama?
Imagine kama ni ndugu yako amepatwa na hili na uko kwenu chato unapata call unafkiri ungeweza kukodi bombadia kwenda Ethiopia kubeba mwili wa ndugu yako? Ndio mana mtoa mada ametaja ubalozi na hizi ni miongoni mwa majukumu ya balozi zilizo nje duniani nzima., wewe hujui chochote.
Sasa Bima unamlaumu NANI? wakati Rais wenu amesema hizo bima zenu ni bure ata ukienda hospitali dawa hamna, unafkiri bima yenu hiyo itoe ndege ikamchukue ndugu yako aliye Ethiopea badala yake?
Kwanza kabisa hapa sijakuita mjinga nimekwambia acha ujinga.
Pili unapojadiliana na mimi kuwa specific, unapoandika kuhusu ubalozi kuwa na jukumu lake la kusaidia unamaanisha nini?
Kwani wapi mimi nimekataa kwamba ubalozi una jukumu la kusaidia?
Unajua kusoma kwa ufahamu?
Mbona mara nyingi tu kwenye uzi huu nimeandika kwamba ubalozi una jukumu la kusaidia ku coordinate mambo.Kwanza mwili hauwezi kuhakikiwa kwamba ni wa Mtanzania bila ubalozi kuhusishwa, sasa hapo ubalozi utakosaje jukumu la kusaidia?
Unaelewa ninachopinga mimi ni ubalozi kubeba gharama za kusafirisha mwili, si ubalozi kusaidia.Ubalozi una jukumu kubwa sana la ku coordinate mwili usafirishwe, hili jukumu kama ubalozi umelitelekeza, haujalikamilisha, kwangu mimi ubalozi una lawama.
Lakini kama kuna hela za kulipa kusafirisha mwili, hilo ni jukumu la familia, si la ubalozi.Watanzania wanafariki wengi sana nje na ubalozi hauna bajeti za kutosha kuwasafirisha, hili ni jukumu la familia.
Mimi kwetu kaka mkubwa naangaliwa kwa mategemeo.Sisi ndugu zetu wakipata matatizo tunafanya vikao vya familia kumaliza matatizo.Hatutegemei serikali kwenye matatizo ya kifamilia, hilo ni jambo la aibu.
Sio kama najitapa, najielezea ukweli wangu, kwa sababu umeniuliza angekuwa ndugu yangu kafariki nje hivyo ningefanyaje. Bahati nzuri nina mfano hai wa leo leo kuhusiana na matatizo ya kifamilia ninavyoyatatua.
Hivi hapa naandika nimepigiwa simu asubuhi hii kuna ndugu yetu kapata matatizo Zanzibar kwenu huko natuma US $900 kumaliza matatizo haya. Kitu nilichofanya ni kupata muhuri wa wazee wa kuaminika wa familia kwamba hili tatizo ni legit na familia ingependa ndugu asaidiwe, baada ya kuhakiki hilo nimeuliza namba ya M-Pesa kutuma muamala. Sijailalamikia serikali kwa matatizo ya familia yetu.Na nimekuwa nikifanya hivyo miaka yote. Ndiyo maana nashangaa watu wanaolalamikia serikali matatizo ya familia yao.
Na huyo ndugu yangu hajafa, na hiyo si mara yangu ya kwanza kumsaidia.Alishawahi kunikopa hela akashindwa kunirudishia, na mimi nilimpa bila kutegemea atarudisha, na sasa namsaidia tena kama ndugu tu. Sijaomba serikali itusaidie kwenye matatizo yetu ya familia, najua serikali ina mambo mengi sana.
Bima kuna mpaka za kimataifa wewe unaongelea rais wenu bado unarudi kulekule kulaumu serikali kwa ujinga na umasikini wako.