Tukubali tu: Sisi wajinga... (I know, it hurts)

Tukubali tu: Sisi wajinga... (I know, it hurts)

Anaweza akakukasirikia lakini kwa vile hajui maana yake sahihi. Kuna wakati niliwahi kumsikia Nyerere akijiita mjinga wa baadhi ya mambo. Kwa kujiita hivyo alikuwa hajitukani bali alikuwa anamaanisha hajui kila kitu....

Na ni kweli maneno yanaweza yakawa na maana zaidi ya moja lakini sidhani kama hili la mjinga, ukiangalia muktadha wa jinsi alivyolitumia Mwanakijiji linakuwa ni tusi au neno linalokasirisha.
Naona leo unasound kama kijana toka mwambao wa pwani...
Kheeeeee heeeee heeeeeee!
 
Inawezekana kabisa hatuna ujinga wowote ule ila viongozi wetu wamejaa ubinafsi wa kutanguliza 10% bila kujali madhara yake kwa taifa; yaani ile chukua chako mapema mentality ndio inayoongoza maamuzi yanayofanyika...

Inawezekana vilevile kuwa Dr. Watson analaumiwa bure...
 
naangalia mjadala unavyokwenda, ila mwisho wa siku tutakuja kufika kwenye point "je nani katufanya tuwe wajinga hivi?" na hapo sasa ndo nitainuka bila hata kuchaguliwa na nitapiga kelele kwa nguvu zangu zooote "NYERERE"

..ushapiga tayari hiyo kelele,lol!
 
Inawezekana kabisa hatuna ujinga wowote ule ila viongozi wetu wamejaa ubinafsi wa kutanguliza 10% bila kujali madhara yake kwa taifa; yaani ile chukua chako mapema mentality ndio inayoongoza maamuzi yanayofanyika...

Inawezekana vilevile kuwa Dr. Watson analaumiwa bure...
Hiyo 10% ianaweza kuwa ndio mwanzo wa ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu? vipi kuhusu "naomba chai" kwa traffic police? Au nipe mdogo dogo " nikupeleke utakotaka kwenda" kwa vishuka au "Una shilingi ngapi kama unataka kote" CD
"Kama unataka leseni ya duka zungumza vizuri" Madiwani na watendaji wa halmashauri zao... "Mzigo wako unataka utoke lini/hili kontena lazima likaguliwe/bosi kasema hili kontena limezidi uzito"-TRA
 
Kitu kimoja kinachotuunganisha watanzania ni kufurahia pale tunapokoselewa na wakati mwingine hata kutukanwa! Pamoja na uelewa wa Mzee Mwanakijiji na nia yake nzuri katika kuleta hoja hii wengi wetu tunaiona kuwa ni nafasi nyingine ya self flagellation. Wengi(kwa kutoelewa bila shaka) tunachukulia ujinga kuwa ni tusi na ndani ya nafsi yetu tumekubali kuwa ni sehemu ya identity yetu. Kutokana na maandiko yake mengi, sidhani kuwa Mzee mwanakijiji yumo katika kundi hili.

Mimi mfano uliotelewa katika kujenga mada hii sikukubaliana nao kwa kuhofia kuwa inakuwa hijacked kuthibitisha kuwa sisi kiasili ni wajinga. Ujinga ambao mimi ninaweza kukubaliana nao ni ule wa baadhi yetu kuangalia zaidi short term returns na kudharau madhara ya muda mrefu ya miradi mingi( tunashupalia vijisenti badala ya kuangalia athari ya miradi yenyewe! Tumejazana kumkazia macho Chenge na hatujisumbui kuangalia masuala ya mzingira kama yanayojiri Ziwa Natron na Geita). Hatujiulizi kwa nini tunapotangaza kwa nia njema kuuza mashirika yetu ni mara chache wanatokea wawekezaji makini, wanaoeleweka duniani? Tunaishia na makampuni ya kitapeli kutoka uhindini, uarabuni,afrika kusini, ulaya na marekani ambayo kwa kushirikiana na baadhi yetu tulio kwenye diaspora wanakuja kutu'fleece'. Ukiachia biashara ya ulevi, sigara ni wapi tumepata wawekezaji wa maana? Kwenye sekta ya benki wameingia ili kuwahudumia watu wao na kutuacha sisi tupambane na wenzetu wakina Greenland.

