Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Suala si ukoefu wa Fund , bali Nchi yetu ina Policy mbaya kwa raia wake.
Iliwahikutokea miakaya nyuma Pale Thailand , Wageni walikamatwa kutoka nchimbali mbali wakiwa hawana documents za kusafiria.
Serikali ya Thailand ikazishauri Balozi za nchi husika ziwapatie Raia wao Traveling Documents na wao watawaruhusu waishi na kufanya kazi bila kuwarudisha..
Mataifa yote yaliwapa raia wao Passport na kuwaacha wafanye kazi Thailand ,lakini TZ waliwarudisha Nyumbani bila huruma.
Balozi kule alikuwa Mapuri kama sikosei
November 14, 2006Omar Ramadhan Mapuri
roho mbaya tu bila shaka atakuwa ashalala kwenye udongo
 
Mwaka 1996 au 1997 Kuna kijana alifariki Ulaya kwa Ukimwi . Baba yake alikuwa ni mmoja wa wafanyakazi wa Ikulu. Maiti ilirejeshwa bongo kwa msaada wa Ubalozi. Kila kitu ubalozi uligharamia.
Siwezi kushuhudia hili, nashuhudia matukio binafsi, mwingine tumemzika March, kafia U.S. wana diaspora walichanga na sisi tukajichanga wakarudisha mwili tukamzika.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Unapopanga hizo bajeti hujui kwamba kuna matukio kama hayo hutokea?

Dhima kuu ya serikali ni kusaidia jamii,it may sound higher opportunity cost in terms of money but when you weigh the returns in terms of prerving the reputation of the country inakuwa bora ku help hao raia wako maana uko kwa ofisi kwa ajili yao.
Kwani serikali ina hela za kigeni zisizo na mwisho?

Nimekuuliza vizuri kwa kukupa limited budget, kama ilivyo kiuhalisi serikalini.

Wewe unajibu kama huelewi concepts za limited resources na opportunity cost.

Kuna mtu kasema balozi zetu zina struggle kulipa bill za umeme.

Hizi ndizo balozi tunazozinyenga zilipe nauli za kurudisha maiti Tanzania?
 
Wengi hamjamuelewa,tujadili hoja yake sio kumshambulia yeye binafsi,ndugu yake alishushwa kwa kuwa alikua anaumwa.
Asingekua mgonjwa asingeshushwa Ethiopia,tuanzie hapo,
Aliposhushwa ndo umauti ukamfika.
Kwa maana hiyo shirika la ndege,ilibidi warudishe chenji ,kibongo bongo,wakate nauli Hadi Ethiopia tu,
Hapo tuendelee Sasa.
Tatizo yeye kaja na hoja za kijinga za kuanza kushambulia Tanganyika na kutaka apewe privilege ubalozini kabla hata ya kuchunguza kama shirika la ndege liko obligated kusaidia abiria wake.

Typical lazy mind approach ya "Serikali nisaidieni kusafirisha maiti kwa kuwa ndugu yetu raia", wakati serikali haina bajeti kwa hiki kitu. Na kafanya hivyo kabla hata ya kuangalia options zake huko kwenye shirika la ndege.

Wangeomba ubalozi uwasaidie ku coordinate na shirika la ndege huko Ethiopia ningeelewa, hiyo ni sehemu ya kazi za ubalozi.

Lakini mtoa maada anataka serikali iingie gharama za kurudisha mwili Tanzania.

Tena kwa some ignorant shit about Muungano na Tanganyika.

Typical ignorant overentitled country bumpkin Zanzibari.
 
Ndugu yangu tupoe sana na tumshukuru Allah S.W.T angalau kwa hao fly dubai kwa kutusogezea ndugu yetu maiti yetu na Battawi mwenzetu kwa hapo Ethiopia, japo imechukua muda kumzika ndugu yetu lakini hatimae tumeweza kumzika ardhi ya nyumbani, muhimu sasa tumtakie dua Allah amfanyie wepesi safari yake, Allah amjalie makazi mema na amjalie malipo yake yawe ni pepo na sisi tumuombe Allah atupe subira na msiba huu na husnul khatima njema.

