Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil

Hakuna siku alifunga mawili, moja na kutoka kapa?????[emoji36][emoji36][emoji36]
 
Nimecheki video nyingi sana za pele YouTube lakini nimeona ni mchezaji overrated tu hana lolote.

Hawezi gusa moto wa maradona na Messi.
 
Huyo Pele alitwaa vikombe gani vikubwa upande wa vilabu??
Kwako makombe makubwa ni yapi..

Campeoneto paulista 10
Seria a 6
Copa libertadores 2
International cup 2
Torneio rio sao paulo 4..

Hapo ni santos,

Akaenda kumalizia soka lake marekani baada ya kuombwa kwenda kulitangaza, soka la marekan sizungumzii alivyobeba huko
 
Ni waenga wenzio tu ndio watakuelewa hayo mapambio yako ila sio kizazi hiki cha King Messi.
 
Asante mkuu nimekukubali
 
Hawana akili
Hizi takwimu messi hana hata robo

Kuwa mstaarabu mkuu. Unavyosema hawana akili ndio mojawapo ya sifa!!!!! Naona umekuja na jazba sana baada ya kuona jana kile alichokifanya mfalme, hayo ni kawaida sana kwake ukizingatia anakutana na magreat teams, so ukaona uje umpambe babu yako na kumpigia mafumbo Mfalme sio? Tumia kauli nzuri mkuu, na hayo ni maoni yako tu, usilazimishe na wengine wakufuate unachoamini
 

Upo sahihi kabisa Mkuu. Na evidence ipo na wakibisha nitaileta hapa
 

Upo sahihi kwa %100. Watu mnaoujuwa mpira....
 
Umesahau kipindi Pele anacheza Mpira, faulo ilikua kuanzia kiunoni kuja juu, marefa hawakua wakiwalinda Wachezaji Masuper star kama Leo!
 

Mkuu upo vizuri sana katika kuchambua. Na umeongea true kabisa.

  1. Maradona alipata 53.6%
  2. Pele 18.53%
  3. Roberto bagio wa italy 5.42%
  4. Romario wa brazil 1.69
 
Soka zamani ilikuwa brazil argentina, italy, germany na zote hizi pele kacheza nazo na wenyewe wanakiri zaidi ya wengine kuwa alikuwa kiumbe wa ajabu katika soka

Wakina nani hao wanakiri? Mbona unaweka maneno yako bila ushahidi wowote!!
 
Mkuu upo vizuri sana katika kuchambua. Na umeongea true kabisa.

  1. Maradona alipata 53.6%
  2. Pele 18.53%
  3. Roberto bagio wa italy 5.42%
  4. Romario wa brazil 1.69
Hizo ni za mashabiki vilaza kwa sisi tunaoujua mpira maradona ni namba 3
1 pele
2 messi
 
Wewe na akina nani mnaojuwa mpira??? Sikiliza hayo ni maono yako tu na usiwajumlishe na wengine mkuu.

Messi
Maradona
Pele
De stefano
Zidane n.k
Unaonyesha jinsi usivyoujua mpira ndugu
Mpira ni takwimu kama unazo toa za messi
Toa za maradona
Ili tuone kama wamemzidi Pele au laa
Sasa unaongea bila takwimu hapa nani mwenye akili atakuelewa?
Kwa sisi tunaoujua mpira duniani kwa upande wa soka Pele ni namba 1 mpaka sasa labda tumsubiri mwingine lakini sio messi wala maradona wala yeyote kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…