Wengi wetu tunasahau kuwa sisi ni moja ya nchi lukuki ambazo zinagombea wawekezaji. Vivutio kama tax-holidays n.k ni silaha inayokubalika katika kampeni hiyo (kwa wenzetu hata majimbo na miji ndani ya nchi inagombea wawekezaji kwa kuweka vivutio kama hivyo na wengine kufikia hatua hata kuwapa mikopo nafuu!). Lakini ili ziweze kufanya kazi ni lazima tuhakikisha kuwa tuna institutions na sheria ambazo zitahakikisha kuwa haki inatendeka kwa pande zote mbili.

Inabidi tujue kuwa kusudi kubwa la bepari ni kupata faida.Ni wajibu wetu basi kuhakikisha kuwa hawa wawekezaji wetu hawatatuharibia mazingira yetu. Sheria kama hizi zinakubalika kwa wawekezaji makini maana wote wanapenda kujenga their green credentials.

Mara nyingi matatizo yetu hayatokani na ujinga bali ni ulafi wa wajanja (wanajiona hivyo) wachache miongoni mwetu.
 
Kule Europe iliwachukua karne 3, ndipo wakazinduka, mijitu kule ulaya kimya!! ila hapa kwetu siku si chache tutakataa tuu, ilimradi tuwe mioyo kama ya ndugu zangu basi haibiwi mtu kitu hapa.
 
naangalia mjadala unavyokwenda, ila mwisho wa siku tutakuja kufika kwenye point "je nani katufanya tuwe wajinga hivi?" na hapo sasa ndo nitainuka bila hata kuchaguliwa na nitapiga kelele kwa nguvu zangu zooote "NYERERE"

Si kweli kuwa Nyerere ndo alikuwa chanzo cha ujinga wetu. Tunaasili ya kujibweteka watanzania na waafrika kwa ujumla saana. Ng'ombe utampeleka mtoni kunywa maji lakini huwezi kumlazimisha kunywa hayo maji.Nyerere alitupeleka mtoni. Kila alichokianzisha huyu Mzee kwa manufaa yetu tulikiharibu. Tulizaliana kwa kasi zaidi ya uwezo wa nchi kujenga mashule. Kutokana na ubaguzi wa utoaji elimu wa mkoloni watu walizeeka bila kujua kusoma hata kuandika.Nyerere alianzisha elimu ya watu wazima na Tanzania ikawa moja kati nchi yenye watu wachache wasiojua kusoma na kuandika duniani.

Watanzania tunapenda kutafuta kila kitu mtu wa kulaumu, pengine ni vizuri sasa tujiulize sisi wenyewe tunachangia vipi katika failure ya mambo katika nchi yetu. Tumekuwa watu tusiojali kabisa as if tunaishi katika nchi ya wageni.Tunavurunda kuanzia kuanzia kwenye uchaguzi na then kila kitu tunakiachia kiende automatic, hata kama mambo yanaharibika tunaangalia tu.We dont demend what we think is the best for us and our country.We just wait and complain.

Mwanakijiji kasema kweli nami siku zote nimekuwa nasema sisi ni wajinga.Iweje tukubali kununuliwa kama bidhaa tena kama mafungu ya nyanya magengeni kwa just a T-shirt,Pilau, kimbo,khanga nk.!!!Kama sio umasikini wa akili ni nini!!
Tunabakila kulaumu wanyantuzu wanaomshangilia Chenge wakati sisi tulioko mjini tumeendelea kuchagua wabunge bomu mijini ambao ndo wanakuwa mawaziri maafisadi, tumeshindwa ku-set standard. Sisi wa mjini wenye uelewa kidogo tulitakiwa tuonyeshe mfano, lakini tumekalia vijiwe na Ngwasuma.

