Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,221
- 2,359
Huo ndio ukweli, barua ya 19 Nov 2020 yenye majina ya wateule ilipelekwa na nani? Tunaambiwa ina saini ya KM alisaini kwa idhini ya nani na kama si yeye, fojali hii imefanywa na nani? sioni kiongozi wa Chadema anayehangaika kueleza hili tukawaelewa. Ndio maana tunajiuliza wateule waandamizi 19 waandamane na wapambe wao kwenda Dodoma, bila viongozi na waume zao ambao wengine ni makada wa chama wasijue? Kigogo2014 awe na taarifa viongozi wawe wamelala inawezekanaje hili?