Yaani umeshaachwa tayari alama ( points ) tano na Simba SC badala ya Wewe Kusikitika kama si Kuumia Watu wazima na Akili zao kabisa hasa Mashabiki wa Yanga wanashangilia Mshambuliaji wao Molinga leo Kufunga Magoli Mawili yaliyopelekea Wao kupata Alama ( Point ) moja tu ambayo sasa imewafanya Wawe Timu ya Pili yenye Hatari ya Kushuka Daraja muda wowote kuanzia sasa.
Nawaonea mno Huruma Yanga SC. Na kwa kuwasaidieni tu wana Yanga SC kuwa kwa Hasira tulizonazo Simba SC msije mkategemea kuwa eti kuna Mechi hata Moja Simba SC tutapoteza kwani kwa sasa hakuna cha Kupoteza na tunataka ' Kuzoa ' Makombe yote muhimu kuanzia la VPL na lile la ASFC ili mwakani tukashiriki wenyewe tu kwani mwaka jana tumewabeba ' Mapopoma ' fulani hivi na hapa Juzi wametoka kututia Aibu tu huko Ndola nchini Zambia.
Mechi ya leo dhidi ya Polisi FC tumeicheza na tayari kuna ' Team ' ya Kamati ya Roho Mbaya ilikuwepo leo Uhuru na nyingine ipo Kazini kuicheza Mechi ya Yanga SC na Coastal Union Jumapili nia na madhumuni katika Mechi Tatu ( 3 ) Yanga SC ' ahabribu ' ili tumuache kwa Alama ( Points ) ama Tano au Saba tu Jambo ambalo tayari linaanza Kufanikiwa.
Kila Mtu acheze Mechi zake tafadhali.