Kama tunaweza kutoa TAX holiday kama kivutio kwa makamuni ya Kigeni, kwanini tusitafute njia ya kuwawezesha Makandarasi wazawa ili waweze kushindana na hawa wageni??

Kuna mzungu mmoja alisema " Sisi waafrika tumekalia kulalamika kwa kila jambo,njaa,vita,umasikini nk, na tunakimbilia hifadhi kwa nchi za wazungu,lakini kama ingewezekana tukabadilishana,wao wakaja Afrika sisi tukaenda kwao.Baada ya miaka 10 tungeziharibu nchi zao na kuanza tena kuomba hifadhi huku Afrika
.
 
Hata siku moja hakuna mtu anayeweza kukufanya mtu uwe Mjinga...Ujinga ni matakwa yetu sisi wenyewe...
Mnyaazi Mungu katuumba sisi sote na akili za kuweza kufikiria umuihimu wa elimu hivyo chanzo cha upataji elimu hiyo ndipo kuna ulemavu mkubwa.
Ujinga sio tusi hata kidogo isipokuwa ni kutokuelewa undani wa kitu wakati tukifikiria ktk nafsi zetu kuwa tunaelewa..
Hata hapa JF tupo wajinga wengi ambao tunafikiria vitu kwa dhana na pengine hata kupendekeza yale yasiyowezekana kulingana na mfumo mzima wa kitu hicho..
Kwa mfano ni ujinga wetu kufikiria JK anaweza kusimama dhidi ya Mafisadi hali hawa ndioo waliomweka ktk kiti cha Ikulu..
Ni ujinga kumtaka Mkapa, Lowassa, Chenge karamagi, Rostam Aziz ajitokeze hadharani kuelezea mali zake wakati ofisi zetu za kodi zina record kamili pia tunazo mahakama zenye madaraka makubwa ktk maswla ya sheria.. Kutangaza mali ulivyoipata sio sheria lakini sisi tunataka kuifanya sheria chini ya mwembe..
Ni ujinga kuona fahari ya fisadi anapoingia nyumbani na mali za wizi, tukasherehekea ushindi bila kufahamu kwamba mali ya serikali ni kodi zetu sisi wenyewe..
Lakini yote haya kama sisi Wadanganyika tutaweza kufahamu undani na taratibu za maswala kama haya (elimu yake) bila shaka tutaufuata na kuwa wapinzani wakubwa..

Nyerere kwa hadhi yake ni sawa na Mtume ambaye katuletea kitabu cha Ujamaa... kitabu ambacho kinasisitiza zaidi sisi tufahamu kuwa mali yote iliyopo ktk ardhi yetu ni mali ya Taifa zima. lakini leo kutokana na mitume wa uongo tumebadilisha mali hiyo kuwa halali ya baadhi viongozi wachache ambao hawakuweka hata senti ya mtaji zaidi ya kukopa benki zetu kwa nguvu ya wadhifa wao... Huu ni ujinga wa kutozingatia yale tuliyofundishwa..
Binafsi wala sina wasiwasi na watu kama Gang Chomba kwani hata Yesu walikuwepo washabiki waliombebesha msalaba na kumtupia mawe wakisema alokuwa akifundisha Ujinga!..
Siku zote mjinga ni yule anayefikiria anajua kumbe hajui na elimu dunia pekee ndiyo mkombozi kwa sababu elimu sio theory tupu bali matumizi ya elimu hiyo yanapokuwa na mafanikio ktk jamii..
Ndio maana unaona siku hizi watu wameingia ktk maswala ya waganga na hizo kamati za Ufundi kuutafuta Utajiri, kutafuta ajira, Mapenzi na kadhalika wakidhani wanafahamu kinachohitajika kufanikiwa...The fact is hawajui kitu na hakuna mtu aliyewabebesha ujinga huo.
NDIVYO TULIVYO ni pamoja na mijumuiko ya imani hizi za kutafuta mchawi..na mchawi hata siku moja hapatiwi dawa toka hospital, shule ama maabala bali kwa mganga mchawi mwingine...
 
