Tuko kati ya janga,tuwe na moyo wa kishujaa. Hakuna kuhitaji lockdown tuchukue tahadhali kitalaamu

Mnajitekenya na kucheka wenyewe. Tatizo ni huyo juha anayejiona mwenye akili kuliko wenzie wote duniani. Wakati wenzenu - ikiwa pamoja na mabeberu wanaowapa msaada - wakifanya maamuzi magumu, nyie mkafanya mzaha. Mkaleta siasa mahala panapohitaji sayansi. Naona sasa porojo za nyungu zimekufa kifo cha asili. Na hata mfalme juha ameacha kujigamba kuwa "tumeishinda Korona."
 
Kwa hiyo tufanyeje? Limeshatokea la kutokea.
 
Tuko kwenye janga na unakatisha tamaa umma.
Contact tracing unaifanyaje? Watu wangapi wanapima? Vipimo vipo mikoa mingapi hapa nchini? Hapo nakatishaje tamaa umma kwenye mtandao? Population yetu ni say +55m na humu wanaojadili mada na kutoa maoni ni watu wangapi?. Ni vema umekiri tuko kwenye janga. Ingependeza sana tusome mapendekezo ya namna ya kutoka kwenye kanga hilo ndiyo italeta maana zaidi.
 
We pambana na hali yako huko kwa mabeberu. Ya watanzania waachie wenyewe. Kwani kila siku ni Ijumaa!
 
Hufahamu contact tracing ipo vipi? Vipimo ni tatizo?
 
Majibu mbona unayo mwenyewe. Kama ndugu wanamtibu mgonjwa na mpaka mgonjwa ajulikane kuwa kafa kwa covid 19 ameambukiza wangapi? Na kama anazikwa kawaida tu na watu hawachukui tahadhari unadhani wanaambukizwa wangapi? Unawa trace vipi?. Vipimo vya USD 100 wangapi wanaweza? Kitu gani kikuvute ukapime na hofu iliyopo?
 
Sidhani kama serikali ikianza kupima raia wa kawaiba kubaini maambukizi kipimo kitagharimu usd 100. Kitakuwa bure. Nafikiri hili tatizo lipo sasa lakini ufuatiliaji ukianza itakuwa rahisi kutrace maana ni suala la taarifa. Wanalipia usd 100 wanaoenda nje kupata cheti
 
Ninaamini kabisa akisimama kiongozi wa nchi akasema na kuagiza watu wachukue tahadhari hata mtu wa kijijini atavaa barakoa,atanawa, na atahakikisha anakwepa mikusanyiko isiyo ya lazima. Sasa hivi tumegawanyika mno: Kuna wanaodhani haiwahusu hasa vijana. Kuna wanaodhani kuchukua hatua ni kutokuwa na imani na Mungu( si tuliomba mwanzo?). Kuna wanaojaribu kuchukua hatua nao wanaonekana kama watu wa ajabu. Lakini kiongozi akisema " Tuna Janga na siyo kama la mwanzo, tuchukue tahadhari" Utashangaa watu watakavyoitikia mpaka vichochoroni.
 
Ikiandikwa historia sasa sisi tunaungana na Zimbabwe, Malawi na Burundi katika nchi ambazo zimepoteza viongozi wa ngazi mbalimbali za juu kwa janga hili mpaka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…