Tukubali tukatae, CHADEMA haikuzichanga vema karata zake wakati wa kushughulikia usaliti wa Wabunge 19

Tukubali tukatae, CHADEMA haikuzichanga vema karata zake wakati wa kushughulikia usaliti wa Wabunge 19

paul sylvester

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2020
Posts
3,503
Reaction score
3,499
Tukubali ama tukatae, ukweli ni kwamba, CHADEMA haikuliangalia suala hili la kina Mdee na wenzake Kwa umakini kama chama

Hoja ya kina Mdee ni kwamba! waliapa kulitumikia Taifa kama wabunge wa kuteuliwa kwa sababu ipo barua iliyotoka Kwao CHADEMA yenye Baraka zote ya wao kufanya hivyo!

Ndugu zangu ni kwamba!

Pesa ni Adui wa haki, na kiukweli linapokuja swala la pesa, wenye kubaki salama ni wachache Sana na huenda hata tuliomo humu tusipone,

Tukumbuke, CCM Kwa sasa ni taasisi ambayo kiuchumi iko vizuri kuliko Wakati wowote, na kama kweli inatumia pesa zake kuvunja vunja nguvu za wapinzani wake, maana yake vyama pinzani havihitaji kukurupuka kwenye uamzi wake kushughurikia wale wanaodaiwa wanahongwa na CCM

Katika suala ambalo limehusisha wabunge wanawake kutoka Chama cha CHADEMA na namna ambavyo limeshughulikiwa, kuna dosari, na dosari hizi ndizo zitakazoifanya CCM iendelee kutumia fimbo hiyo kuviua Vyama pinzani hasa Vyama vinavyoibukia kupata umaarufu Kwa sababu ya kushindwa namna nzuri ya kudili na mienendo na Tuhuma hizo kutoka CCM

Ikumbukwe pia kwamba, zimekuwepo tu tuhuma za kuituhumu CCM kuwa inanunua watu!! Kina Tomaso tunaka uthibitisho wa Hilo

Ndiyo, Inawezekana kweli kina Mdee wamekula shere na CCM ili kuhujumu nguvu ya Chama Chao, na kama Hilo limefanyika, ndipo unaiona nguvu ya fedha inavyoweza kuangamiza hata taasisi imara kabisa, na tukumbe kipindi cha nyuma, Pesa hiyohiyo iliweza kununua Chama chote cha Chadema kupitia mgombea mmoja wa Uraisi aliyevumaga sana enzi hizo

Na kama CHADEMA wanataka Chama Chao kipone, basi kinatakiwa kudili na Mbinu hizi mbovu kutoka CCM ili kuweza kukinusuru Chama Chao, ni kudili na kila Aina ya michezo mibovu inayosababisha mvurugano kwa Chama Chao! Ile saini inayodaiwa ni ya katibu mkuu chama, ndio ingelikuwa ni Jambo la kuanza nalo ndipo kina Mdee wafuate!!

Mf. Mdee na wenzake, wanasema, wao wamepewa Baraka zote za kushiriki Bunge Kupitia ofsi ya KM Chadema,

CHADEMA isingedili moja Kwa moja na kina Mdee, badala yake ingedili na huo mfumo uliosababisha kina Mdee waape bungeni!! Yaani wafuatilie Kwanza hiyo saini inayohusishwa Kutokea kwenye ofs za CHADEMA kwamba ilitokea wapi na nani anahusika.

Naamini ingebainika, na kama ingebainika, moja Kwa moja inahusisha Chama cha CCM, CCM tungeidharau watu wengi sana na endapo wangelikumbatia Kwa namna yoyote Ile, wao CCM lingewaletea matatizo makubwa ya kuaminika Kwa wananchi kuhusu swala la kushughurikia Rushwa nchini.

Kilicho fanyika Kwa CHADEMA sasa, ni kujaribu kufunika kidonda Kwa bandage bila dawa yake, bado kina Mdee wengine wataendelea kupigwa pesa humo ndani ya CHADEMA na kuendelea kufukuzwa, Zifedhehesheni Kwanza njia mbovu mnazozituhumu Kutokea CCM.

