Naona leo unasound kama kijana toka mwambao wa pwani...Anaweza akakukasirikia lakini kwa vile hajui maana yake sahihi. Kuna wakati niliwahi kumsikia Nyerere akijiita mjinga wa baadhi ya mambo. Kwa kujiita hivyo alikuwa hajitukani bali alikuwa anamaanisha hajui kila kitu....
Na ni kweli maneno yanaweza yakawa na maana zaidi ya moja lakini sidhani kama hili la mjinga, ukiangalia muktadha wa jinsi alivyolitumia Mwanakijiji linakuwa ni tusi au neno linalokasirisha.
naangalia mjadala unavyokwenda, ila mwisho wa siku tutakuja kufika kwenye point "je nani katufanya tuwe wajinga hivi?" na hapo sasa ndo nitainuka bila hata kuchaguliwa na nitapiga kelele kwa nguvu zangu zooote "NYERERE"
Hiyo 10% ianaweza kuwa ndio mwanzo wa ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu? vipi kuhusu "naomba chai" kwa traffic police? Au nipe mdogo dogo " nikupeleke utakotaka kwenda" kwa vishuka au "Una shilingi ngapi kama unataka kote" CDInawezekana kabisa hatuna ujinga wowote ule ila viongozi wetu wamejaa ubinafsi wa kutanguliza 10% bila kujali madhara yake kwa taifa; yaani ile chukua chako mapema mentality ndio inayoongoza maamuzi yanayofanyika...
Inawezekana vilevile kuwa Dr. Watson analaumiwa bure...
naangalia mjadala unavyokwenda, ila mwisho wa siku tutakuja kufika kwenye point "je nani katufanya tuwe wajinga hivi?" na hapo sasa ndo nitainuka bila hata kuchaguliwa na nitapiga kelele kwa nguvu zangu zooote "NYERERE"
Si kweli kuwa Nyerere ndo alikuwa chanzo cha ujinga wetu. Tunaasili ya kujibweteka watanzania na waafrika kwa ujumla saana. Ng'ombe utampeleka mtoni kunywa maji lakini huwezi kumlazimisha kunywa hayo maji.Nyerere alitupeleka mtoni. Kila alichokianzisha huyu Mzee kwa manufaa yetu tulikiharibu. Tulizaliana kwa kasi zaidi ya uwezo wa nchi kujenga mashule. Kutokana na ubaguzi wa utoaji elimu wa mkoloni watu walizeeka bila kujua kusoma hata kuandika.Nyerere alianzisha elimu ya watu wazima na Tanzania ikawa moja kati nchi yenye watu wachache wasiojua kusoma na kuandika duniani.
Watanzania tunapenda kutafuta kila kitu mtu wa kulaumu, pengine ni vizuri sasa tujiulize sisi wenyewe tunachangia vipi katika failure ya mambo katika nchi yetu. Tumekuwa watu tusiojali kabisa as if tunaishi katika nchi ya wageni.Tunavurunda kuanzia kuanzia kwenye uchaguzi na then kila kitu tunakiachia kiende automatic, hata kama mambo yanaharibika tunaangalia tu.We dont demend what we think is the best for us and our country.We just wait and complain.
Mwanakijiji kasema kweli nami siku zote nimekuwa nasema sisi ni wajinga.Iweje tukubali kununuliwa kama bidhaa tena kama mafungu ya nyanya magengeni kwa just a T-shirt,Pilau, kimbo,khanga nk.!!!Kama sio umasikini wa akili ni nini!!
Tunabakila kulaumu wanyantuzu wanaomshangilia Chenge wakati sisi tulioko mjini tumeendelea kuchagua wabunge bomu mijini ambao ndo wanakuwa mawaziri maafisadi, tumeshindwa ku-set standard. Sisi wa mjini wenye uelewa kidogo tulitakiwa tuonyeshe mfano, lakini tumekalia vijiwe na Ngwasuma.
Kama tunaweza kutoa TAX holiday kama kivutio kwa makamuni ya Kigeni, kwanini tusitafute njia ya kuwawezesha Makandarasi wazawa ili waweze kushindana na hawa wageni??
Kuna mzungu mmoja alisema " Sisi waafrika tumekalia kulalamika kwa kila jambo,njaa,vita,umasikini nk, na tunakimbilia hifadhi kwa nchi za wazungu,lakini kama ingewezekana tukabadilishana,wao wakaja Afrika sisi tukaenda kwao.Baada ya miaka 10 tungeziharibu nchi zao na kuanza tena kuomba hifadhi huku Afrika.
