Si kweli kuwa Nyerere ndo alikuwa chanzo cha ujinga wetu. Tunaasili ya kujibweteka watanzania na waafrika kwa ujumla saana. Ng'ombe utampeleka mtoni kunywa maji lakini huwezi kumlazimisha kunywa hayo maji.Nyerere alitupeleka mtoni. Kila alichokianzisha huyu Mzee kwa manufaa yetu tulikiharibu. Tulizaliana kwa kasi zaidi ya uwezo wa nchi kujenga mashule. Kutokana na ubaguzi wa utoaji elimu wa mkoloni watu walizeeka bila kujua kusoma hata kuandika.Nyerere alianzisha elimu ya watu wazima na Tanzania ikawa moja kati nchi yenye watu wachache wasiojua kusoma na kuandika duniani.
Watanzania tunapenda kutafuta kila kitu mtu wa kulaumu, pengine ni vizuri sasa tujiulize sisi wenyewe tunachangia vipi katika failure ya mambo katika nchi yetu. Tumekuwa watu tusiojali kabisa as if tunaishi katika nchi ya wageni.Tunavurunda kuanzia kuanzia kwenye uchaguzi na then kila kitu tunakiachia kiende automatic, hata kama mambo yanaharibika tunaangalia tu.We dont demend what we think is the best for us and our country.We just wait and complain.
Mwanakijiji kasema kweli nami siku zote nimekuwa nasema sisi ni wajinga.Iweje tukubali kununuliwa kama bidhaa tena kama mafungu ya nyanya magengeni kwa just a T-shirt,Pilau, kimbo,khanga nk.!!!Kama sio umasikini wa akili ni nini!!
Tunabakila kulaumu wanyantuzu wanaomshangilia Chenge wakati sisi tulioko mjini tumeendelea kuchagua wabunge bomu mijini ambao ndo wanakuwa mawaziri maafisadi, tumeshindwa ku-set standard. Sisi wa mjini wenye uelewa kidogo tulitakiwa tuonyeshe mfano, lakini tumekalia vijiwe na Ngwasuma.
Kama tunaweza kutoa TAX holiday kama kivutio kwa makamuni ya Kigeni, kwanini tusitafute njia ya kuwawezesha Makandarasi wazawa ili waweze kushindana na hawa wageni??
Kuna mzungu mmoja alisema " Sisi waafrika tumekalia kulalamika kwa kila jambo,njaa,vita,umasikini nk, na tunakimbilia hifadhi kwa nchi za wazungu,lakini kama ingewezekana tukabadilishana,wao wakaja Afrika sisi tukaenda kwao.Baada ya miaka 10 tungeziharibu nchi zao na kuanza tena kuomba hifadhi huku Afrika.