Tukitoa tofauti za kimaumbile tofauti kati ya Mwanamke na Mwanaume haipo

Tukitoa tofauti za kimaumbile tofauti kati ya Mwanamke na Mwanaume haipo

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Najaribu kuwaza juu ya tofauti zaidi ya maumbile "body parts" kati ya Mwanamke na Mwanaume siioni.

Na kikubwa zaidi ni kwamba tofauti hizi za kimaumbile ni chache sana kuliko maumbile yanayoonesha kuwa Mwanamke na Mwanamume wote ni binadamu na ni kitu kimoja.

Tuendelee.
 
Kafanye tena utafiti.

Kuna section ya ubongo ambayo upande m'moja ni wa logic wa pili ni wa hisia.... Wanawake wamewekewa upande mkubwa wa hisia ila wa logic ni mdogo, mwanaume kapewa upande wa logic mkubwa wa hisia mdogo.

Ndio maana mwanamke kwenye msiba analia mwanaume anaendelea na taratibu za mazishi, kwenye kuanza familia mwanamke anawaza kutiwa mimba apate mtoto na kuanza kulea familia mwanaume atawaza kwa logic kuwa familia itakula nini na wataishije baada ya mtoto kuja na vipi muda wa shule ukifika kwa watoto, kodi, pesa ya matumizi.

Vingi sana tunatofautiana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majibu ninayoyaona ni sawa na kusimama kwenye upande mmoja wa ukingo wa mto na kuamini upande mwingine haupo sahihi.

Tuweke pendeleo zetu kando tujiulize je kati ya yanayotufanya kuwa kitu kimoja na yanayotutifautisha, mengi ni yapi?.

Je, yanatikana na asili au zao la jamii?
 
Samcezar,
Je, hiyo ndiyo tofauti ya kututambulisha bila shaka kuwa fulani ni mwanaume na mwingine ni Mwanamke?

Mkuu tafakari vizuri hujanielewa huenda umewahi kutoa jibu lako. Haujawahi kusikia watu wakisema fulani ni jike dume au dumejike unafikiri ni kwa sababu uliyoitoa tu?

Nature of creation is so gendered ...tuendelee
 
Je hiyo ndiyo tofauti ya kututambulisha bila shaka kuwa fulani ni mwanaume na mwingine ni Mwanamke?..Mkuu tafakari vizuri hujanielewa huenda umewahi kutoa jibu lako.
Haujawahi kusikia watu wakisema fulani ni jike dume au dumejike unafikiri ni kwa sababu uliyoitoa tu?...
Nature of creation is so gendered ...tuendelee
Mkuu jamaa kaeleza vizuri kabisa,.. cha kuongezea ni kwamba kuna tofauti kati ya binadamu na mtu,,. kwa upande wa mtu (Nafsi) sote tupo sawa lakini kwa binadamu tunatofautiana ki mtazamo na maumbile pia,.. kwani Mme anafanya mambo kwa mantiki(logic), Mke anaongozwa na Hisia(intution).
 
Najaribu kuwaza juu ya tofauti zaidi ya maumbile "body parts" kati ya Mwanamke na Mwanaume siioni.

Na kikubwa zaidi ni kwamba tofauti hizi za kimaumbile ni chache sana kuliko maumbile yanayoonesha kuwa Mwanamke na Mwanamume wote ni binadamu na ni kitu kimoja.

Tuendelee.
Nani kasema si binadamu sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jamaa kaeleza vizuri kabisa,.. cha kuongezea ni kwamba kuna tofauti kati ya binadamu na mtu,,. kwa upande wa mtu (Nafsi) sote tupo sawa lakini kwa binadamu tunatofautiana ki mtazamo na maumbile pia,.. kwani Mme anafanya mambo kwa mantiki(logic), Mke anaongozwa na Hisia(intution).
Unaweza ukathibitisha kama tofauti za kimaumbile (feminine and masculine) zinavyoonesha?..
Make it plain Brethren
 
Samcezar,
... kile kitabu ambacho hakijabakiza kitu kinazungumzia haya mambo?
 
Najaribu kuwaza juu ya tofauti zaidi ya maumbile "body parts" kati ya Mwanamke na Mwanaume siioni.

Na kikubwa zaidi ni kwamba tofauti hizi za kimaumbile ni chache sana kuliko maumbile yanayoonesha kuwa Mwanamke na Mwanamume wote ni binadamu na ni kitu kimoja.

Tuendelee.
Umesema kweli Mkuu. Ndivyo ilivyo.
 
Najaribu kuwaza juu ya tofauti zaidi ya maumbile "body parts" kati ya Mwanamke na Mwanaume siioni.

Na kikubwa zaidi ni kwamba tofauti hizi za kimaumbile ni chache sana kuliko maumbile yanayoonesha kuwa Mwanamke na Mwanamume wote ni binadamu na ni kitu kimoja.

Tuendelee.
Wewe unaonekana ni mende, kunamtu unampigia hesabu mtaani kwako kiasi amekuchanganya.
Ushindwe na ulegee.
 
Wewe unaonekana ni mende, kunamtu unampigia hesabu mtaani kwako kiasi amekuchanganya.
Ushindwe na ulegee.
Hiyo no mental picture yako ila nipo nilivyo na sivyo unavyodhani. Kuwa mpole jenga hoja Jamii forum siyo kipewe cha kahawa Mkuu.
 
Vipi kuhusu tofauti za kihomoni na kihisia, ndo maana hawawekwi pamoja kwenye ulingo wa ngumi au riadha
 
Hilo suala kinaweza kutokea kwa binadamu yoyote.
Haujawahi kusikia "Jike dume au dume jike"..?Mkuu.
I think vinavyotuunganisha ni vingi kuliko vinavyotutofautisha.
 
Back
Top Bottom