Si kweli kuwa Nyerere ndo alikuwa chanzo cha ujinga wetu. Tunaasili ya kujibweteka watanzania na waafrika kwa ujumla saana. Ng'ombe utampeleka mtoni kunywa maji lakini huwezi kumlazimisha kunywa hayo maji.Nyerere alitupeleka mtoni. Kila alichokianzisha huyu Mzee kwa manufaa yetu tulikiharibu. Tulizaliana kwa kasi zaidi ya uwezo wa nchi kujenga mashule. Kutokana na ubaguzi wa utoaji elimu wa mkoloni watu walizeeka bila kujua kusoma hata kuandika.Nyerere alianzisha elimu ya watu wazima na Tanzania ikawa moja kati nchi yenye watu wachache wasiojua kusoma na kuandika duniani.

Watanzania tunapenda kutafuta kila kitu mtu wa kulaumu, pengine ni vizuri sasa tujiulize sisi wenyewe tunachangia vipi katika failure ya mambo katika nchi yetu. Tumekuwa watu tusiojali kabisa as if tunaishi katika nchi ya wageni.Tunavurunda kuanzia kuanzia kwenye uchaguzi na then kila kitu tunakiachia kiende automatic, hata kama mambo yanaharibika tunaangalia tu.We dont demend what we think is the best for us and our country.We just wait and complain.

Mwanakijiji kasema kweli nami siku zote nimekuwa nasema sisi ni wajinga.Iweje tukubali kununuliwa kama bidhaa tena kama mafungu ya nyanya magengeni kwa just a T-shirt,Pilau, kimbo,khanga nk.!!!Kama sio umasikini wa akili ni nini!!
Tunabakila kulaumu wanyantuzu wanaomshangilia Chenge wakati sisi tulioko mjini tumeendelea kuchagua wabunge bomu mijini ambao ndo wanakuwa mawaziri maafisadi, tumeshindwa ku-set standard. Sisi wa mjini wenye uelewa kidogo tulitakiwa tuonyeshe mfano, lakini tumekalia vijiwe na Ngwasuma.

Kama tunaweza kutoa TAX holiday kama kivutio kwa makamuni ya Kigeni, kwanini tusitafute njia ya kuwawezesha Makandarasi wazawa ili waweze kushindana na hawa wageni??

Kuna mzungu mmoja alisema " Sisi waafrika tumekalia kulalamika kwa kila jambo,njaa,vita,umasikini nk, na tunakimbilia hifadhi kwa nchi za wazungu,lakini kama ingewezekana tukabadilishana,wao wakaja Afrika sisi tukaenda kwao.Baada ya miaka 10 tungeziharibu nchi zao na kuanza tena kuomba hifadhi huku Afrika
.

Ujinga wetu si ujingwa wa asili bali ni ujinga uliotokana na sera za kikoloni halafu sera za ujamaa na kujitegemea ambazo kusema kweli zilikopiwa kutoka China na Soviet Union na kisha kupestiwa Tanzania.

Leo hii kutoka na ukoloni mjomba wangu akimuona Mzungu au mtu yeyote mweupe anakuwa kama kaona Mungu mdogo.Roho yake inapaparika bila hata kujitambua na atataka kujipendekeza kwake hata kama ni total stranger.Ujinga wa baadhi yetu kudhani kuwa Wazungu ni watu special kuliko sisi na kila wanachokisema ni sawa upo hadi leo.Kiini cha unyonge wetu tunaanzia hapo.

