Mwanamalundi
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,125
- 1,435
Mzee Mwkjj, watanzania siyo wajinga, ni maskini na wasiojiamini! Lakini viongozi wetu ni wajinga wakubwa!
Ukiwa na watu masikini na wasiojiamini halafu wakachagua watu wajinga, combination hiyo inatisha wangu!
Kama aliyosema Prof. Ndulu ndio ukweli wenyewe, nini basi kifanyike?
1. Kampuni yoyote ya Kigeni inayofanya kazi Tanzania lazima isajiliwe kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
2. Kampuni yoyote ya Kigeni inayosjiliwa kufanya fanya kazi Tanzania lazima iwe na account ya benki katika benki za Tanzania na
malipo yote kwa kampuni hiyo yafanywe kupitia accounti ya Tanzania.
3. Ikisha sajiliwa na kuwa na account ya Tanzania ni lazima ijisajili kama mlipa kodi TRA.
4. Itakuwa ni jukumu la TRA kufatilia makampuni yote yaliyosajiliwa kuhakikisha yanalipa kodi kulingana na mapato wayapatayo (Faida), kwa kazi za ujenzi wazifanyazo nchini kwetu.
Tatizo la mikataba mingi ya kimataifa kuna kipengele huwa kinawekwa kwamba kodi zote zitalipwa na client na siyo consultant. Matokeo yake mwenye kazi anamlipia kodi consultant/contractor. Kwa nini, sheria zetu za kodi zimekaaje?
kwamba kuna sheria inayoweza kumfanya mwekezaji aondoke na fedha zote alizochuma Tanzania na inaruhusu remittance iende huko ng'ambo.
kama asilimia 70 ya wakandarasi ni wageni... kuna ugumu gani wa kuhakikisha kuwa mapato wanayopata kiasi kikubwa nacho kinabakia Tanzania? Kwa mfano, tumepewa hizi bilioni 700 na US, sisi tukashangilia; na zimetolewa kwa ajili ya miundo mbinu nk sasa tutakapotaka kuleta mkandarasi na wamarekani wakatuambia tutafute mkandarasi wakwao ina maana when it is all said and done, kiasi kikubwa "tulichopewa" kinarudi Marekani!!
huu ni ujinga.
Fundi Mchundo, nimekusikia vizuri na pointi zako zinakubalika kabisa.
a. Je makampuni ya kigeni yanasimamiwa kwa kiasi gani katika kuendesha biashara zao Tanzania?
b. Je kuna sheria ya namna gani inayohakikisha kuwa menegiment ya kampuni ya kigeni nchini iwe?
c. Je faida wanayoipata Tanzania wanailipia kodi kwa kiasi gani?
d. Je mfumo tulionao sasa unaweza kwa namna yoyote kuboreshwa ili kuhakikisha kuwa mapato yanayopatikana nchini mengi yanabakia nchini pia?
Sidhani kama kuna nchi iliyoendelea ambayo inaacha kampuni ya kigeni kuchukua faida yote na kuipeleka kwao!
Bila shaka Umaskini unatokana na Ujinga..
Hadi siku mtakapo kubali kuwa elimu ndio nguzo kuu ya maendeleo basi tutakesha na Umasikini wetu.
Na hili la kujifunza kiingereza kama ndio elimu dunia tutamezwa vibaya sana...
Naomba nifahamishwe, katika hili suala ni kipi kinachothibitisha ujinga wetu? Kuwa makampuni ya kigeni ndiyo yanayoshikilia sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi ambayo mara nyingi inafadhiliwa na kodi za wananchi wao? Au kuwa wanaremit faida wanayoipata? Au kuna jambo ambalo mimi sijalielewa!
Akili zetu zimedumazwana sera za ukiritimba,tukaingia katika soko huria kama wajinga na tunaendelea kuwa wajinga hadi siku akili zitakapozinduka.Si katika siasa tu bali hata katika uchumi wetu.
Ksumaba ile ileee....haimaliziki hadi generation hii iondoke au atokezee Mkombozi atakayefanya kama Jerry Rawlings kule Ghana.Halafu kipite kipindi cha miaka kama kumi tukiwa chini ya mtu kama Jerry....na ten tuanze kuingia katika enzi za Kufour.hapo tutaweza kuwa Watanzania wenye akili hasa baada ya kupiga deki hizi akili zetu na kusafisha kabisa uoza uliomo ndani yake.
