Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil

Pele alifunga goli mbili ambazo kutokana na uhaba wa teknolojia hazikuwa kurekodiwa kuna hilo vs juve ambapo aliwapiga vidali mabeki 2/3 hiv na kipa nae akala kidali mwanaume akatupia kambani
na kuna jinginr linaitwa gol de la placa hilo hata maradona hakufunga lisake hilo, aliwala vyenga karibia timu pinzani yote.. Inasemekana ndio goli bora kufungwa katika nyasi za maracana.

Kutokana na uhaba wa teknolojia matukio ya pele yaliyowahi kirekodiwa ni 30% tu ya mabalaa yake yote uwanjani
 
Vilaza wangapi wamekatiza mbele ya Ferdinand....usituletee ushit hole kama vile ulikiwa unamwangalia peke yko huyo Ferdinand
 
Naomba kujua kama tangu ujue soka hasa la majuu. Ulishawahi kusikia mchezaji yeyote nafananishwa na Pele?

Utasikia. New Maradona
New Christiano Ronaldo
New Gaucho nk

Huwezi kusikia new pele...
Hana mfano wake sasa, we hushangai hakuna mchezaji anaefananishwa na pele..

Hebu imagine mtu kama aguero vile umpe uwezo wa messi.. Hapo ndio unaweza kumpata ama kupata picha ya mfanano wa pele, anayofanya messi kwa mguu wa kushoto pele alikuwa anafanya kwa mguu wa kulia, halafu kushoto nyongeza kifupi alikuwa anatumia miguu yote, ana nguvu balaa, skills zimelala, mtu wa miaka 50 kweusi alikuwa akipiga rabona, controll uchochoro kontro imelala..

Wewe unamjua pele vizuri wewe..
 
Usibishane na anayempamba Maradona aliyekuwa anataumia dawa za kuongeza nguvu wakati wenzie wakitumia vipaji vyao...kibongo bongo Maradona ni sawa na anayetumia nguvu za giza kutusua huwezi kumfananisha na wanaotumia vichwa vyao kuonesha uwezo wao
 
Na tena 66 bulgaria na portugal walimfanyia faulo, kiasi pele akasusa akasema hatokuja kucheza tena kombe la dunia, la siivyo angechukua na hilo pia.
 

Hujafanya jitihada za kumcheki mkuu, kuna video zinaonesha alivyokuwa anarukiwa miguu, utafikiri lile soka letu la utotoni ikifika muda wa giza kuingia muda wa rafu ndio pele alikuwa anakutana na adha hiyo, utafikiri alikuwa "nyama" kama umecheza mpira utaelewa maana ya nyama.

Hawa masharobaro wenu ndio wangefeli kipindi hicho. Mtu anavutwa jezi anaanguka[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Timu ipi imefungwa tano na imefungwa na nani?? Mbona rekodi inaonyesha Czechslovakia na Hungary zilikuwaga zinawapa watu visago vya saba bila enzi hizo?? Mabeki hao walikiwa wapi??
We hungary ya puskas ulikuwa unaijua wewe, waulize waingereza ndio walijua balaa la huyu mtu
 
Huyu Maradona inavyoelekea hana adabu hata chembe,kuna mwaka alishawahi kuitwa na Rais wa nchi yake Ikulu lkn alikataa kwenda na akasema "siwezi kwenda Ikulu kwa kuwa sijafanya jambo lolote la kijasiri la kumfanya Rais aniite Ikulu" matokeo yake siku aliyopaswa kwenda Ikulu kuonana na Rais yeye alienda Kuonana na Rafiki yake ambaye ni Rais wa Venezuela by then ( Hugo Chavez)
 
Na gwiji wa madrid fundi di stefano.. Na balaa lake lote alikubali pele si wa dunia hii..
 
Mi sijawahi hata kuona clip za huyo Pele ila nikisomaga mambo yake kipindi anacheza soka niki compare na sura na muonekano wake vinaendana na simulizi zake kabisa.....Messi,Ronaldo na Ronaldinho wakali ktk zama zao lkn Pele mkali ktk zama zote za soka zilizopita,zilizopo na zijazo japo,mm ni shabiki wa Zinedine Zidane lkn nasema viva PELE viva.
 
Mkuu makaveli10 Nikubaliane na wewe kwenye eneo moja la tecnology kwa enzi za pele. Hatujaona vodeo nyingi za pele kama ilivyo kwa maradona na kina messi.

Point yangu ipo hapa. Kwa mujibu wa Fifa goal of century ndio bora kabisa ndani ya miaka 100 iliyopita. Hili alifunga Diego Maradona. Hilo mnalosema alifunga Pele dhidi ya juve nani analitaja kuwa goli bora kabisa. Fifa? Waandishi wa habari? Au nani.
 
Kama alikua anacheza na mabeki vilaza miaka hyo ya 60 ataacha kufunga hata goli 10,000???
 
Kama alikua anacheza na mabeki vilaza miaka hyo ya 60 ataacha kufunga hata goli 10,000???
Kama ishu ni competition inakuwaje mtu anayecheza soka ktk zama hizi ambazo unaamini ndo zina ushindani anashinda balon dor 5 na kufunga goli 50+ peke yake...????
 
Mkuu mie pia sikupingi kuwa goli la fundi maradona ndilo goli bora la karne, lakin haimaanishi hakuna magoli mazuri zaidi ya hilo la maradona, nilikuwa nataka nikuoneshe hata pele aishawahi kufunga magoli mazuri hayajawahi kutokea..

Kuna utofauti wa goli bora na goli zur mkuu.. Goli bora linatokana na goli zuri lakin lina msisimko gani, ulimfunga nani, lilikuwa na umuhimu gani, katika pressure ipi ya mchezo,
Ukifatilia hapo kwa umakin utagundua kwanini goli la maradona ni goli bora la karne,
kumbuka messi alifunga goli zuri kama hilo vs getafe sijui osasuna lakin hakuna anaeliongelea lina baki kuwa goli zuri, tena litakumbukwa siku ukimtaja messi, ila ukiongelewa mpira na magoli yake huwez kukumbuka la messi utakumbuka la maradona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…