Kuhusu hila za ubalozini ni kwamba nchi yetu huko bado haijawa nchi yenye kutenda haki, ingawa haya malalamiko kwa hapa jf hayatasaidia sana kama ni kwa ajili ya kuona hatujatendewa haki na kutoa madai nashauri tumuandikie rais moja kwa moja kuhusu hili naamini mama yetu Samia atajali sana.

Tupoeni sana nimeona clip ya huyu dada akiwa kwenye ndege akipunga mkono ya kuaga kwa heri kumbe ndio anaaga kwa kundoka hapa Ulimwenguni. Allah amsamehe madhambi yake na sisi sote. Amin.
Acheni ujinga wa kulaumu ubalozi.

Mmejipanga wenyewe mkamzika ndugu yenu.

Siku nyingine jifunzeni kununua bima na kuwa na mifuko ya dharula ya familia msije kurudia ujinga wa kutaka kuzikiwa ndugu zenu na ubalozi.

Zaidi, acha ubaguzi kwa Watanzania wenzako kwa sababu wametoka bara.

Tatizo lako ni umasikini, ujinga na kujiona una privilege kuliko ilivyo kiuhalisia.

Huo ubaguzi wako ni ubaguzi unaotokana na ujinga tu.
 
Upo sahihi eti Mtanzania anapoteza passport kupata travelling document ili arudi nyumbani anaambiwa alipie vikaratasi tuu hawa watu kama Kiranga ndio watoa maamuzi wetu na wapo wengi mno huko...
Mkuu Kiranga unamlaumu kwa kipi?

Kwa umasikini wa nchi yako inaposhindwa kurudisha maiti za watu?

Kwa ujinga nanutegemezi wa Watanzania wanaotaka serikali iwachambe mpaka mavi wakinya?

Mimi siwezi kukulaumu.

Nchinyenyewe ina ugonjwa wa akiki wa "schizophrenia".

Inaongozwa kwa "Ujamaa na Kujitegemea" wakati "Ujamaa" ni kitu kinachopingana na "Kujitegemea".

Matokeo yake kwenye kulipa kodi watu hawana mchango, kwa sababu GDP per capita ndogo, halafu kwenye kudai huduma kila mtu anadai huduma kama analipa kodi kama Bakhressa.

Acheni ujinga wa kutegemea serikali.

Serikali yenyewe ina bajeti ndogo na kazi nyingi za kufanya.
 
Serikali haiwajibiki kulipia familia zisizoweza kulipia nauli za kurudishia maiti za ndugu zao Tanzania.

Ikifanya hivyo, bajeti za kuendesha balozi zote zitaishia kusafirisha miili ya watu kurudi Tanzania.

Kuna sehemu nyingine nauli hii ni zaidi ya $20,000.

Kwani nyie familia yenu yote mlishindwa kuchangishana kupata kiasi kilichohitajika?
Mkuu unamaanisha kitu fulani unachokifahamu Mkuu...kuwa wazi fungu lipo au Bajeti ya Balozi za Tanzania ni ya madafu?!Maana hata Dr.Slaa bado mkavu mkavu vile au majukumu au anajibana Sana?!!!.$20,000,kitu gani?!
 
Suala si ukoefu wa Fund , bali Nchi yetu ina Policy mbaya kwa raia wake.
Iliwahikutokea miakaya nyuma Pale Thailand , Wageni walikamatwa kutoka nchimbali mbali wakiwa hawana documents za kusafiria.
Serikali ya Thailand ikazishauri Balozi za nchi husika ziwapatie Raia wao Traveling Documents na wao watawaruhusu waishi na kufanya kazi bila kuwarudisha..
Mataifa yote yaliwapa raia wao Passport na kuwaacha wafanye kazi Thailand ,lakini TZ waliwarudisha Nyumbani bila huruma.
Balozi kule alikuwa Mapuri kama sikosei
November 14, 2006Omar Ramadhan Mapuri
Balozi zetu si za kutegemea labda ukute hapo ubalozini kuna "mtu". Ikiwa kupata hati ya kusafiria ni mbinde wataraji nini ukiwa ughaibuni?
 