Leo hii kutoka na ukoloni mjomba wangu akimuona Mzungu au mtu yeyote mweupe anakuwa kama kaona Mungu mdogo.Roho yake inapaparika bila hata kujitambua na atataka kujipendekeza kwake hata kama ni total stranger.Ujinga wa baadhi yetu kudhani kuwa Wazungu ni watu special kuliko sisi na kila wanachokisema ni sawa upo hadi leo.Kiini cha unyonge wetu tunaanzia hapo.
.
Mashoo, I hear you!
Wakati mwingine inabidi uchukue days off na usisome kabisa JF kwa siku tatu hivi kwani unaweza kupasuka kwa hasira na uchungu.
Mara nyingi mimi huikimbia JF siku za weekend ili kusafisha kichwa kwani nikiendelea kupata habari kama hizi kila siku na kuendelea kuona hakuna kinachofanyika naweza kujikuta nimelaza kwa mshtuko wa moyo au nikajikuta nikiwapigia simu hit men wa kirussia watusaidie kupunguza mafisadi nchini (kitu ambacho sio plan yangu kabisaaaaa).
Naomba nifahamishwe, katika hili suala ni kipi kinachothibitisha ujinga wetu? Kuwa makampuni ya kigeni ndiyo yanayoshikilia sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi ambayo mara nyingi inafadhiliwa na kodi za wananchi wao? Au kuwa wanaremit faida wanayoipata? Au kuna jambo ambalo mimi sijalielewa!
..."we mtu mweusi utaweza vipi kushindana na wazungu" Sasa ukiamini mambo hayo hasa ukiwa bado TZ ni rahisi sana kujiona duni mbele ya watu weupe.
Ujinga wetu si ujingwa wa asili bali ni ujinga uliotokana na sera za kikoloni halafu sera za ujamaa na kujitegemea ambazo kusema kweli zilikopiwa kutoka China na Soviet Union na kisha kupestiwa Tanzania.
.Baadhi yetu si wajinga lakini kama majority ni kama wale waliompokea Chenge basi kumbe wote tunaonekana wajinga.huu ndiyo ukweli wenyewe.
Hata siku moja hakuna mtu anayeweza kukufanya mtu uwe Mjinga...Ujinga ni matakwa yetu sisi wenyewe...
Mnyaazi Mungu katuumba sisi sote na akili za kuweza kufikiria umuihimu wa elimu hivyo chanzo cha upataji elimu hiyo ndipo kuna ulemavu mkubwa...
...Kwa mfano ni ujinga wetu kufikiria JK anaweza kusimama dhidi ya Mafisadi hali hawa ndioo waliomweka ktk kiti cha Ikulu..
Kitu ambacho mpaka sasa nashindwa kuelewa kwa sababu hakuna aliyewahi kukijibu kwa kuridhisha ni hiki: Hivi kwa nini sisi watu weusi (au wengi wetu)tunajiona kuwa ni duni mbele ya wazungu? Chanzo chake hasa ni nini? Kwa nini wao mwanzoni wakati wa makutano na Waafrika walikuwa na confidence...waliitoa wapi hiyo confidence? Na kwa nini sisi hatukuwa nayo? Si sote ni binadamu bwana..
Halafu hii tabia ya kutukuza wazungu iko hata kwa watu waliosoma na ambao wameishi na wazungu kwa muda mrefu. Bado watu wanatukuza lugha zao na kudharau wenzao ambao hawazungumzi kizungu (kiingereza) kizuri. Hata humu foramuni watu wanashindana kuandika kiingereza kwa kutumia maneno magumu (ni wazi ktk akili yao wanadhani ni maneno magumu kwa wengine) ili waonekane wanakijua sana kiingereza. Jamani, hivi huku sio kutukuza wazungu kweli? Kwa mfano utasikia...aah jamaa anaongea English nzuri na blah blah nyingine...Raisi wetu akienda kwenye mikutano nchi za nje au akiwa anakutana na viongozi wa nje akichapia kiingereza kidogo..watu wanamshikia bango (ingawa hata hicho kiingereza sio lugha yake ya kwanza). Aaaagh....Ndivyo Tulivyo bana....
According to Genesis 9:2025, Noah began to raise grapes after the flood, and became drunk one day. While drunk, he lay naked in his tent. Ham saw his father naked, and told his brothers Shem and Japheth about it. Shem and Japheth went into the tent with their faces away from him, and covered him. When Noah awoke, he realized what had been done to him, and cursed Canaan, son of Ham, to be the "servant of servants" of Shem and Japheth.[1]