Ujinga wa pili ni ule tuliouchukua wakati wa utawala wa JK Nyerere.Miaka ile ya ya elimu ya kujitegemea wengi wetu tuliishia kulima mashamba na kuimba nyimbo za kumsifia Baba wa Taifa.Tulikuwa kama waumini wasiohoji imani ila tukamfanya Nyerere kama Kiongozi na nabii.Kasumba ya ujamaa ilijaa mashuleni kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu na itikadi ya Nyerere ikazama kwenye akili zetu.Fikra za Mwenyekiti wa CCM zikawa ndizo dira na Tanzania haikuwa na watu waliokuwa na mawazo yao bali kila kitu kilitoka kwa Kiongozi Mkuu.Ubunifu ukawa haupo na ujinga ukachukua nafasi yake.

Hapo ndipo wenye meno wakaanza kutafuna mashirika ya umma na wakiagundulika kuwa mafisadi wanahamishwa kwenye mashirika mengine au serikalini.Ufisadi haukuanza leo jamani.Kuna ndoa zilizovunjika kwa sababu ya mafisadi wa RTC.Wanyinge wakawa wakijipendekeza kwa miungu wadogo wa mashirika ya umma kama NMC,RTC na kadhalika na ujinga ukazidi kuota mizizi.

Ujinga huu wa kuwaza kwa mtimdo mmoja bila kuacheck upande wapili ndiyo unaotufanya hadi hii tukawa hatuchgui viongozi wa vyma vya ushindani kwa kuwa imani yetu kwa Kiongozi Mkuu na wale makomrediwake si rahisi kutoka vichwani mwetu.Viongozi wenye fikra na mtazamo mpya hawatakiwi.Katika chaguzi tulizozifanya baada ya mfumo wa vyama vingi matokeo yanaonesha kuwa bado maradhi ya ujinga ni makubwa kuliko tunavyoweza kufikiri.Mambo haya hayakuja kwa ajali tu.Ni mambo yaliyo accumulate kwa miaka nenda rudi na sirahisi kuondokana na ujingwa huu kwa hali inavyojionesha.

Sasa wa kumlaumu ni nani kwa ujinga huu tuliyorithishwa na JK Nyerere pole pole kwa miaka 25?

Sisi ni wajinga lakini kuna siku tutaondokana na ujinga.Baadhi yetu si wajinga lakini kama majority ni kama wale waliompokea Chenge basi kumbe wote tunaonekana wajinga.huu ndiyo ukweli wenyewe.
 
Leo hii kutoka na ukoloni mjomba wangu akimuona Mzungu au mtu yeyote mweupe anakuwa kama kaona Mungu mdogo.Roho yake inapaparika bila hata kujitambua na atataka kujipendekeza kwake hata kama ni total stranger.Ujinga wa baadhi yetu kudhani kuwa Wazungu ni watu special kuliko sisi na kila wanachokisema ni sawa upo hadi leo.Kiini cha unyonge wetu tunaanzia hapo.
.

Uncle Ruckus wako wengi sana!

Hili la unyonge wa fikra na rangi, ni kasumba ya kikoloni ambayo ilipandwa na Wamishenari wa kwanza waliokuja Afrika.

Hoja yangu kuhusiana na unyonge wa mwafrika Kihistoria ni kupitia ulaghai na matumizi mabaya ya dini na imani yaliyofanywa na Waingereza, Wajerumani, Wataliano, Wahispania, Wareno, Wafaransa, Wabelgiji na Wadachi ambao walijipatia makoloni katika kila kona ya dunia hii.

Ikiwa mwafrika alipandwa mbegu ya inferiority complex kwa kuambiwa kuwa yeye ni kutoka kizazi cha yule Ham (mtoto wa Nuhu aliyelaaniwa kizazi kwa kumcheka babaye aliyekuwa uchi) ambaye aliambiwa atakuwa mtumishi na mtumwa wa kaka zake, kisha akaambiwa aheshimu dola (mamlaka), alipe kodi (mpeni ya kaisari) na kisha kupoozwa kwa kuambiwa adui mpende, mgeuzie shavu au msamehe 7 x 70 kwa kutumia dini ambayo ni imani, ni rahisi basi kujenga jamii ambayo ilikuwa ni nyonge hata kwa kutumia jina la Bwana.

