Tukipika kuku nyumbani, mimi nalishwa vipapatio, vitoto vyangu vya umri wa miaka 5 na 8 ndio vinalishwa mapaja. Je, hii ni sahihi wakuu?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Wakuu Bwana Yesu asifiwe!

Ebana kuna issue inanitatiza halafu nimeshindwa kuizungumza kwa mhusika ambae ni wife nikaona nitafute kwanza mawazo humu.

Issue nzima iko hivi, ninavyojua kwa mila na ustaarabu wa kiafrika endapo itatokea familia ikachinja kuku basi baba ndiye mwenye kustahili kula mapaja ya kuku.

Sasa hapa kwangu sielewi wife ananichukuliaje, yaani kila kuku akichinjwa basi mimi father house ntalishwa vipapatio na vitoto vyangu viwili vya kiume vyenyewe ndio vinawekewa mapaja. Hii kitu wakuu inanishangaza kidogo as iko kinyume na mila na desturi za kiafrica.

Wife yeye kwao walikua ni mambo safi hivyo nadhani hawakua watu wa kujali vitu hivyo vidogo vidogo ndio maana anaona ni sawa tu mimi Baba kula vipapatio.

Wakuu, nitumie mbinu gani kumfikishia ujumbe kuwa siridhishwi na kulishwa vipapatio?
 
Huyo mkeo hajafundwa hata kidogo, hebu ongea na mkeo bana
 
Watoto wanayahitaji hayo mapaja ya kuku kuliko wewe, si wanakua?

Wewe si utakula tu huko mtaani...

Wala hata sio jambo la uanaume wala nini, ni utu tu

Si umeona mkeo japokuwa hajakutengea kawapa watoto na sio kula yeye? Unadhani kawaza nini?

Legeza bwana😅
 
Ajengewe mnara wife wako 🤣🤣kuku ni kuku tu
 
😂😂😂😂😂😂😂 nimependa sana hii..
We jamaa unaonesha upo happy with your family aiseee ...

Napenda interaction kama hiyo an hakuna ubabe aiseeee sio kama wengine tulivyolelewa kuwa mzee ndo anakula vinono...

😂😂😂😂😂😂 Hapo mkuu cha kukushauri endelea hvo hvo hiyo haina shida kabisa an
 
Nunua kuku wengi mkuu wapikwe wote watoto watakula mapaja mpaka wabakishe na ww utapakuliwa
 
Huenda unamtreat vibaya
 
Huyo mkeo kaamua kuharibu mila na desturi za ki africa?, iv anachotutafuta ni kitu gan?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…