Tukisema Rushwa imetembea Dodoma Jiji FC hamtaki Kuamini

Tukisema Rushwa imetembea Dodoma Jiji FC hamtaki Kuamini

Kufungwa goal kizembe sio kigezo cha kupokea rushwa maana hata ligi kubwa duniani tunaona yanatokea tofauti ya kule na sisi kule hawaamini mtu kuuza ila wanaamini mtu kukosea sisi huku haya mambo ya kununua game yapo sana tu kwa team zote kubwa sio ya leo wala jana miaka na miaka.

Sasa ikitokea tu mtu kucheza vibaya tunaamini kapokea pesa sababu ndio hulka zetu na hakuna wakulikana hili ni team zote kubwa. Sasa kwa jana kama kipa alifanya kosa tu ndio uwezo wake basi fair enough inatokea lakini kama yanayosemwa ni kweli basi ni aibu na hawana nia nzuri kukuza mpira nchi hii hawana tofauti na wahujumu uchumi.

Huwezi kuwa unatumia pesa kununua wachezaji, makocha na mishahara mikubwa halafu mwisho wa siku unanunua mechi, kama hili limefanyika kwa ushahidi ni wakati wa FA kulichukulia serious ikibainika bila shaka ni kweli ni kushusha team na kufungia mchezaji maisha iwe Yanga iwe Simba au Azam na wengine hata wadogo wananunuana pia.

Mimi sifuatilii sana siku hizi sababu najuwa haya yanafanyika japo sina ushahidi lakini jambo lisemwa sana kuna ukweli na tunaona sifa hakuna wakulikemea hili tunauwa mpira wetu. Tushindane uwanjani..
 
Basi ibaki kwamba Yanga walishinda wanahonga na Simba wakishinda ni uwezo wao. Nashauri Kila timu ishinde mechi zake.
 
Back
Top Bottom