Lakini kwa kuwa tumeng'amua janja ya mkoloni kutumia dini kututawala, kwa nini tunaendelea kulea side effects?

Wakati Kilimanjaro hotel ilipokuwa inauzwa, Reginald Mengi alijitokeza kama mzabuni aliyetaka kununua hiyo hoteli. Mkapa akaamua kuiza kwa Kempiski ambao walitoa dau dogo kuliko Mengi au ile Kampuni ya Libya.

Je suala ni unyonge huu wa "Uncle Ruckus" kuona Mzungu ni bora?
 
Wengi hapa mnaweza kuwa na experience kama ya kwangu; nilipokuja mara ya kwanza hapa US jamaa zangu walikuwa wananitania kama kuniambia ukweli "huwezi kushinda na wazungu bwana", mara "utakuwa mtu wa mwisho darasani, wazungu wana kila kitu bwana", mara "we mtu mweusi utaweza vipi kushindana na wazungu" Sasa ukiamini mambo hayo hasa ukiwa bado TZ ni rahisi sana kujiona duni mbele ya watu weupe.

Sitashangaa wengi mlipoingia darasani na kusoma na hawa wazungu na ile test ya kwanza ulipasua na kuwa mtu wa kwanza au wa pili, na wazungu kibao wakiwa nyuma yako, it gave you something; confidence and self-respect. Ukaamini kuwa unaweza.

Na pale ulipowekwa kwenye dean Roll ndiyo kabisa ukajua wazungu hawatokutisha tena! Leo hii baadhi yetu tumepata nafasi ya kuwasimamia (supervise) au kuwa manage hawa wazungu katika shughuli mbalimbali, na unagundua kumbe na wao ni binadamu na wana ujinga wao tu.

Hata hivyo, kwa watu wetu wengi hili wazo kuwa wazungu ni binadamu tu na kila walichokipata wamekifanyia kazi kwa jasho na kwa damu inawashangaza.

Msemo wa mababu kuwa " ukiona vyaelea vimeundwa" una upungufu mmoja mkubwa hautuambii kuwa walioviunda walikuwa binadamu. Sisi leo tunataka kufurahia vya kuelea lakini tukiambiwa tunaweza kuviunda tunauliza "wahisani wako wapi".

Hivyo, ndugu zangu katika kuelewa mjadala huu nina uhakika mtauweka katika maudhui (context) ya hoja zangu kuwa kabla ya kuwashinda kwenye sanduku la kura ni lazima tuwashinde kwenye uwanja wa fikra kwanza; kabla hatujaweza kuwashawithi watu kubadili viongozi wao lazima kwanza tuweze kuwashawishi kubadili fikra zao.

Niliandika huko nyuma makala isemayo "Taifa la Watu Duni linajengwaje"?

Hivyo mjadala huu naomba tuuchukulie katika mapana yake na kwa pamoja nina uhakika tutafika ambako nilikusudia tufike kifikra, and yes we are getting there slowly but surely.

A. UJINGA WETU NI WA KWETU WENYEWE!
 
Mwanakijiji,
Tatizo la Ujinga sio elimu ya darasani tu ni pamoja na ukweli kwamba elimu hiyo unaweza kuitumia ktk maisha yako ya kila siku...Ninawafahamu Maprosefa kibao ambao wamechukua elimu ya Kilimo na hawezi kumwelekeza mkulima kwa lugha yake mwenyewe ya Kiswahilii.. Sasa elimu kama hiyo ambayo huwezi kuitumia Afrika nyumbani kwako ina maana gani?..Ujinga mkuu una marefu yasiyopimika..
Tunajifunza maswala ya snow kuwa ndio baraka na mvua imekuwa gharikisho, ktk nchi inayokabiriwa na jangwa!.. Hata utaalam wa miundombinu yetu haikujengwa kukabiliana na hali halisi ya climate yetu isipokuwa ile ya Ulaya tulikopata hizo Phd....
Wapo wengi walioshinda na kuwa wa kwanza darasani lakini inapofikia ktk matumizi ya elimu hiyo ni zero... ndio maana wazungu pamoja na kuwa wengine hawakusoma lakini maisha yao ya kila siku ni darasa kubwa....(Exposure).
Sisi Wabongo pamoja na hizo Phds wapo wengi wasojua hata kutenganisha kati ya Haki (Right) na Previledge...acha mbali kabisa matumizi ya vitu vidogo kama PC.
Kwa hiyo bado mkuu bado sana Elimu ni bahari kuu ilozidi ukubwa wa kufahamu kwetu..Hivyo basi elimu ya darasa tu haitoshi na ndio maana kuna vijiwe kama hivi vya JF ambako kuna mengi huwezi yakuta darsani...
 