CHADEMA tujitahidi Sana kudili na mifumo na ujanja ujanja wa CCM kutaka kuuwa Vyama vya Upinzani nchini, na endapo tutakuwa tunadili na tunodhani ni wasaliti tu wa chama, pengine huo mchezo Usiwe na kikomo, Ukiniuliza kwamba kwamba, ni Nani anayeweza kukwepa pesa za CCM zikitumwa hapo chadema, nitakwambia, Ni Lissu pekee ambaye anaweza kuzikwepa angalau Kwa 70% lakini wengine wote, hakuna atakwepa pesa hizo.

Kataeni ubaya unaotengenezwa na CCM na kuushughurikia Kisha kuanika na kutilia mashaka juu ya kile CCM wanawaaminisha wananchi na Dunia kuwa wanashughurikia na kaikomesha Rushwa, mkidhibiti Hilo mtakiponya Chama chenu na Vyama vingine vya upinzani, la sivyo zitaendelea kuwa ni tuhuma tu zisizo na msingi wowote na mtaendelea kutimua wanachama wengine wengi tu hapo kama kweli CCM inacheza mchezo huo.
 
Mbona mnahangaika Sana na CDM badala ya kushughulikia ufisadi ndani ya CCM?

Mnatumia fedha nyingi za walipa kodi maskini kurubuni na kununua watu, afu unaleta porojo!
Tumia Ubongo wako kutawala maamuzi yako mkuu!

Ukiambiwa kuthibitisha sijui utaanzia wapi, Soma Kwanza nilichoandika na uelewe ndipo uniponde

Ni wakati gani unapaswa uthibitishe Jambo bila ya chembe ya Shaka yoyote?
 
....Ukiniuliza Hadi hivi Leo kwamba, ni Nani anayeweza kukwepa pesa za CCM zikitumwa hapo chadema, nitakwambia hivi, Ni Lissu pekee ambaye anaweza kuzikwepa angalau Kwa 70% lakini wengine wote, hakuna atakwepa pesa hizo
Pesa za ccm, eeh?!
Ukiambiwa kuthibitisha sijui utaanzia wapi, Soma Kwanza nilichoandika na uelewe ndipo uniponde
Wewe mleta uzi ndo umebainisha kuwa mnatumia "...pesa za ccm" kurubuni watu ndani ya vyama vingine!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama ulivyosema kudiri na CCM kukomesha mtindo wa kutumia pesa kuua upinzani Ni kazi. wanatumia pesa, wanatumia taasisi za Dora. utaanzia wapi kwa mfano, Takukuru, police, mahakamani au wapi?
 
Hoja yako nimeilewa vizuri na sio Chadema tu hata vyama vingine vya upinzani vijifunze kwenye hili suala. Kama hawatabadilisha jinsi ya kupata wawakilishi wa viti maalum basi wataendelea kuchezewa hizi rafu kila uchaguzi.
 
Mbona mnahangaika Sana na CHADEMA badala ya kushughulikia ufisadi ndani ya CCM?

Mnatumia fedha nyingi za walipa kodi maskini kurubuni na kununua watu, afu unaleta porojo!
We ni mtu usiye stuka ufisadi pia ulioko Chadema mnakoona kuko sawa, wenzenu tulishalionaga kitambo tukafunga mdomo, wewe kama ni mpenzi wa hicho chama pole kwa kutokujua au wewe ni mmojawapo pi.
 
Yeyote atakayeshirikiana na CCM au kuonyesha dalili ya kushirikiana na CCM ni kupiga chini tu, bila kujali ni nani na cheo chake.
Watakao baki hata wakiwa 10 ndio wapinzani wa kweli.

Kama kungekuwa na uwezekano wa ku deal na system ya serikali ambayo ndiyo inawafanya wananchi kama mazezeta, CCM isingekuwa madarakani!
 
Kwahiyo we ulitaka waasi hao wasichukuliwe hatua yo yote kwanza ili kamati kuu idill na mfumo uliowarubuni au?

Huoni kuwaacha bila hatua zo zote ni kubariki uovu wa ccm (watatambulika ni wateule wa chadema huku chadema ikilia kuhujumiwa na hao hao wabaya wao au mi ndo sijakuelewa?

Kuuwacha kwanza hao ni kosa kubwa.
 
Back
Top Bottom