Naomba kueleweshwa..Kinachopelekea gharama za kusafirisha maiti kuwa kubwa hivyo ni nn??..Naomba mchanganuo kama unafahamu..
Sehemu nyingi zina mchakato tofauti kabisa unaopitia funeral homes, hospitali kuhakiki mwili hauna magonjwa, vyombo vya sheria kuhakiki hakuna foul play, ubalozini kuhakiki makaratasi na uraia, by the time maiti inasafirishwa inakuwa process ndefu sana si kama mzigo wa kawaida.

Unaweza kusoma zaidi baadhi ya processes zinazopitiwa hususan kwa nchi kama USA.

Of course kila nchi ina utofauti wake lakini mara nyingi vitu vya msingi huwa vinakuwa sawa.

Mkuu unamaanisha kitu fulani unachokifahamu Mkuu...kuwa wazi fungu lipo au Bajeti ya Balozi za Tanzania ni ya madafu?!Maana hata Dr.Slaa bado mkavu mkavu vile au majukumu au anajibana Sana?!!!.$20,000,kitu gani?!
$20,000 zingejuwa si hela nyingi familia ya marehemu ingechanga bila matatizo.

Unajua kuna Watanzania wangapi wanafariki nje kila mwaka?
 
Lakini mtoa maada anataka serikali iingie gharama za kurudisha mwili Tanzania.

Tena kwa some ignorant shit about Muungano na Tanganyika.

Typical ignorant overentitled country bumpkin Zanzibari.
Wewe unachukia kitu ambacho kimsingi ni maslahi kwa raia yeyote wa Tanzania awapo nje ya nchi yake na akapatawa na dharura asiyoitarajia.
Au wewe ni sehemu ya wafaidika wa mfumo uliopo?

Kusema Zanzibar ni ''Typical ignorant overentitled country bumpkin Zanzibari'' hii ni chuki na tuu binafsi kwa mshirika wa Muungani wa hiari.
Kama unaona Zanzibar haistahiki kupewa privilage si mukaungane na Congo au kenya nchi munayolingana ki Poulation na ukubwa wa ardhi?

MIMI NAKUSUDIA KAMA RAIA NINAYO HAKI YA KUHUDUMIWA IPASAVYO NJE YA NCHI NIKIPATA DHARURA .
Huyu marehemu hakuwa na mtuyeyote wa kumsaidia nchini ethiopia,isipokuwa Serikali ya Ethiopia kuiarifu Balozi kuhusu tukio hili na ,ndio hapo utakapona umuhimu wa kuwepo Balozi na msada kwa raia wake ikiwemo coordination and cost of handling the dead person of this kind of incidence.

Hii ndiyo Huruma ya Taifa kwa raia wake na kutimiza wajibu wa kibalzi.
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.

Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege 'Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line.

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Serikali ya CCM ni kinyesi cha mbwa Koko,haina faida yoyote kwa Watanzania,mbwa hawa....
 
Acheni ujinga wa kulaumu ubalozi.

Mmejipanga wenyewe mkamzika ndugu yenu.

Siku nyingine jifunzeni kununua bima na kuwa na mifuko ya dharula ya familia msije kurudia ujinga wa kutaka kuzikiwa ndugu zenu na ubalozi.

Zaidi, acha ubaguzi kwa Watanzania wenzako kwa sababu wametoka bara.

Tatizo lako ni umasikini, ujinga na kujiona una privilege kuliko ilivyo kiuhalisia.

