Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika [TLS] Boniface Mwabukusi ambae alikuwa mstari wa mbele pamoja na makamanda wa CHADEMA katika kuhubiri NRNE tayari amewageuka wenzake na sasa anahamasisha watu waende kwenye uchaguzi.
Yaani kiufupi iko hivi, Mwabukusi akiwa na CHADEMA anasema No Rifomu No Eleksheni, akiwa na wanasheria wenzake wa TLS anawaambia waende wakagombee ubunge kwa kupitia CCM ili waende bungeni.
Hii ikufunue akili mwananchi, uache kuwa mtaji wa kisiasa wa wanaojiita wanasimamia msimamo wa No Rifomu No Eleksheni, kimsingi hakuna msimamo kama huo ndani ya chama cha CHADEMA na viongozi wanasimamia msimamo huo sababu ndio propozo waliopeleka wa wazungu wakapewa hela.
Propozo hiyo ndiyo inawafanya daily unasikia viongozi wa CHADEMA wanataka kwenda mara Canada, mara Ubelgiji wako wako airport, mara wako Namanga.....ni wanaenda kuchukua pesa zao za mradi wa NO RIFOMU NO ELEKSHENI ambazo zinaingia kwa awamu halafu wewe mtanzania wanakutumia ili ukajaze umati wapige picha wawatumie wazungu wanaowapa fedha hizo.
Hujiulizi Mwenyekiti wa chama ambae ni mwanasheria mkongwe na hata wao wanamtaja kuwa ni mwamba wa sheria Tundu Lissu ni kwa nini alitamka maneno ya "......tutafanya uhaini....." mbele ya vyombo vya habari, au unadhani ile ni siasa tu?
Alitamka vile akijua lazima atakamatwa sababu sheria zetu zinakataza maneno ya aina ile, shida yake akamatwe ili kuipa uzito propozo yao kwa wazungu na hela ziongezeke nyingi zaidi, ukidhani aliongea vile bahati mbaya, umejidanganya mtanzania!
Soma Pia: Rais TLS ampigia chapuo Nkuba Ubunge Kahama Mjini
Ni kwamba kila mtu anaeunga mkono NRNE ndani ya CHADEMA anakula mahala ambapo ana mkate wake, huyu Mwabukusi yeye akienda CHADEMA anasema No Rifomu, akirudi kwa CCM anahamasisha watu waende kwenye uchaguzi yaani ni kama Ronaldo Cr7 wa siasa, anapiga miguu yote na header anaruka nazo pia!
Rudi kafanye kazi, acha kuwa ugali wa wanaharakati biashara wa watanzania.