Mashoo, I hear you!

Wakati mwingine inabidi uchukue days off na usisome kabisa JF kwa siku tatu hivi kwani unaweza kupasuka kwa hasira na uchungu.

Mara nyingi mimi huikimbia JF siku za weekend ili kusafisha kichwa kwani nikiendelea kupata habari kama hizi kila siku na kuendelea kuona hakuna kinachofanyika naweza kujikuta nimelaza kwa mshtuko wa moyo au nikajikuta nikiwapigia simu hit men wa kirussia watusaidie kupunguza mafisadi nchini (kitu ambacho sio plan yangu kabisaaaaa).

Na huu ndio ukweli halisi hata kwa 'yours truly'
 
Mkandara huo ulikuwa ni mfano mdogo tu; lakini nakubaliana na wewe kabisa kujiamini hakutokani na elimu ya darasani. Kwani baadhi ya watu wanaotufanya tujione duni ni wale wenye ma PHD!!
 
Naomba nifahamishwe, katika hili suala ni kipi kinachothibitisha ujinga wetu? Kuwa makampuni ya kigeni ndiyo yanayoshikilia sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi ambayo mara nyingi inafadhiliwa na kodi za wananchi wao? Au kuwa wanaremit faida wanayoipata? Au kuna jambo ambalo mimi sijalielewa!

Pamoja na mengine, ni kutoweza kujenga uwezo wa vyombo vyetu miaka karibu hamsini baada ya uhuru ili navyo viweze kushindana vizuri na hao wageni.

Hata tunapowapa kazi hao wageni hadi leo hii, hatuhakikishi kuwa watu wetu wanajifunza chochote kutokana na miradi hiyo; kwa hiyo tutaendelea kuwa tegemezi zaidi kwa miaka mingine 50 ijayo!

Hayo makampuni yanayowekeza, hata nyanya, mayai n.k., na hata wapishi wanaletwa toka kwao? (pengine - lakini nadhani unapata hoja yangu).

Wewe fikiria, Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE) ipo - hivi ni makampuni mangapi ya nje yanayofanya kazi hapo nchini yanashiriki hapo ili na sisi wananchi tufaidi?

Kama haya, pamoja na mengineyo si ujinga wetu (viongozi na wanaojiita wasomi) tuuite nini?
 
..."we mtu mweusi utaweza vipi kushindana na wazungu" Sasa ukiamini mambo hayo hasa ukiwa bado TZ ni rahisi sana kujiona duni mbele ya watu weupe.

...nakweli Mkuu Mwkjj ukiamini ujinga, ujinga huo utakufanania mpaka usoni!

Ujinga wetu si ujingwa wa asili bali ni ujinga uliotokana na sera za kikoloni halafu sera za ujamaa na kujitegemea ambazo kusema kweli zilikopiwa kutoka China na Soviet Union na kisha kupestiwa Tanzania.
.Baadhi yetu si wajinga lakini kama majority ni kama wale waliompokea Chenge basi kumbe wote tunaonekana wajinga.huu ndiyo ukweli wenyewe.

...hapana mkuu alnadaby, siku zote naamini kusema ujinga unatokana na fulani ni sawa na kukana Responsibility yako binafsi kutokuwa mjinga, yaani kama vile ndio unauzidisha huo ujinga.