Huo ubaguzi wako ni ubaguzi unaotokana na ujinga tu.
Kuniita mimi mjinga haimaanishi kwamba wewe sio mjinga mara elfu moja zaidi.,

sasa ahadi ya marehemu imemtokea kwenye ndege tena fly dubai na kwa ihsani ya flay dubai wakatua Ethiopia kwa dharura kwa vile ni karibu na Tanzania sasa huoni kwamba ubalozi wenu umeacha jukumu lake kusaidia palipo bakia ili mwili wa mtanzania huyu ufike nyumban salama?

Imagine kama ni ndugu yako amepatwa na hili na uko kwenu chato unapata call unafkiri ungeweza kukodi bombadia kwenda Ethiopia kubeba mwili wa ndugu yako? Ndio mana mtoa mada ametaja ubalozi na hizi ni miongoni mwa majukumu ya balozi zilizo nje duniani nzima., wewe hujui chochote.

Sasa Bima unamlaumu NANI? wakati Rais wenu amesema hizo bima zenu ni bure ata ukienda hospitali dawa hamna, unafkiri bima yenu hiyo itoe ndege ikamchukue ndugu yako aliye Ethiopea badala yake?
 
Wewe unachukia kitu ambacho kimsingi ni maslahi kwa raia yeyote wa Tanzania awapo nje ya nchi yake na akapatawa na dharura asiyoitarajia.
Au wewe ni sehemu ya wafaidika wa mfumo uliopo?

Kusema Zanzibar ni ''Typical ignorant overentitled country bumpkin Zanzibari'' hii ni chuki na tuu binafsi kwa mshirika wa Muungani wa hiari.
Kama unaona Zanzibar haistahiki kupewa privilage si mukaungane na Congo au kenya nchi munayolingana ki Poulation na ukubwa wa ardhi?

MIMI NAKUSUDIA KAMA RAIA NINAYO HAKI YA KUHUDUMIWA IPASAVYO NJE YA NCHI NIKIPATA DHARURA .
Huyu marehemu hakuwa na mtuyeyote wa kumsaidia nchini ethiopia,isipokuwa Serikali ya Ethiopia kuiarifu Balozi kuhusu tukio hili na ,ndio hapo utakapona umuhimu wa kuwepo Balozi na msada kwa raia wake ikiwemo coordination and cost of handling the dead person of this kind of incidence.

Hii ndiyo Huruma ya Taifa kwa raia wake na kutimiza wajibu wa kibalzi.
Nakwambia hivi, raia wanatakiwa kuisimamia serikali itatue matatizo makubwa kama.

1. Kuweka mazingira mazuri ya uchumi watu wawe na ajira na biashara nzuri. Wakisafiri waweze kukata bima za dharula. Familia ziwe na akiba za kutumia katika dharula.

2. Kuweka mazingira mazuri ya elimu watu wawe na muamko wa kujua mambo mengi, si kutegemea serikali kila kitu kama watoto.

Kwa haya masuala mawili nailaumu serikali, haijaweza kuyatimiza.

Ndiyo maaana raia hawana uchumi wa kuchangishana kifamilia kurudisha mwili wa marehemu ndugu yao nyumbani, halafu wanalaumu serikali kwa ujinga wa kushindwa kuchangia mambo.

Serikali si baba yako.

Serikali si mfadhili wako.

Serikali inaendeshwa kwa bajeti yenye mambo mengi na haiwezi kukutatulia matatizo yako ya kifedha.

Nimeishi ughaibuni Marekani miaka zaidi ya 20. Ningekuwa mtu wa kupenda dezo ningekuunga mkono na kulalamikia serikali.Hata siku moja sijawahi kufikiria ubalozi utanisaidia kwenye jambo la gharama yoyote.

Nakwenda kwa maneno ya John Fitzgerald Kennedy.

"Ask not what your country can do for you. Ask what can you can do for your country".

