Kufuatia tukio la watu wanne wa familia moja kupoteza maisha katika mazingira ya utata, ikidaiwa kuwa ni kwa sababu ya kuvuta moshi wa jenereta, mapya yameibuka.
Mmoja kati ya ndugu wa familia hiyo iliyokuwa ikiishi Temeke jijini Dar es Salaam, amedai kuwa tukio hilo limetekelezwa na watu kwa sababu majeruhi wamekutwa na alama za kupigwa kwenye miili yao.
Maelezo hayo, yanapishana na maelezo yaliyotolewa na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo na kuzusha utata mkubwa.