Nilidhani ndugu yangu JK angeweza kuwa smart na kuleta kitu kipya lakini mpaka sasa naona hana will ya kufanya hivyo.
Hali inakuwa ngumu kila kukicha na ahadi za Mheshimiwa hazionekani kutekelezeka.
Kwa nini Kikwete asiwe kama Jerry? Kwa nini Kikwete asiwe kama Nelson Mandela?
Ni kwa sababu ya kasumba ya tangu awali kabisa ambayo inashindikana kuondoka kichwani mwake?Mbona ni mtu ambaye ametembea nchi nyingi tu duniani?
BoT: We`ve no control over earnings by foreign firms
2008-05-09 09:20:15
By Patrick Kisembo
........He cited lack of funding from financial institutions as one of the biggest challenges facing local contractors.
``This is due to the fact that most of the local contractors are small with no tract record and lack collateral to enable them access loans from financial institutions,`` he said..
CRB Registrar Boniface Muhegi admitted that foreign contractors benefited a lot owing to the fact that they were able to access finance, plant and machinery, as well as support, from their home countries or institutions.
Mifano iliyotumika kuonyesha kwamba "sisi ni wajinga" si mizuri. Fundi Mchundo katoa somo tosha sana.
Chukulia mfano uliotolewa wa msaada wa bilioni 700 toka Marekani. Sawa, watajenga barabara makandarasi wa Kimarekani. Sehemu kubwa ya fedha itarudi huko, lakini sisi tutabaki na barabara! Kuna ujinga gani hapo?
Kuna kushangilia maoni kama mpira. Kumpa tenda ya ujenzi mzawa ambaye hana uwezo wa kufanya hiyo kazi ndio kungekuwa ujinga kweli kweli.
It is defeatist to think that we are stupid. We are not. Ukiamini kwamba wewe ni mjinga, basi unaanza kuzorota tu.
Ushabiki wa mawazo hapa, bila kuangalia ukweli, unaweza kuwa dalili ya kuingia kwa ujinga hapa JF (sio nchi nzima).
Mwalimu nadhani neno Ujinga hulielewi maana yake. Ujinga si upumbavu. Upumbavu ni tusi na ujinga ni hali ya kutojua. Ujinga huondolewa kwa mtu kuerevuka au kuelimika. Kila mtu ni mjinga (ignorant) kwa jambo fulani. Sasa mtu ambaye anafanya mambo kana kwamba anajua na wakati anajua kuwa hajui ujinga wake umejificha katika kujifanya anajua.
Sisi ni wajinga kwa sababu hatujui nini kinapaswa, nini kinastahili, na nini tunaweza; na hapa nazungumzia kama Taifa na si mtu mmoja mmoja. Kama tungekuwa tunajua kuna mambo ambayo kamwe tusingeyafanya kwani mtu anayejua hafanyi mambo ya kijinga.
Mjinga is as mjinga does..
Jamani maneno yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja.
Hivi kweli ukimwambia mtu mjinga atakuacha kweli? Sio tusi neno mjinga katika jamii yetu?
Nipeni ka' nusu saa tu nimalizie Big Mac yangu and then ready to go.. ingia kule kwenye Podcast.. and probably will make a link here tu...
kwikwikwiiii....meant to say 'too'? oh...it's friday...
Duh! ebwana leo unawapatia kishenzi watu humu ndani na vi-comebacks vyako. Yaani una-sound kaa mimi vile. Mega kudos!!
Hapana bwana wajinga ni hao tuliowakabidhi kuendesha vyombo vyetu lakini wamesalimu amri kwa hao wazungu.
Naomba nifahamishwe, katika hili suala ni kipi kinachothibitisha ujinga wetu? Kuwa makampuni ya kigeni ndiyo yanayoshikilia sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi ambayo mara nyingi inafadhiliwa na kodi za wananchi wao? Au kuwa wanaremit faida wanayoipata? Au kuna jambo ambalo mimi sijalielewa!