Nunueni bima, kuweni na mifuko ya dharula ya kifamilia.

Acheni ujinga wa kutaka serikali iwalipie gharama zenu kila pahala.
 
Suala si ukoefu wa Fund , bali Nchi yetu ina Policy mbaya kwa raia wake.
Iliwahikutokea miakaya nyuma Pale Thailand , Wageni walikamatwa kutoka nchimbali mbali wakiwa hawana documents za kusafiria.
Serikali ya Thailand ikazishauri Balozi za nchi husika ziwapatie Raia wao Traveling Documents na wao watawaruhusu waishi na kufanya kazi bila kuwarudisha..
Mataifa yote yaliwapa raia wao Passport na kuwaacha wafanye kazi Thailand ,lakini TZ waliwarudisha Nyumbani bila huruma.
Balozi kule alikuwa Mapuri kama sikosei
November 14, 2006Omar Ramadhan Mapuri
Na ukifika home unapokelewa na police uende segerea😄
 
Kuniita mimi mjinga haimaanishi kwamba wewe sio mjinga mara elfu moja zaidi.,

sasa ahadi ya marehemu imemtokea kwenye ndege tena fly dubai na kwa ihsani ya flay dubai wakatua Ethiopia kwa dharura kwa vile ni karibu na Tanzania sasa huoni kwamba ubalozi wenu umeacha jukumu lake kusaidia palipo bakia ili mwili wa mtanzania huyu ufike nyumban salama?

Imagine kama ni ndugu yako amepatwa na hili na uko kwenu chato unapata call unafkiri ungeweza kukodi bombadia kwenda Ethiopia kubeba mwili wa ndugu yako? Ndio mana mtoa mada ametaja ubalozi na hizi ni miongoni mwa majukumu ya balozi zilizo nje duniani nzima., wewe hujui chochote.

Sasa Bima unamlaumu NANI? wakati Rais wenu amesema hizo bima zenu ni bure ata ukienda hospitali dawa hamna, unafkiri bima yenu hiyo itoe ndege ikamchukue ndugu yako aliye Ethiopea badala yake?
Kwanza kabisa hapa sijakuita mjinga nimekwambia acha ujinga.

Pili unapojadiliana na mimi kuwa specific, unapoandika kuhusu ubalozi kuwa na jukumu lake la kusaidia unamaanisha nini?

Kwani wapi mimi nimekataa kwamba ubalozi una jukumu la kusaidia?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Mbona mara nyingi tu kwenye uzi huu nimeandika kwamba ubalozi una jukumu la kusaidia ku coordinate mambo.Kwanza mwili hauwezi kuhakikiwa kwamba ni wa Mtanzania bila ubalozi kuhusishwa, sasa hapo ubalozi utakosaje jukumu la kusaidia?

Unaelewa ninachopinga mimi ni ubalozi kubeba gharama za kusafirisha mwili, si ubalozi kusaidia.Ubalozi una jukumu kubwa sana la ku coordinate mwili usafirishwe, hili jukumu kama ubalozi umelitelekeza, haujalikamilisha, kwangu mimi ubalozi una lawama.

Lakini kama kuna hela za kulipa kusafirisha mwili, hilo ni jukumu la familia, si la ubalozi.Watanzania wanafariki wengi sana nje na ubalozi hauna bajeti za kutosha kuwasafirisha, hili ni jukumu la familia.

Mimi kwetu kaka mkubwa naangaliwa kwa mategemeo.Sisi ndugu zetu wakipata matatizo tunafanya vikao vya familia kumaliza matatizo.Hatutegemei serikali kwenye matatizo ya kifamilia, hilo ni jambo la aibu.

Sio kama najitapa, najielezea ukweli wangu, kwa sababu umeniuliza angekuwa ndugu yangu kafariki nje hivyo ningefanyaje. Bahati nzuri nina mfano hai wa leo leo kuhusiana na matatizo ya kifamilia ninavyoyatatua.

