Tukio la Rais Kikwete, Dr. Shein kukabidhiwa Rasimu ya pili na tume ya Katiba - Karimjee Hall

Tukio la Rais Kikwete, Dr. Shein kukabidhiwa Rasimu ya pili na tume ya Katiba - Karimjee Hall

image.jpg
 
Mbona sijaona hii rasmu ikitoa mchanganuo juu ya namna ya mgawanyo wa raslimali za taifa na muungano, kama vle gas, madini, mafuta, nk.
 
Saaaaaaaaaaafi, Warioba kasema mzigo utasambazwa kwa baadhi ya wananchi, viongozi wa siasa nk. Nadhani leo leo mzigo utakuwemo humu JF.
 
Naona mtangazaji naye anashangaa uwepo wa zzk!!!kweli usaliti mbaya aiseeee!!!!
 
Bado tuna safari ndefu kuelekea Tanzania yenye amani
 
pumba kelele mabezo na vitimbi viiingi vya ccm leo leo vimefika mwisho baada ya jaji walioba kupigilia msumari juu ya serikali tatu kuwa ndiyo suruhisho na mwarobain ya mungano
 
Naona Zitto kaishika Rasimu na Anatabasamu,Bila shaka kipengele cha Umri wa Raisi miaka 35 Kimepita.
 
Mkuu, usishangilie sana. Hii ni sawa na kupewa mahindi mabichi utafune wakati hauna meno. Serikali tatu, uraia mmoja, rais mmoja, jeshi moja, polisi moja na usalama wa taifa mmoja. Umeona changamoto iliyo mbeleni?

Changamoto gani wewe!!!... Usichanganye masuala ya utawala na mamlaka ya nchi!! Afrika kusini wana Serikali tisa na mabunge tisa ya majimbo na wanaunganishwa na Serikali moja ya Shirikisho... Hata hapa Tanzania tuna Serikali mbili lakini ukiangalia kuna Serikali za Mitaa na Mabaraza ya Madiwani, wanapitisha Sheria ndogondogo na kutoza kodi!!.. Kilichofanyika ni kuipunguzia Serikali ya Muungano mambo ambayo si ya Muungano that's why kuna umuhimu wa Tanganyika iwepo isimamie mambo yake ya maji, umeme, barabara, afya na miundombinu... Kuna haja gani Wabunge wa Zanzibar waje kujadili Bajeti ya Wizara ya Maji, ujenzi, Afya na nyingine zisizokuwa za Muungano... Nasema iko poa...
 
Back
Top Bottom