Hata siku moja hakuna mtu anayeweza kukufanya mtu uwe Mjinga...Ujinga ni matakwa yetu sisi wenyewe...
Mnyaazi Mungu katuumba sisi sote na akili za kuweza kufikiria umuihimu wa elimu hivyo chanzo cha upataji elimu hiyo ndipo kuna ulemavu mkubwa...

...Kwa mfano ni ujinga wetu kufikiria JK anaweza kusimama dhidi ya Mafisadi hali hawa ndioo waliomweka ktk kiti cha Ikulu..

...Spot on Mkuu Mkandara! 'tunajisahau'(?) kuwa ni JUKUMU LETU watanzania wenyewe kusimama dhidi ya mafisadi hao, kwa mfano kama alivyotanabahisha Alnadaby ule mfano wa (Mb).Chenge na hata Lowassa kupokelewa kwa shangwe huko jimboni kwake.

Sasa Je, wananchi waamshwe vipi toka katika ujinga huo kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010?,
naamini ni jukumu la kila mmoja wetu, kwa kuanzia hapa JF na haswa viongozi wa upinzani kuwaamsha wananchi wenzetu hasa wale wa vijijini wajue thamani ya kura zao kabla ya chaguzi zijazo, wajue visima vya maji, ujenzi wa shule, zahanati, barabara, zana za kilimo, mbolea na maendeleo yao kwa ujumla ni HAKI YAO, sio Takrima ya kuombea kura, wakijichelewesha wimbo utabakia ule ule kuonekana wapinzani 'wanaibukia' siku za lala salama kupigania RUZUKU!
 
Kitu ambacho mpaka sasa nashindwa kuelewa kwa sababu hakuna aliyewahi kukijibu kwa kuridhisha ni hiki: Hivi kwa nini sisi watu weusi (au wengi wetu)tunajiona kuwa ni duni mbele ya wazungu? Chanzo chake hasa ni nini? Kwa nini wao mwanzoni wakati wa makutano na Waafrika walikuwa na confidence...waliitoa wapi hiyo confidence? Na kwa nini sisi hatukuwa nayo? Si sote ni binadamu bwana..

Halafu hii tabia ya kutukuza wazungu iko hata kwa watu waliosoma na ambao wameishi na wazungu kwa muda mrefu. Bado watu wanatukuza lugha zao na kudharau wenzao ambao hawazungumzi kizungu (kiingereza) kizuri. Hata humu foramuni watu wanashindana kuandika kiingereza kwa kutumia maneno magumu (ni wazi ktk akili yao wanadhani ni maneno magumu kwa wengine) ili waonekane wanakijua sana kiingereza. Jamani, hivi huku sio kutukuza wazungu kweli? Kwa mfano utasikia...aah jamaa anaongea English nzuri na blah blah nyingine...Raisi wetu akienda kwenye mikutano nchi za nje au akiwa anakutana na viongozi wa nje akichapia kiingereza kidogo..watu wanamshikia bango (ingawa hata hicho kiingereza sio lugha yake ya kwanza). Aaaagh....Ndivyo Tulivyo bana....
 
Nyani,

Angalia ndizi isikwame kooni kwa hasira🙄

Tulishapigwa Limbwata na Mkoloni kuwa sisi ni Uzao wa Kaanani, mtoto wa Ham ambaye alipewa laana ya milele na Babu yake Nuhu kuwa tutakuwa watumwa!

According to Genesis 9:20–25, Noah began to raise grapes after the flood, and became drunk one day. While drunk, he lay naked in his tent. Ham saw his father naked, and told his brothers Shem and Japheth about it. Shem and Japheth went into the tent with their faces away from him, and covered him. When Noah awoke, he realized what had been done to him, and cursed Canaan, son of Ham, to be the "servant of servants" of Shem and Japheth.[1]

Tukaambiwa ni laana hizo ndio maana tuna nywele Kipilipili!
 
Back
Top Bottom