Hivi hapa naandika nimepigiwa simu asubuhi hii kuna ndugu yetu kapata matatizo Zanzibar kwenu huko natuma US $900 kumaliza matatizo haya. Kitu nilichofanya ni kupata muhuri wa wazee wa kuaminika wa familia kwamba hili tatizo ni legit na familia ingependa ndugu asaidiwe, baada ya kuhakiki hilo nimeuliza namba ya M-Pesa kutuma muamala. Sijailalamikia serikali kwa matatizo ya familia yetu.Na nimekuwa nikifanya hivyo miaka yote. Ndiyo maana nashangaa watu wanaolalamikia serikali matatizo ya familia yao.

Na huyo ndugu yangu hajafa, na hiyo si mara yangu ya kwanza kumsaidia.Alishawahi kunikopa hela akashindwa kunirudishia, na mimi nilimpa bila kutegemea atarudisha, na sasa namsaidia tena kama ndugu tu. Sijaomba serikali itusaidie kwenye matatizo yetu ya familia, najua serikali ina mambo mengi sana.

Bima kuna mpaka za kimataifa wewe unaongelea rais wenu bado unarudi kulekule kulaumu serikali kwa ujinga na umasikini wako.
 
Kwanza pole sana kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Mungu ampe kauri thabiti huko aendako ambako ni kwetu sote but jamani hebu tuweni realistic hapa; hivi kwa uwezo wa nchi yetu inawezekana kweli kusafirisha kila anaekufa huko nje kweli? Nchi gani duniani huaga inasafirisha raia wake waliofia nje ya nchi, hasa kama raia huyo kafia huko nje ya nchini mwake but alikwenda kwa shughuli zake binafsi? Kuna nchi ya namna hiyo hapa duniani kweli? I dont think so. Umesema kuna wanafunzi waliwahi kukwama kwenye nchi X na wabara hawakusaidiwa but wa visiwani, SMZ iliwasaidia, huoni (kama ni kweli ) Wazanzibar mko vizuri zaidi kuliko sisi wabara? Again, not sure, hao wanafunzi huko nje ya nchi, walipelekwa na serikali huko au wazazi/walezi wao? Tusijaribu kutengeneza sheria ambazo sisi wenyewe hatuna uwezo wa kuzitekeleza. Hilo la Zanzibar kua na ubalozi nchi zingine, ni wazo zuri but itabidi kwanza ijulikane kimataifa kwamba Zanzibar is a sovernity state na ikifanyika hivyo, nikwambie tu ukweli, nyie hamna uwezo wa ku finance balozi zenu nje ya nchi kwasasa, uchumi wenu bado unaitegemea sana BARA. Angalia tena bajeti yenu, chief financer ni nani?

Tatizo kubwa linakuja hapa kwa mujibu wa uoni wangu, Serekali ya SMZ inajaribu sana kusaidia raia wake pale wanapopatwa na matatizo nje ya nchi, Kitu ambacho serekali ya SMT mara nyingi hua haifanyi juhudi zozote za kujaribu kusaidia, na mara nyingi huishia kuwashutumu hao wananchi. Mifano ipo mingi sana.
 
Sasa mnazidisha upuuzi.
Hao wanaofanya kazi ubalozini wanafanya kwa kujitolea au nao wanalipwa mshahara? Kama wanalipwa mishahara, unaona shida gani wao kwenda kufanya shopping Dubai? Wivu wa kijinga kabisa.

Amandla...

Nione wivu wa kazi gani? Mimi nisingaliandika ila huyo Dada ninamfahamu vizuri .

Ndio watoto wa Vigogo wa CCM
 
Kwa mapato gani ya Znz kuendesha balozi zake yenyewe? Hizo balozi zitakosa hata huduma ya simu.

MKuu jaribu kuwa serious, Hivi ikiwa Comoro wanaweza Zanzibar watashindwaje?
 
Back
Top Bottom