Tukio la ndugu wa Familia kufariki kwa moshi wa jenereta, ndugu adai marehemu walipigwa kabla ya vifo vyao

Tukio la ndugu wa Familia kufariki kwa moshi wa jenereta, ndugu adai marehemu walipigwa kabla ya vifo vyao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Kufuatia tukio la watu wanne wa familia moja kupoteza maisha katika mazingira ya utata, ikidaiwa kuwa ni kwa sababu ya kuvuta moshi wa jenereta, mapya yameibuka.

Mmoja kati ya ndugu wa familia hiyo iliyokuwa ikiishi Temeke jijini Dar es Salaam, amedai kuwa tukio hilo limetekelezwa na watu kwa sababu majeruhi wamekutwa na alama za kupigwa kwenye miili yao.

Maelezo hayo, yanapishana na maelezo yaliyotolewa na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo na kuzusha utata mkubwa.

Chanzo: Global TV Online

Pia soma > Dar: Watu wanne wa familia moja wafariki baada ya kuvuta hewa chafu ya jenereta
 
Hata brief tu Mkuu imekuwa tabu.

Basi tuseme uzi bila maandishi ni uchochezi
 
Mwandishi naye,ameshindwa kuuliza/kutaka kujuwa hao marehemu walikuwa wanajishugulisha na nini?

Ova
 
Back
Top Bottom