Tukio la Rais Kikwete, Dr. Shein kukabidhiwa Rasimu ya pili na tume ya Katiba - Karimjee Hall

Tukio la Rais Kikwete, Dr. Shein kukabidhiwa Rasimu ya pili na tume ya Katiba - Karimjee Hall

Huvisa naye anasinzia live on stage, hivi huwa hawajaiandai? Si angelala mapema jana?
 
Warioba anaonyesha kujiamini sanaaa nadhani anajua lengo lake la kuinyonga ccm linaenda kutimia...ccm ndo basi tena inaenda kukata roho...

Kadiri Mzee Warioba anavyoendelea kutoa maelezo, lile smile la Kikwete linapungua.
 
Safi sana,Speaker na Naibu Speaker,wasitokane na Wabunnge wala Vyama vya Kisiasa.
 
Madaraka ya rais yamepunguzwa hasa katika uteuzi, wapiga kura wawe na uwezo wa kumwajibisha mbunge, mawaziri wasiwe wabunge, spika na naibu wake wasiwe wabunge pia.
Namuona Jk kanuna hapa.
 
kuwa najeshi moja,polisi moja na idara ya usalama wa taifa moja.
 
Kuendelea kwa serikali 2, kulihitaji ukarabati mkubwa, upi huo?
 
Madaraka ya rais hasa yale ya uteuzi yamepunguzwa,kutakuwa na vyombo vya kupendekeza uteuzi wao na hatimae kuthibitishwa na bunge.pia spika na naibu wake wasitokane na chama chochote cha siasa.pia tume ya uchaguzi itakua ni taasisi inayojitegemea.yapo mengi,kifupi rasimu hii ikipitishwa tunaweza kuja kuwa na TANZANIA tunayoitaka.Hongera jaji Warioba.
 
Back
Top Bottom